Hakika maisha ni vita. Maisha ni mapambano. Mimi pia nimekuwa nikijaribu huku na huku ili kuinua kipato cha familia.
Kazi ya kwanza
Baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo kikuu, nilitafuta kazi kama mwezi mmoja hivi. Mungu mkubwa, mwezi wa pili nilipata kazi kwenye taasis moja binafsi. Nilifanya nao kazi kwa muda wa miaka miwili. Nikawaambia, nilihitaji baadae kuendelea na masomo naomba muda utakapofika wawe wananipa hata nusu mshahara. Nikirudi nitaendelea nao. Wakasema hawana bajeti hiyo. Basi nikatemana nao kiroho safi. Nikasonga mbele.
Kazi ya pili
Baada ya kutemana na mwajiri wangu wa kwanza nikipata kazi taasis moja ya serikali, hapa nilifanya miezi sita tu, nikaomba uhamisho nikaamia shirika lingine. Ambako ndio nafanyia kazi mpaka leo. Miaka miwili baadae nikapata ruhusa ya kwenda masomoni
Biashara.
Nikiwa kwa muajiri wangu wa kwanza, nilifungua duka. Miaka miwili ya mwanzo nilipata faida sana na biashara ilikuwa inakwenda vizuri. Lakini baadae biashara iliyumba baada ya kuanza masomo na kukosa usimamizi mzuri. Nikaamua kuifunga na bidhaa nikauza kwa watu wengine.
Ufugaji wa kuku
Nikafanya ufugaji wa kuku. Nilitoa kama batch nne hivi. Kuku wa faida nzuri kiasi, ila inachukua muda na inahitaji uangalizi na commintment kama zilivyobiashara nyingine. Sikuifanya biashara hii kwa muda mrefu. Ila nitairudia tena.
Uchimbaji wa madini
Jamaa zangu fulani wakanishawishi kufanya Uchimbaji wa dhahabu. Nikawapatia mtaji kama milioni mbili hivi kwa ajili ya kununua miti na kufanya kazi zingine ikiwemo kupiga baruti. Ule mlipuko wa kwanza tu shimo lote likadidimia. Hawakuwa na nguvu tena za kuendelea. Na mimi woga ukaniingia wa kutoa kuendelea na biashara hiyo. Nikakubali hasara.
Kilimo
Kwa sasa ninafanya kilimo cha bustani. Nawatumia ndugu na baadhi ya watu kama wanne hivi wa kuajiri. Ndio nimeanza awamu ya pili. Wacha niendelee nayo kwanza nitakuja kuwapa feedback
Uvuvi
Hii ni kazi nyingine inayolipa. Ndio kwanza nimeianza. Nimemaliza boat na nyavu 60. Natumaini itakwenda vizuri. Hii ndio imekula mtaji mkubwa kuliko biashara yoyote niliyowahi kufanya.
Maono
Natarajia baadae kuanzisha mabwawa ya kufugia samaki na kuinvest zaidi kwenye kilimo.
Changamoto:
Changamoto kubwa ambayo imekuwa ikinikabili ni usimamizi. Bado najaribu kufigure about solution ya hii changamoto. Kwa sababu biashara hizo zinafanyika eneo tofauti na ninapoishi. Sijui kama una ushauri wowote!