Hizi ndio barua za mandela alimwandikia winnie akiwa jela

Hizi ndio barua za mandela alimwandikia winnie akiwa jela

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
43,242
Reaction score
60,939
Salamu sana wana CC wote,

Nilisikia hii kitu BBC, nimeitafuta nimepata moja;
Naomba wale wenye barua nyingine waziweke hapa;

Kweli Mzee Mandela alikuwa na mapenzi ya ajabu.

-------------------------------------------------
From a letter dated Oct. 26, 1976:
My dearest Winnie,
I have been fairly successful in putting on a mask behind which I have pined for the family, alone, never rushing for the post when it comes until somebody calls out my name. I also never linger after visits although sometimes the urge to do so becomes quite terrible. I am struggling to suppress my emotions as I write this letter.

I have received only one letter since you were detained, that one dated August 22. I do not know anything about family affairs, such as payment of rent, telephone bills, care of children and their expenses, whether you will get a job when released. As long as I don't hear from you, I will remain worried and dry like a desert.

I recall the Karoo I crossed on several occasions. I saw the desert again in Botswana on my way to and from Africa--endless pits of sand and not a drop of water. I have not had a letter from you. I feel dry like a desert.

Letters from you and the family are like the arrival of summer rains and spring that liven my life and make it enjoyable.

Whenever I write you, I feel that inside physical warmth, that makes me forget all my problems. I become full of love.

 
Huyu Winnie alikua na roho ngumu sana kumbe watu walikua wanamlaumu Mandela tu mara oh ajui kuchapiwa ni siri ya ndani ! Mara bla blah kibao kumbe awakujua. RIP Nelson.
 
Barua zilizoandikwa na aliyekuwa Rais wa
Afrika Kusini Nelson Mandela wakati alipokuwa
miaka 27 gerezani zinaeleza maumivu makali
aliyokuwa akiyasikia alipotenganishwa na
familia yake.
Dondoo za barua hizo, zitakozoanza kuuzwa
siku ya Jumanne, zinaonyesha jinsi alivyokuwa
tafrani wakati mke na watoto wake walipokuwa
wakisumbuliwa na serikali ya ubaguzi wa rangi.
Alimwambia Winnie Mandela alipotumikia
kifungo cha miezi 18 alipotengwa na kufungiwa
katika chumba cha peke yake, " Najihisi
nimelowanishwa kwenye kidonda."
Katika barua kwa watoto wake aliandika, "Kwa
muda mrefu mnaweza kuishi kama yatima."
Nakala za barua nyingi zilikuwa zikiandikwa
katika madafatri ambayo yalitaifishwa na
serikali.
Hatimaye zilirejeshwa kwake na aliyekuwa
askari wa usalama mwaka 2004.
Mwandishi wa kujitegemea anaelezea namna
mume na mke, wanavyojaribu kushikilia familia
yao pamoja huku kukiwa na mtikisiko mkubwa
wa kisiasa na hisia.
Mwaka 1969, aliwaandikia mabinti zake wawili,
Zeni na Zindzi wenye umri wa miaka tisa na
10, wakati wote wawili yeye na mkewe wakiwa
gerezani.
Aliwaambia, " Sasa hamtosherehekea siku za
kuzaliwa wala Krismasi, hamna zawadi au
magauni mapya hamna viatu wala vidude vya
kuchezea watoto."
Katika mwaka huo huo, alizuiwa kuhudhuria
mazishi ya Thembi, mtoto mkubwa wa kiume
miongoni mwa watoto wake wawili katika ndoa
ya mwanzo, aliyefariki dunia kwenye ajali ya
gari akiwa na umri wa miaka 24.
Aliandika, " Nilipoambiwa kwa mara ya kwanza
kuhusu kifo cha mwanangu nilitikisika tangu
juu mpaka chini."
Barua kwa Winnie Mandela mwezi Agosti 1970
inaonyesya hasira kutokana na misukosuko
inayoikumba familia yake.
Uhusiano uliojaa wasiwasi
Barua hizo pia zinaonyesha uhusiano wake na
Winnie Mandela. Mwaka 1976 aliandika
kwamba tatizo lake kubwa ni "kulala bila wewe
kuwa pembeni mwangu na kuamka bila wewe
kuwa karibu yangu, kupita siku bila mimi
kukuona wewe."
Wakati huo, alipandishwa cheo na chama cha
African National Congress kama ishara ya ya
kupambana kwake na ubaguzi wa rangi. Lakini
katika miaka ya kati ya 80 matendo yake
yaliongezeka kuwa na utata na uhusiano wao
ulianza kuleta wasiwasi.
Mwaka 1987, aliandika kwa rafiki yake kuhusu
hasira aliyoonyesha Winnie Mandela
alipomwambia namna watoto wake wawili wa
kike walivyokuwa wakubwa:
"Alinikumbusha:Mimi, si wewe, ndiye
niliyewakuza hawa watoto ambao sasa
unanileza mimi. Nilishtushwa."
Japokuwa alitembea naye sambamba
alipoachiwa huru mwaka 1990, walitengana
mwaka 1992 na kuachana miaka minne ijayo.
Aya kutoka barua hizo zimetolewa kwenye
gazeti la Uingereza, The Sunday Times, na
katika magazeti ya Afrika Kusini.
Zimechapishwa kwenye kitabu, Mazungumzo na
Nafsi yangu, inayojumuisha hifadhi za nyaraka
za kumbukumbu na vitu alivyorekodi
mwenyewe pamoja na barua.
Kutoka dondoo moja kwenye kitabu hicho, ni
wazi kuwa Bw Mandela alianza kuwa
mwangalifu kutokana na kuongezeka kwa
heshima yake katika nyanja za kimataifa wakati
alipokuwa gerezani katika kisiwa cha Robben.
"Jambo moja ambalo lilikuwa likinitia wasiwasi
mno ni sura isiyo sahihi nilioiweka bila kujua
kwa ulimwengu wa nje; wa kuonekana kama
mtakatifu.
"Sijawahi kuwa hivyo," Aliandika !

Maelezo hayo nimeyatoa BBC..
 
na winnie si ndo alikuwa anatoka na mtu mwingine mandela akiwa jela?
 
na winnie si ndo alikuwa anatoka na mtu mwingine mandela akiwa jela?

Ni kweli kabisa yeye kama binadamu asingeweza kukaa miaka yote hiyo bila vitasa, lakini kuna kitu pia hajikawahi kuhojiwa kwa sababu zisizojulikana nacho ni Madiba alianza lini mahusiano na Graca? Ukijaribu kufuatilia kwa makini kuna contradiction kubwa sana kuhusu hilo
 
hii habari ni ya kumbukumbu muhimu, sijui kwa nini mama ameiweka hapa cc.[/QUOTE
Wakati mwingine tunakumbuka mambo matamu kama hizo barua. Na kujiuliza kama miaka hii inaweza kutokea tena
 
Ni kweli kabisa yeye kama binadamu asingeweza kukaa miaka yote hiyo bila vitasa, lakini kuna kitu pia hajikawahi kuhojiwa kwa sababu zisizojulikana nacho ni Madiba alianza lini mahusiano na Graca? Ukijaribu kufuatilia kwa makini kuna contradiction kubwa sana kuhusu hilo


Nakubaliana.
Pengine ni sababu ya winne kuzira na kuchepuka
 
Back
Top Bottom