figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
OVULATION ni hali ya kutoka kwa yai la kike baada ya kukomaa kutoka kwenye follicle baada ya kukua na kukomaa katika ovary. Hali hii hutokea katika hali ya kawaida katika siku ya 14 katika mzunguko wa siku 28.
Alama/dalili hizoza Ovulation si ngumu kuzitambua, iwapoutafahamu unatafuta alama gani. Kunabaadhi ya alama za mwilizinazokutahadharisha kwamba Ovulationiko njiani, hivyo kuweza kukusaidiakupanga vyema muda wa kujamiiana kwaajili ya kupata mimba.
Alama/ dalili nyinginezozinakufahamisha kwamba Ovulationimewadia au imeshapita. Ingawa alama hizoziko nyingi na nitazungumzia baadhi yahizo, lakini usifikiri kwamba unatakiwautumie zote, kwani kufanya hivyo kunawezakukuchanganya.Iwapo hutoona alama zozote za Ovulationau iwapo siku zako za mwezi hazinampangilio maalum, ni bora umuone daktariambaye atakusaidia zaidi.
1.Mabadiliko ya joto lako la MwiliTunaweza kusema kuwa Joto lako la mwiliau (Body Basal Temperature) ndio alama/ dalilimaarufu inayotumiwa na wanawake wengiili kufahamisha kwamba Ovulationimewadia pale wanapotaka kubeba mimba.Hii ni kwa sababu joto lako la mwilihuongezeka kwa kiasi kidogo na huendeleakuongezeka baada ya Ovulation. Ongezekohilo la joto husababishwa na homoni yaprogesterone, ambayo huongezeka sanapunde baada ya Ovulation.
Kwa kujipimajoto lako la mwili na kuandika chati yamabadiliko hayo unaweza kufahamuongezeko hilo la joto lako la mwili. Unahitajia kipimamoto kwa ajili yakufanikisha suala hilo.
Zipo pimajotomaalum kwa ajili hiyo lakini unawezakutumia pimajoto ya kawaida pia. Hakikishaunapima joto la mwili wako asubuhi baadaya kuamka na uhakikishe huna homa,hukukosa usingizi, hukunywa pombe, simgonjwa wala huna wasiwasi na fikranyingi. Ni bora ufanye hivyo kwa mizungukokadhaa ya siku zako ili uweze kuijua vyemachati ya mabadiliko ya joto la mwili kwamujibu wa mzunguko wako wa mwezi.
Ingawa njia hii haiainishi moja kwa mojakuwa Ovulation imewadia, lakini joto lamwili huongezeka kidogo kabla ya kipindihicho na huongezeka kwa kwa degree 0.4hadi 0.6 baada tu ya kumalizika Ovulation.Kuongezeka joto kwa kiasi kikubwa baadaya Ovulation huendelea hadi sikuutakayopata siku zako ambapo hupunguana mzunguko wako wa mwezi huanza tena.Iwapo utakuwa umepata mimba joto lako lamwili litaendelea hivyo hivyo kuwa juu.
Kwakuwa mabadiliko ya joto hutokea wakati waOvulation iwapo unajaribu kubeba mimba,kufuatilia mabadiliko hayo kwa mudausiopungua miezi miwili ni jambo ladharura ili uweze kujua wakati wa Ovulationambapo una uwezekano mkubwa wakubeba mimba.
2.Mabadiliko ya majimaji ya ukeniWakati Ovulation inakaribia majimaji yaukeni hubadilika pia kwa kiasi na hali. Ikiwahakuna Ovulation majimaji ya ukeni huwayanayonata au kama kremu au hukosekanakabisa. Wakati Ovulation inakaribia majimajiya ukeni huongezeka na huwa katika hali yamajimaji na wakati mwingine huwa ranginyeupe kama ya yai bichi.
Iwapo utapimakwa vidole vyako huvutika kwa inchi auzaidi kati ya vidole vyako.Ni bora nikumbushe hapa kwamba, kuangaliawakati unaweza kuwa na majimaji ya ukeniyanayofanana na ya wakati wa Ovulationhali ya kuwa huko katika Ovulation. Hali hiyoni ya kawaida kwa watu wenye PCOS.Kutumia dawa za Clomid au Antihistaminhuweza kufanya majimaji ya ukeni yakaukena hivyo kuwa vigumu kutumia njia hii ilikujua ni zipi siku zennye uwezekanomkubwa wa mimba. Njia hii huhesabiwakuwa yenye itibari zaidi.
3.Ongezeko la MatamanioInaonekana kuwa maumbile nayohutusaidia kujua ni siku gani tunawezakubeba mimba! Wataalamu wameonyesha(jambo ambalo pengine wengiwameshalihisi) kwamba wanawakewanapokuwa katika siku zenye uwezekanomkubwa wa kupata mimba, matamanio yaoya kufanya mapenzi huongezeka. Hizo ni siku chachekabla yakujiri Ovulation, ambapo ndio wakatiunaofaa wa kujamiiana iwapo unatakakubeba mimba.
Hata hivyo njia hii si ya kutumainiwa sanakwani baadhi ya hali kama vilemsongamano wa mawazo, fikra nyingi nawasiwasi huweza kupunguzaa matamanio.Au mtu anaweza akahisi matamanio katikamuda wote wa mzunguko wa mwezi.
4.Mabadiliko ya Ukeni:Kama ambavyo majimaji ya ukeniyanavyobadilika wakati wa Ovulation, ukenao (cervix) hubadilika wakati wa kukaribiaOvulation. Wakati huo uke husogea mbele,huwa laini na hufunguka zaidi.
5.Maumivu kidogo katika Matiti:Baadhi ya wanawake wakati wanapokaribiaOvulation au baada ya hapo matiti yao huwana maumivu kidogo. Suala hili huhusiana namabadiliko ya homini mwili ambazohujitayarisha kwa ajili ya mimba.
Hata hivyonjia hii sio yenye kutegemewa sana kwanimaumivu ya matiti huweza kusababishwana masuala mengine. Pia maumivu ya matitihutokea kabla ya hedhi au baada ya kutumiabaadhi ya dawa za kusaidia uzazi.
Alama/ dalili nyinginezoBaadhi ya wanawake huhisi maumivukidogo ya tumbo ambayo baadhi huyaitaMiddle Pain. Maumivu hayo kwa kawaidahutokea upande ule yai linapotoka yaaniupande wa Ovulation. Maumivu hayohutokana na mwendo wa yai wakatilinapopenya kwenye mirija.
Maumivu hayo siya kuendelea na wala si makubwa na huishaharaka. Hali hiyo huweza kutokea marakadhaa katika siku za Ovulation.Kunabaadhi ya alama kama vile baadhi yawanawake huhisi kichefuchefu, gesi,kukojoa mara kwa mara na maumivu wakatiwa kujamiina, hali ambayo haitokei kwawatu wengi.
Pia kuna baadhi ya vifaavinavyopaatikana katika maduka ya dawakatika baadhi ya nchi ambavyo huwezakukusaidia kujua wakati wako wa Ovuationumewajia, vifaa hivyo hujulikana kama'Ovulation Kit"
La muhimu ni kufahamu kuwa wanawakehutofautiana katika kupata alama hizi,kwani kuna baadhi wanaweza wakapatabaadhi ya alama hizi na wengineo wakapatanyinginezo. Kuuelewa vyema mwili wako nijambo zuri linaloweza kukusaidia kuzijuasiku zako la Ovulation na hivyo kuwezakujua siku zako za kubeba mimba.
Chanzo:Blogspot