Hizi ndio nchi barani Afrika zenye idadi kubwa ya watoto ambao hawapo shuleni (Out Of School Children). Nchi namba 3 itakushangaza!

Hizi ndio nchi barani Afrika zenye idadi kubwa ya watoto ambao hawapo shuleni (Out Of School Children). Nchi namba 3 itakushangaza!

Kanda ya ziwa nazan inaweza kuongoza watoto kutokwenda shule.,..huku shule kwao sio kipaumbele....huku unakutana na pisi kali haijui kusoma wala kuandika...
 
Namba 3 elimu utolewa bure bila malipo kinachowazuia watoto kwenda shule ni nini ?.....
1. Uniform na mahitaji mengine ya elimu kama daftari, kalamu etc.
2. Shule kuwa mbali na makazi.
3. Watoto kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali kama uvuvi, kuchunga ng'ombe n. k
4. Mwamko mdogo wa wazazi na jamii kuhusu elimu
5. Kukosekana kwa walimu na vifaa vya kujifunzia hivyo watoto wanaona ni kama wanapoteza muda wao
 
Tuanze hapa kwanza, Mtoto asiyeenda shule wamesema anaanzia miaka mingapi?
Mtoto huishia miaka 17 na miezi 11.Chekechea huanza miaka minne na tunategemea hadi miaka 17 awepo katika taasisi za elimu zinazomuhusu kiumri au kiuwezo.
 
Mabolozi wa mitaa kwa kushirikiana na TAMISEMI,washirikiane kuhakikisha kila mtaa watoto wa shule wote wanakuwa shule!
Unadhani nini kinachangia uwepo wa hilo tatizo ?
Bila kufahamu mzizi wa tatizo, inawezekana isiwe rahisi kulitatua.
 
Wakuu,

Hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO limetoa ripoti mpya inayoelezea kwa undani idadi ya watoto ambao wanastahili kuwepo shuleni lakini kwa sababu tofauti tofauti hawapo shuleni.

Soma pia: Ukatili unaofanyika kwa watoto wa shule binafsi ya EXPERANCIA (Sengerema)

Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), watoto na vijana milioni 244 wenye umri wa miaka 6 hadi 18 duniani kote bado hawajapata elimu, na takriban shule 14,300 zimefungwa katika nchi 24 za Afrika kufikia Juni 2024 kulingana na Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC).

Ripoti hiyo imezitaja nchi kama Burkina Faso, the Democratic Republic of Congo, Cameroon, Chad, Nigeria na Niger kama nchi zinaozoogoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule huku umasikini ukitajwa kuwa ni sababu kubwa inayopelekea watoto kukosa kwenda shule.

And yes Tanzania pia ipo.

Kulingana na ripoti ya UNESCO hizi ndio nchi zinazoongoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule Afrika:

  • Nigeria – 18.18M
  • Ethiopia – 11.1M
  • Tanzania – 6.42M
  • DR Congo – 6.17M
  • Sudan – 5.6M
  • Niger – 5.5M
  • Uganda – 4.9M
  • Angola – 3.9M
  • Burkina Faso – 3.4M
  • Mali – 3.1M
Source: Business Insider Africa, Unesco

Kwa hiyo hapa Tanzania kuna watoto Milioni 6 hwaendi shule, hawa watoto huwa wanafanya nini huko mitaani kama hawaendi shule? Elimu si bure?
Kwa Tanzania bado sijakubaliana. Watoto wengi sana wanaenda shule, labda effect iwe kuanzia kidato cha kwanza hadi nne hapo yaweza kuwa sahihi. Lakin elimu ya msingi hatuwezi kuwa na idadi hiyo.
 
Kwa Tanzania bado sijakubaliana. Watoto wengi sana wanaenda shule, labda effect iwe kuanzia kidato cha kwanza hadi nne hapo yaweza kuwa sahihi. Lakin elimu ya msingi hatuwezi kuwa na idadi hiyo.
Umezingatia neno "watoto" wakati unasoma?
 
Mtoto huishia miaka 17 na miezi 11.Chekechea huanza miaka minne na tunategemea hadi miaka 17 awepo katika taasisi za elimu zinazomuhusu kiumri au kiuwezo.
Tanzania shule za serikali chekechea ni kuanzia miaka 5. Mpaka hapo kuna hizo takwimu hazija-account for hili sUala..
 
Namba 3 elimu utolewa bure bila malipo kinachowazuia watoto kwenda shule ni nini ?.....
Wanaona bora walime na kufuga na wa mjini kuomba omba. Elimu ingekuwa na mvuto hakuna mtu angelazimishwa kwenda au kupeleka mtoto shule.

