wakuu kuna hizi subwoofer za jbl underseat za kwenye gari ambazo hapa mjini dar es salaam zinauzwa laki mbili, hivi kweli hizi ni jbl Original ama fake? bas hata kama sio original je zinagonga mziki vizuri, bass nzito? wajuzi wa mambo tafadhali
Sijaziona hizo subwoofer lakini kuhusu kama ni original nina wasiwasi kutokana na bei . Kama inauzwa laki 2 na bado muuzaji anapata faida hapo pana alama ya kuuliza kwa sababu original bei yake ilipaswa iwe angalau laki 5.
Pili kuhusu kama zinawajibika vizuri nadhani masikio yako ndio yenye kauli ya mwisho kuhusu hilo. Tafuta fursa usikilize mwenyewe kisha utafanya conclusion.
Labda tungejua ni model gani ingesaidia. Fanya utafiti na utest. Kuwa "made- in-China" hilo pekee halihitimishi juu ya ubora labda jbl wana tawi huko . Lakini kwa bei hiyo labda yawe matoleo ya zamani kidogo.
Kwenye maelezo kuna brand ya JBL alafu humohumo kuna neno subwoofer. Sina cha kusema zaidi ya kukueleza kwamba hayo maneno mawili yakiwa sentensi moja bei haiwezi kuwa 200,000.
Kuhusu ubora sijui, ila kuliko kununua kitu copy ya brand kubwa. Bora ninunue kitu cha brand inayojitafuta ila ni bidhaa original.