Hizi ndio nyimbo mbovu ila zinabebwa na media

Madee - Hela ni wimbo mzuri labda kama wewe huna hela ndo unaweza ukachukia
[emoji1] [emoji1] [emoji1] eti kama sina hela...we ni mwanamke so sishangai,wanawake mnapenda manyimbo ya ajabuajabu sana
 
Nilikuwa namheshim mshkaji sana ila huo waya wake umenifanya nimpuuze. Anaimba mambo ya ujinga kwa style za kijinga na kwa sauti na melody za kijinga
Katika ngoma mbovu,hii Joh kazingua sana,ni mbovu kupitiliza
 
sizipendi nyimbo zote za bongo fleva napenda zilipendwa mpaka leo unasikia utamu wa nyimbo hao bongo fleva wakiimba mpaka washike sehemu za siri ndio style yao wanaboa ovyo
 
Wimbo mzuri baada ya ule wa Darasa ni PHONE wa Ben Paul
ni kweli wimbo wa ben paul mzuri .

Anachosema mleta mada ni cha kweli wimbo kama ni mzuri ukipigwa mara ya kwanza uta ujuani mzuri .

Kama ule wa Darasa Too much mi nilisikiliza mara ya kwanza nikaona upo vizuri, nikamuuliza mshikaji wangu nani kaimba akasema darasa nika muuliza darasa huyuhuyu anaezeekea gemuni bila kuwa na hit song kasema ndio yeye nikasema huu amewin
 
wimbo mbovu sana huo, unaweza fananisha na moyo mashine??
Daaah,ila muziki bhana.kila mtu na taste yake.mimi bora hata PHONE kuliko moyo mashine.huwa ikiwa ni redio naisikiliza wakipiga moyo mashine huwa nabadilisha station
 
Mimi huwa naupenda au kuuchukia wimbo kwa mala ya kwanza ninapousikiliza
 
Kila mtu ana chaguo lake aisee...Upande wangu unaweza ukawa m'baya ila kwako ukawa mzuri...nadhani kila msanii ana "Fan base" yake na anaeleweka kile anachokifanya ila upande wa pili lazima wakosoe hata kama Wimbo ni mkali vipi..!!! Na hii ishu sidhani kama itaisha leo kwa maana kuna wale wanaokubali, wanaokataa na wale wa yote sawa(neutral)
 
Waya ni JIMBO BOVU Sana Pamoja na Kuwa na VIDEO Nzuri Lakini AUDIO Ni MBAYA kweli,Joh Rudi kule kwenye Brand.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…