Wewe fikiria mtoto wa mfugaji na wa mkulima na wa seremala wote wanafundishwa kilimo cha miwa Cuba. Hakuna tija wanaona bora kuungana na wazazi wao kujifunza kulima au kufuga. Wa omba omba nao wanaungana na wazazi wao kuomba.

Wakikaa kuangalia TV wanaona Rais Kikwete, Katibu mkuu CCM Makamba, Waziri, Riziwan, waziri Januari, Mbunge Salma, Mbunge Nape. Sasa kwanini na wao wasirithishe watoto kazi zao?

Elon Musk hasomeshi watoto katika mfumo wa shule za kawaida. Ana mitaala na shule zake binafsi kwa watoto wake tu.

Sasa kwetu UNESCO wanatupongeza kwa kushika namba 3 wazazi kurithisha watoto kazi zao na kukataa mitaala ya jumla. Hongereni Nigeria kwa kuongoza
 
Sipingi.

Mwezi wa kwanza watoto wataanza form one, shuleni wanaweza report wanafunzi 200, wakifunga mwezi wa 4, wanafunzi 10 hawarudi shuleni. Mpaka wanamaliza form four wanakuwa wanafunzi kuanzia 40-80.

Hii hasa ni kwa shule za vijijini hasa usukumani, sijajua kwa maeneo mengine.
Huko hawaachi!
Kuna mkoa robo ya walioanza form One wanaacha by April; kifika Dec. nusu yao wanazuzrura mtaani.
Kuna sehemu nilidikia Rukwa 30% ya waliosajiliwa darsa la 1 mwaka jana (2023) wameshaacha
 
Wakuu,

Hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO limetoa ripoti mpya inayoelezea kwa undani idadi ya watoto ambao wanastahili kuwepo shuleni lakini kwa sababu tofauti tofauti hawapo shuleni.

Soma pia: Ukatili unaofanyika kwa watoto wa shule binafsi ya EXPERANCIA (Sengerema)

Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), watoto na vijana milioni 244 wenye umri wa miaka 6 hadi 18 duniani kote bado hawajapata elimu, na takriban shule 14,300 zimefungwa katika nchi 24 za Afrika kufikia Juni 2024 kulingana na Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC).

Ripoti hiyo imezitaja nchi kama Burkina Faso, the Democratic Republic of Congo, Cameroon, Chad, Nigeria na Niger kama nchi zinaozoogoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule huku umasikini ukitajwa kuwa ni sababu kubwa inayopelekea watoto kukosa kwenda shule.

And yes Tanzania pia ipo.

Kulingana na ripoti ya UNESCO hizi ndio nchi zinazoongoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule Afrika:

  • Nigeria – 18.18M
  • Ethiopia – 11.1M
  • Tanzania – 6.42M
  • DR Congo – 6.17M
  • Sudan – 5.6M
  • Niger – 5.5M
  • Uganda – 4.9M
  • Angola – 3.9M
  • Burkina Faso – 3.4M
  • Mali – 3.1M
Source: Business Insider Africa, Unesco

Kwa hiyo hapa Tanzania kuna watoto Milioni 6 hwaendi shule, hawa watoto huwa wanafanya nini huko mitaani kama hawaendi shule? Elimu si bure?
Aaah wapi, Tz haipo
 
1. Uniform na mahitaji mengine ya elimu kama daftari, kalamu etc.
2. Shule kuwa mbali na makazi.
3. Watoto kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali kama uvuvi, kuchunga ng'ombe n. k
4. Mwamko mdogo wa wazazi na jamii kuhusu elimu
5. Kukosekana kwa walimu na vifaa vya kujifunzia hivyo watoto wanaona ni kama wanapoteza muda wao
6. Hali duni ya maisha kiasi kwamba nyumbani hakuna msosi, hivyo bora kwenda kibaruani
 
Tanzania watoto wadogo wote wako bize na usanii kukata mauno
Huko ndiko kwenye ndoto zao

Ova
 
Tungekuwa #1 pia nisingeshangaa na tungesema tunaonewa maana masikini huwa wanajifanya yatima
Hao 6.4m ndio wanakuja kuwa madiwani, katibu kata nk
 
Elimu ya darasani kwasasa ni kujifunza Lugha tu basi mengine unakuja kufundishwa na Jamii.
 
I think Ingekuwa kwa percentage ingeonyesha ukubwa/udogo wa tatizo.

Watoto wangapi wanatakiwa kuwa shule na wangapi hawapo shule, ukiweka Hivi for last 5years unajua kama kuna tatizo au hakuna.

Thanks
 
Back
Top Bottom