Hizi ndio zinazodaiwa kuwa sifa za Watu waliozaliwa Mwezi Oktoba

Hizi ndio zinazodaiwa kuwa sifa za Watu waliozaliwa Mwezi Oktoba

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Wanaidawa kuwa na upendo, huwa maarufu sana, ni watu watulivu, wenye amani na pia wanasifika kuwa na uvumilivu

Inadaiwa Watu hawa huwa na mtazamo chanya wa mambo na hivyo huwafanya kuwa werevu na Washauri wazuri. Huwa ni watu wanaojitahidi kufikia malengo yao bila kujali changamoto au vikwazo wanavyokutanana navyo

Watu hawa ni wanaoamini katika Haki na Usawa, hii inawafanya wanaaminika kuwa wana uwezo wa kutatua migogoro

Baadhi ya Watu maarufu kutoka Tanzania waliozaliwa mwezi wa Oktoba ni pamoja na Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Awamu ya 5 wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli na aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Hayati Maalim Seif Sharif Hamad

Wengine ni Wanamuziki maarufu Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' , Mwanasiasa Anna Tibaijuka na Mcheza Mpira, Simon Msuva

Je kuna Ukweli Gani kuhusu Tabia hizi?
 
Back
Top Bottom