Hizi ndiyo njia rahisi zaidi kuingia Marekani, Ulaya na Asia

Hizi ndiyo njia rahisi zaidi kuingia Marekani, Ulaya na Asia

Forgotten

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,518
Reaction score
10,839
Habari wana-JF!

Najua tayari kuna nyuzi kedekede kuhusu njia za kufika Marekani, Ulaya na Asia kwaajili ya kubadili upepo na kutafuta fursa mpya ila leo nitaongezea maarifa hasa kwa wale wanaojipanga kutoka nje ya mipaka ya Tanzania na Africa kwa ujumla.

Nitaanza kuweka njia rahisi za kuingia Marekani, wenyewe wanapaita 'KIWANJA'

NOTE: Njia rahisi zaidi ndiyo zina ushindani mkubwa.

1. Green Card Lottery
Hii wengi wanaijua, kwa wasiojua njia hii: kwa wale wahitimu wenye elimu; kuanzia kidato cha sita, wanayo nafasi ya kucheza bahati nasibu kushinda 'Green Card' inayomuwezesha raia wa kigeni kuishi, kufanya kazi na kupata haki kama raia wa Marekani. Njia hii ni rahisi vilevile ni ngumu maana utahitaji bahati, pesa na mwenyeji wa kukupokea nchini Marekani kama ukishinda. Ushindani ni mkubwa sana hivyo nafasi ya kushinda ni karibu zaidi na 0 kuliko 1.

2. Seasonal Jobs w/ H-2A, H-2B Visa Sponsorship
Hii njia nayo inaonekana kama rahisi ila ni ngumu pia. Kuingia Kiwanja kwa njia za halali haijawahi kuwa kazi rahisi. Hizi ni kazi za msimu: Winter, summer, nyingi huwa ni kazi za mashambani na ujira wake ni mdogo ila kwa atakayeweza kupata atapata nafasi ya kuingia Marekani na kufanya kazi mpaka mwaka 1 na baada ya hapo atatakiwa kurudi nchi aliyotoka. Sasa hapa vijana wa mjini huwa baada ya mwaka hawarudi, wenyewe wanaita 'KUJIONGEZA' ukishaingia ardhi ya Biden unatafuta mbinu itakayokufanya ubaki kihalali Marekani: wengi huwa wanaingia kwenye ndoa ili kupata tu makaratasi.

Sasa tuhamie Ulaya, hapo juu sijaweka njia ya elimu/shule kwasababu wengi wanaotaka kuondoka ardhi ya mtu mweusi hizo fedha za ada hawana.

1. Finland: Vocational School
Kama mnavyojua Finland Vocational School ni bure. Kwa mliokuwa hamjui leo mmejua. Hii ndiyo njia rahisi zaidi kuingia Ulaya ila pia ni ngumu kwasababu ina ushindani mkubwa maana nafasi ni chache. Hapa utahitaji tu elimu ya Form 4, pesa ya kujikimu, uwe umefanya English test: Duolingo, umri kuanzia 18, CV, Passport au National ID wakati wa application.

Vocational School zinazotoa fursa hii kwa International Students ni: Vamia & Riviera. Zipo nyingine pia ila hizi ndiyo maarufu zaidi. Wanatoa course mbalimbali: Cook, Waiter/Waitress na Mechanical fitter. Hapa unaweza kuchagua yoyote tu kama njia ya kuingia Finland na uzuri ni kwamba utapata fursa ya kufanya kazi part time ukiwa unaendelea na masomo. Ugumu upo kwenye kupata nafasi hiyo maana ni bahati nasibu, application inayofuata ya Vamia itakuwa December na iliyofanyika May ndani ya saa 1 walishapata application 500 ambazo ndiyo limit yao baada ya hapo huwezi kutuma maombi tena na katika mchujo wanachaguliwa watu 20-25. Ukishakuwa selected unathibitisha unao uwezo wa kujikimu ukiwa masomoni na utapewa Resident Permit.

2. Portugal: D7 & Digital Nomad Visa
Najua nchi kama Ureno siyo chaguo la wengi kwasababu ya uchumi wao ila ndiyo nchi nyepesi kwa sasa Ulaya kuingia kama salio lako la benki limenona.

D7 Visa, hii ni kwa wale wenye passive income, ni wachache wenye hizo passive income. Ila kwa wanaotumia njia hii wanahitaji bank statement yenye €9,840 na kwa mwezi uwe unaingiza €820. So, kama una michongo kama biashara zinazoingiza pesa hiyo unaweza kuingia kupitia njia hiyo na baada ya miezi 4 unaweza kuomba permit itakayokuwezesha kufanya kazi na baada ya miaka 5 ya kuishi Portugal unaweza kuomba uraia.

Digital Nomad Visa, hii ni expensive na kwa wale waliojiajiri au wanaofanya kazi na waajiri nje ya Ureno. Utahitajika kuthibitisha unafanya kazi remotely na kipato chako ni €3,280 kwa mwezi. Fasta tu Ureno wanakugongea Visa ya kuingia nchini kwao.

