Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Sijasema kwamba TPDF ndio wanalipa mishahara mikubwa kuliko taasisi zote ila nawashangaa wanaosema eti wanajeshi wanalipwa chenji tu, hata hivyo hilo gap siyo kubwa sana kwa sababu private naye ni mwanajeshi anayeanza kazi yani shati tupu tena hiyo ni kwa mwenye elimu ya form four tu ukiwa na elimu zaidi ya hapo kwa cheo hicho hicho maokoto yanaongezeka, ni taasisi chache sana zinazoizidi TPDF ndio maana nikasema kama wanajeshi wanalipwa chenji basi taasisi nyingi za serikali zinalipa chenji tu
 
Duuuh mbona sioni vyuo vikuu kwenye hii list?! Unataka kusema lecturers na maprofesa wetu nao wana njaa kali?![emoji3064][emoji3064]
 
Mkuu una uhakika na hizo salary za JWTZ? Mimi kuna jamaa yangu luteni alinikopa laki 1. Hivi ninavyoongea unaelekea mwezi wa tano story tupu.
Kama hiyo 2.3 ni mshahara wa luteni basi mimi kanizidi zaidi ya laki 9.
Ujue mimi huwa nashangaa kwanini watu wanajudge mishahara ya watu kwa kuangalia maisha yao hili nilishaliongelea sana humu, tunatofautiana mkuu kuna mtu akipokea mshahara wake hana majukumu yoyote wala wategemezi hivyo pesa yote ni yake na kuna mwingine akipokea mshahara ana majukumu mengi na wategemezi wengi hivyo anajikuta pesa yake inaishia huko, kukopa ni kawaida mtumishi kukopa au kulia njaa siyo lazima sababu iwe ni kutokulipwa vizuri kuearn ni jambo moja na kuexpend ni jambo jingine mimi nina mifano ya maluteni ambao wana maisha mazuri kabisa
 
Hao ni Agency, bila shaka salary zitakuwa zipo ki-Agency hivi
Agency mishahara yao inakuwa mizuri mfano mzuri TARURA baada ya kuanzishwa kuwa agency kutoka halmashauri na kusimamiwa madiwani mpaka kuweza kusimama yenyewe mambo yakawa mazuri.

Mfano mhandisi Daraja la pili Tarura anakula 2M+
 
Duuh mimi nimeongelea aviation engineer wa hilo shirika na nina mifano, sijaongelea kada nyingine yoyote mkuu, sasa sijui wewe nani kakukaririsha kuwa mashirika yote yana mishahara ya kawaida tu
Sawa sikupingi mkuu!!
 
Agency mishahara yao inakuwa mizuri mfano mzuri TARURA baada ya kuanzishwa kuwa agency kutoka halmashauri na kusimamiwa madiwani mpaka kuweza kusimama yenyewe mambo yakawa mazuri.

Mfano mhandisi Daraja la pili Tarura anakula 2M+
Nakubali mkuu, Kuna workmate hapa nilikuwa napiganae story, ana ndugu yake engineer ambaye alitoka Halmashauri ya Tunduru kwenda TArura,, Sasa hivi maisha yake yamechange ghafla,, TARURA Kuna maokoto sana
 
Unataka kusema wanatumia TGS E?😂
Najua mishahara yao kama kuna mtu anabisha aje hapa, chukua hii meneja wa pale TAA hamfikii kwa mshahara afisa anayeanza TCRA,TANAPA ,LATRA ,huyo ni meneja na miaka 13 kweny utumishi..

Kweny pesa ni TCAA ila wapo kimya hao jamaa wanapiga pesa hatari ,safari za kutosha ila TAA inafanya kazi kama subsidiary ya TCAA ila TAA ndio ina miaka mingi kweny utumishi kuliko TCAA... Maslahi duni kutwa wanataka kubadili salary scale ila hawana uwezo.

Kwanza wanalipwa kweny mfumo wa utumishi kama watu wa Tamisemi tu ,hwana mpya.
 
Nakubali mkuu, Kuna workmate hapa nilikuwa napiganae story, ana ndugu yake engineer ambaye alitoka Halmashauri ya Tunduru kwenda TArura,, Sasa hivi maisha yake yamechange ghafla,, TARURA Kuna maokoto sana
Sehemu zote kweny kazi za field kuna pesa na utendaji kazi wake ni nzuri kwa vile unakuwa offshore mara nyingi, Tarura trip hata mwezi unaenda hapo kama per diem taasisi nyingi sasa zimepanda mpaka 240k -250k acha tu .
 
Lete ushahidi
 
Tarura kutamu sana... Kipindi cha nyuma walikuwa hawana ishu mishahara ilikuwa kama tamisemi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…