KERO Hizi gari za Kakola kwenda Kahama na Kakola kwenda Geita hazifai

KERO Hizi gari za Kakola kwenda Kahama na Kakola kwenda Geita hazifai

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Huko kuna shida tena kubwa mwaka jana kuna gari huwa inakipindia sppend isiyo ya kawaida coster hiyo inaitwa mkono inaongoza kwa kupata ajri na kugonga watu na kuua .

kuhusu malalamishi ya mtoa mada nikweli gari zimechoka sana hasa siti lkn barabara pia ni mbaya sana njia nzuri ni geita to msalala karumwa. Barabara hiyo ndo nzuri japo ni ya vumbi.

Binafsi niliwahi panda nikitokea bugarama kwenda geita ilikuwa majira ya 12 jioni hadi tunafika nyakumbu geita saa5 kasoro.

tumeenda hadi nyarugusu tumeenda kabisa mbele kuna kijij kama kuna njia panda vile tunaambiwa njia haipitiki kule hivo inatubidi turudi tena sijui kuna sehemu inaitwa nyakagwe karibu na geita asee njia ilikuwa mbovu sana na gari nalo bovu siti zimeng'oka halitamaniki aswee kuna sehemu watu wanateseka sana.

cha kushangaza kakola inamgodi mkubwa tu wa dhdhabu pale bukoli kwa mbele kuna mgodi mdogo nao tulikuta watu kibao pale wakifanya shughuli za uchimbaji ukienda hapo nyarugusu ni machimbo ya miaka na miaka lkn barabara ni mbovu ajabu geita ni bonge la mgodi. serkali jaribuni kuangalia eneo hilo. Uchuymi upo vizuri sana anga hizo lkn cha ajabu lami ipo geita pekee kakola pale kuna kipande cha lami hakifiki km3 inachekesha sana
Mbona mkuu nimesema wazi kuwa Barabara ni mbovu au niandike kwa kimombo?
Tunaomba toa ushauriwako mkuu.....traffic wafanyeje ? Wazuie lisiende ? Hapo mtaanza kulalamika tena....unakwepa kusema barabara mbovu......
 
Eneo la Hilo lina uchumi mkubwa, haswa kutokana na rasilimali zake, ikiwa ni pamoja na mgodi wa dhahabu wa Bulyankulu.

Mgodi huu unachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa taifa,ila eneo Hilo ,hakuna ajira na mapato ni madogo kwa wakazi wengi.

Hata hivyo, licha ya kuwa na rasilimali hizi, bado kuna changamoto nyingi zinazoathiri maendeleo ya jamii.

Kilimo cha mpunga ni moja ya shughuli muhimu katika eneo hili, na wakulima wengi hutegemea zao hili kama chanzo chao cha kipato. Hata hivyo, hali ya barabara ni tatizo kubwa.

Barabara za vumbi zinakwamisha usafiri wa mizigo na watu, hali inayosababisha bidhaa kufika kwa wakati na kwa gharama nafuu. Kutokuwepo kwa barabara zilizowekwa lami kunazuia maendeleo zaidi ya kiuchumi na kijamii.

Kuhusu uongozi, ingawa viongozi wote wa eneo hilo ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umaskini bado unashamiri. Hii inaweza kuashiria kukosekana kwa mipango madhubuti ya maendeleo na usimamizi mzuri wa rasilimali.

Wananchi wanahitaji kuona matokeo ya rasilimali wanazozalisha, na hii inahitaji juhudi za pamoja za viongozi na jamii ili kuboresha miundombinu na hali ya maisha kwa ujumla.

Kujenga barabara za lami na kuimarisha huduma za kijamii kungeweza kuboresha uchumi wa eneo hilo na kupunguza umaskini, hivyo kusaidia jamii kufikia maendeleo endelevu.
Uzi ni wa muda kidogo huu kwa sasa wameanza maandalizi ya awali ya kuiwekea lami wanaanzia manzese Kuja kakola
 
BAada ua lami utaona magari mazuri yakija....
Na wewe jichange uweke hata coasyer 59mil hapo uwe msafirishaji ...sio mlalamishi ingia ngomani uchezee
Mkuu kwahiyo sitakiwi kutoa kero zangu? Yaaani wote tuwe wa ndio mzee wakati Kodi nakatwa zaidi ya laki7 kila mwezi hii ni sawa?
 
Nzega coach nmepanda sana hio kwenda Ilogi na Bugarama, gari zile ni Bora ufike mana hata barabara zenyewe ni mbovu .
 
Mkuu unapanda magari gani?monbona kunatataa nzuri tu,au panda nyaunge ferrari pori....
 
asante kiongozi,ni gar gani lina uafadhali kutoka geita to kakola?maana naona wachangiaji wanasema magari ni mabovu na chakavu...ninatarajia kuja huko wiki ijayo
Bedui ipo costa, mengi yapo geita to kahama yanapitia kakola kikubwa ni kwamba huwa haya haribiki njiani ila sit ndo mbovu mimi ni wahuku
 
Back
Top Bottom