Hizi ndio ajira zisizotaka akili wala nguvu nyingi na zinalipa.

Hizi ndio ajira zisizotaka akili wala nguvu nyingi na zinalipa.

samsun

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
7,386
Reaction score
5,965
Hizi ndio ajira zisizotaka akili wala nguvu nyingi,ni kwa kiasi kidogo tu cha mtaji waweza kuanza na ikakulipa mara 5 ya mtaji unaowekeza na kila siku unapata pesa nyingi zisizo na ushindani wala jasho. Unaweza kuwa na mtaji wa 10,000 - 50,000. na ukaianzisha biashara yako.

1.Udalali wa nyumba,viwanja,vyumba na hata magari.

2.Fundi viatu

3.Dobi.

4.Kuuza bidhaa ndogo ndogo stendi.

5.Kuuza matunda kwenye mikusanyiko ya watu.

6.Kutembeza matunda.(wakina mama wengi wanaifanya hii)

7.Upigaji Debe kwenye stendi za mikoa.(kama ubungo au kule Nyegezi Mwanza)

Hizo kazi/biashara zinalipa sana na tena mitaji yake ni midogo na nyingine hazina mtaji ni uchangamfu wako tu.

Haya ongezea na wewe au toa maoni yako.
 
Namba moja ndo angalau inaweza kukutoa kimaisha hizi zingine ni kuchumia tumbo tu ili siku ziende..
 
Namba moja ndo angalau inaweza kukutoa kimaisha hizi zingine ni kuchumia tumbo tu ili siku ziende..
Mimi nilishafanya ufundi viatu asikuambie mtu jamaa wanaingiza pesa kwa siku wanaingiza si chini ya 15,000 - 35,000 isiyoitaji mtaji mkubwa ili mradi awe sehemu yenye pilika nyingi. Na hizo nyingine si mbaya kama bado hujapanga mambo yako kwa siku hukosi 8,000 - 15,000. KUMBUKA HIZI AJIRA SI MBAYA KWA MTU AMBAYE HAJAJUA HAFANYE KITU GANI ILI AISHI.
 
ila ilikufikia mlengo inahitaji nidhamu kubwa sana na pesa maana pesa ya kazi hizo hua ni ndogo ndogo sana.
 
ila ilikufikia mlengo inahitaji nidhamu kubwa sana na pesa maana pesa ya kazi hizo hua ni ndogo ndogo sana.
Mi niliweka benki ilipofika kiasi fulani nikanunua kiwanja kikubwa nikajisahaulisha kama miaka 4 hivi,halafu nikakigawa x 2 nikakiuza kimoja na kile kilichobaki nikajenga na chenji ikabaki nikaongezea mtaji nikabadili biashara sasa hivi niko mbali sana na nina maujuzi kibao.
 
Ebanaaa kuna kusuta hivi vikundi vinalipa sana uswahilini unajiunga nyie mnalipwa kwenda kumsuta mtu mbeya muongo mwizi wa mume wa mtu basi walioibiwa waume wako desperate wanalipa tu
 
Na kitu kizuri, baadhi ya biashara hizo, huna ugomvi na TRA
 
Back
Top Bottom