yani bora nimesoma hii leo, manake nilikuwa naiona tuuuu naiacha, sasa nimeisoma nimechaka sanaaaaa,
kweli inachekesha sana,
hapo hatujaweka hata fedha!! makaratasi kibao!!
nimekumbuka dadammoja mtanzania alieolewa na mdachi alikuja Tanzania kwa likizo fupi akaibiwa pochi/handbag. Hasara aliopata anajua malipo yake karibu miezi miwili Tz na mingine miwili Holand kuhangaikia alivyopoteza,
makaratasi kibao, hata sijui kwanini alikuwa anatembea nayo,
Mie mwenzenu huwa nahakikisha SINUNUI handbag kubwa kwani nitaijaza tu,
pia huwa weekend naipitia yote kuhakikisha sijaanza kulundika vitu ambavyo nikiibiwa pochi nitahamia polisi na maofisi yote kudai document mpya.
hayo ya vipodozi, ujanja ni kutafuta container ndogo kabisa unakuwa unarefill favourate zako mf perfume, poda na lotion,
Kuna rafiki yangu lazima awe na hivyo vyote ikiwamo kanga nyepesi na mtandio mwepesi (havijazi nafasi) sandals nyembaba sana huwa pia hazichukui nafasi kubwa. (huwa anaenda sana kwenye misiba)
bila kusahau sabuni special (ana alergy)
chupa special ya maji huwa anatumia ile biodisk!