3. Svalbard, Norway
Rahisi sana kuingia ila kupata kazi na kuishi ndiyo shughuli ilipo. Svalbard ni kisiwa kilichopo Norway, ndiyo sehemu pekee Duniani raia wa nchi yoyote anaweza kuishi na kufanya kazi bila Visa. Ila, kufika huko itakubidi upitie Norway/Schengen Area kwahiyo ni lazima upate Schengen Visa kama Tourist ndiyo ufike Svalbard. Hili ni eneo la kitalii zaidi kwahiyo kazi zake nyingi ni za kitalii maana ni eneo lenye barafu na baridi kali zaidi na maajabu ya aina yake: ikiwemo jua kuwaka masaa yote 24 kwa karibu nusu mwaka na giza totoro kwa masaa yote 24 karibu nusu mwaka. Eneo hili Dubu weupe ni wengi kuliko watu.

Kabla ya kwenda ni vizuri kufanya jitihada za kupata kazi ndiyo uanze safari au kama unataka kucheza kamari andaa pesa ya kukuwezesha kuishi hata mwezi kama mtalii halafu ukifika huko ndiyo uitafute kazi "good luck with that". Nyumba za kuishi huwezi kupata kwasababu uhitaji ni mkubwa na zote zinamilikiwa na makampuni hivyo ukipata kazi ni jukumu la muajiri kukupatia makazi. Hivyo ukienda kama mtalii utapaswa kuishi kwenye hotel mpaka utakapopata kazi. Ila kuishi Svalbard haihesabiki kama ukazi wa Norway hivyo siyo njia ya kupata uraia wa Norway.

Sasa tuende Asia, njia hii inahitaji pesa pia ni ngumu.

1. Japan: Language School
Watu wengi wanatumia hii njia kupata ukazi wa Japan maana gharama zake ni afadhali zaidi kuliko kujiunga na elimu ya chuo kikuu kwa fani mbalimbali. Hapa utakachohitaji ni pesa za ada, makazi na kujikimu. Hapa utahitaji $20,000 mpaka $25,000 kukamilisha mission hii ya mwaka.

Utatuma maombi ya kujiunga na chuo cha lugha ya Ki-Japan, vipo vingi tu na ukikubaliwa taratibu za Visa zitafuata. Shule zao nyingi za lugha zinatoa hostels ambazo ni affordable kwa 'mwananchi wa kawaida'. Ukishakamilisha taratibu zote ukiingia Japan ni shule inaanza baada ya mwaka kuisha hapa ndiyo watoto wa mjini wanafanya yao: katika huo mwaka unatakiwa kuhakikisha umeshajua unabaki vipi Japan, ukimaliza masomo utapata kibali cha kutafuta ajira ila itakubidi uwe unakijua Ki-Japan vizuri, sasa watoto wa mjini huwa hawa-bet akishachora ramani yake kabla hajatoa mguu ardhi ya baba na mama anahakikisha anakijua Ki-Japan shule anaenda kuchukua karatasi tu baada ya mwaka huyoo anajitosa kwenye ajira.

NOTE: Uzi huu umetoa mwanga tu, yapo mengi ya kujua kwa kila nchi. Kabla hujachagua njia ya kupita fanya kwanza utafiti kujua utahitaji nini kabla ya kuomba Visa na baada ya kufika huko itakubidi ufanye nini kwa kipindi cha muda gani.

Ni hayo tu, ciao!
 
Eeh Chifu mi nina mwanangu alikuwa anapambana na haya mambo ya GL card miaka nenda rudi anapoteza muda tuu but baadae aliamua kufanyia kazi vitu vyote muhimu

Nowdays yupo somewhere ana surf tuu na wala makato ya tanesko hayamuhusu😂😂😂😂
Wewe vipi ume give up mkuu? Mimi naamini tu one day yes do or die
 
Hii hapa njia rahisi
Tuma maombi ya viza ya Mexico hapa nchini, ni kama kumsukuma mlevi
Keko hata mimi naweza kupanga chumba
1720043156257.png

Ukifika Mexico, ulizia La Bestia ikimaanisha The Beast, ambayo inajulikana kama the Train of Death(Treni ya Wafu)
Hiyo inakupeleka mpaka mji wa Ciudad Juárez katika jimbo la Chihuahua, hapo ni makao makuu ya Sinaloa cartel au watwana wao New Generation (or CJNG) cartels.
1720043040025.png




Hao watakununua kama bidhaa na kukuuza kwa wandigwa wanaiitwa Coyote(Mbweha), hawa wanajua chochoro zote mpaka kukufikisha US

1720044246956.png
 

Attachments

  • 1720043533277.png
    1720043533277.png
    274.9 KB · Views: 36
  • 1720043576872.png
    1720043576872.png
    315.9 KB · Views: 43
Hii hapa njia rahisi
Tuma maombi ya viza ya Mexico hapa nchini, ni kama kumsukuma mlevi
Keko hata mimi naweza kupanga chumba
View attachment 3032892
Ukifika Mexico, ulizia La Bestia ikimaanisha The Beast, ambayo inajulikana kama the Train of Death(Treni ya Wafu)
Hiyo inakupeleka mpaka mji wa Ciudad Juárez katika jimbo la Chihuahua, hapo ni makao makuu ya Sinaloa cartel au watwana wao New Generation (or CJNG) cartels.
View attachment 3032891



Hao watakununua kama bidhaa na kukuuza kwa wandigwa wanaiitwa Coyote(Mbweha), hawa wanajua chochoro zote mpaka kukufikisha US

View attachment 3032903
Sasa hizi ndio nondo sasa....Lete vitu mzee tukajipige huko
 
Back
Top Bottom