Hizi ndio sababu za Vanessa Mdee kuacha rasmi muziki

sinza pazuri

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
3,344
Reaction score
9,066
Baada ya kelele nyingi za mashabiki wa msanii Vanessa Mdee (V Money) kwa nini amekaa kimya kwa muda mrefu hatimaye atangaza kuachana na tasnia ya muziki akitoa sababu zifuatazo.

Akizungumza kwenye podcast yake amesema.

1. Muziki umekuwa haumlipi kwa muda wote ambao ameufanya.

2. Muziki ulimletea msongo wa mawazo yani depression na anxiety mpaka kufikia kunusulika kufa.

3. Muziki ulimuingiza kwenye ulevi uliopitilia wa kulewa kwa masaa 24 kwa mwaka mzima 2019.

4. Hakuwa na maelewano mazuri na mama yake kwa kuwa hakuwa akipenda V afanye muziki.

5. Muziki ulifanya aishi maisha ya kuigiza na kufurahisha mashabiki huku deep down akijua anaishi maisha yaliyo juu ya uwezo wake.

Hizi ndio sababu zilizofanya aache muziki na kuweka maisha yake kwa Rotimi ambaye anasema kamrudisha kwenye maisha na kazaliwa upya baada ya kukutana naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…