Hizi Fedhea nimezichoka!

Gx 110 utauza nyumba soon
 
Mabasi hayana kikubwa cha kutisha sana.

Wao wanachoweza ni time management.
Hapo uko sahihi ndugu watu wengi wanayaogopa mabasi na wkt mwingine utasikia sijui mzunguko wa tairi ni mkubwa ajabu kweli kweli!
 
We kweli mvivu,mi na ka passo kangu mji kasoro meli to dar natumia masaa 2.30,nyoosha goti hilo,mtu barabara unakuta nyeupe unanyata sasa si lazima upitwe hata na bajaj ndugu
Muongo sana wewe
 
mkuu usijidanganye hivo, bus zinatembea mpaka 120, mara nyingi tu nakua road nafukuzana na hizi sauli na newforce.... unakuta niko 120 na jamaa ananiovateki.

Hii njia ya Mbeya na njia ya Mwanza mabasi naona hayana speed limit,jamaa wanatembea balaa nilijaribu kufukuzana nao nina landcruiser natoka Iringa nakuja Dsm, nafika mpaka 170km/hr ila nikiwapita nikipunguza popote hawa haswa Sauli nikachoka,mtu anaingia Iringa saa saba akitoka Dar asubuh kona zote zile ye anapita na speed zaidi ya 100 dah
 
Kama unafuata sheria na alama za barabarani watakupita tu.
Ila kama unafungu la matrafic, hawawezi kukukuta.
 
Mabasi hayana kikubwa cha kutisha sana.

Wao wanachoweza ni time management.
Hii kauli unaweza kuiongea kwenye miaka ya hivi karibuni.

Lakini kwenye miaka ya nyuma kuipita basi ukiwa na kigari kidogo kisichoeleweka kwenye safari ndefu ilikuwa ni ndoto.

Acheni tochi ziitwe tochi aisee. Na faini zimesaidia.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000 mabasi ya Scania ilikuwa ni moto wa kuotea mbali.

Ila kama unaongelea miaka hii ambayo abiria akiachwa na basi anaikimbiza kwa bodaboda. Vitzi ina overtake basi.😄😄

Miaka ya nyuma ilikuwa ukiona basi (Scania) iko nyuma yako unaipisha mwenyewe. Imagine Dar to Mwanza gari zinaanza kufika saa mbili au tatu. Wachelewaji ni saa sita.
 
Inawezekana kabisa kupitwa na basi kwa sababu wao ni wazoefu wa njia, wanajua matuta yako wapi, traffic huwa wanakaa mara nyingi maeneo gani, hivyo kwenye 50 au no overtake anapita tu akijua eneo hilo halina traffic, pia mabasi ni mazito yanaweza kukata kona akiwa na speed mia kitu ambacho kwa mwenye gari ndogo hawezi, dereva yuko juu kidogo hivyo ana uwezo wa kuona mbali zaidi kulinganisha na gari ndogo hasa kwenye milima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…