HIZI NDIZO FAIDA NA HASARA ZA KUSAHAU

Akilidebe

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2018
Posts
204
Reaction score
124
Kusahau ni changamoto kwa watu wengi sana.

Kwa sababu ya kusahau 🙁hasara)
-wanafunzi na wanavyuo wanakesha kujisomea. Kama kungekua Hakuna kusahu basi ingewezekana kusoma chekechea hadi chuo kikuu kwa mwaka mmoja.

-watu wanapoteza uaminifu. Kwasababu wanasahau kufanya jambo la msingi.

-watu wanapoteza pesa nyingi (mtu kulipa mara mbili, wengine kusahau walipo ziweka.

-Ugomvi ndani ya ndoa (mke kusahu alichotakiwa kufanya au kuagizwa na Mume wake, mke/mume kusahau kufuta message za mchepuko.

Na hasara nyinginezo ambazo pengine umekumbana nazo.


Lakini kusahau kuna faida
-ingekuaje leo una uchungu uleule (yaani hujasahau) kifo cha mama au baba yako, pengine rafiki yako mpendwa.

-ingekuaje mwanamke alietoka leba kuwa na uchungu na maumivu yaleyale kila siku, je atafikiria kujifungua tena?

-je ungekua na uchungu wa kuachwa au kumizwa na mme, mke au mpenzi wako hadi wakati huu ungeweza kuwa na amani??

Je ungeweza kumsamehe rafiki ako aliekukosea, au mwanao?? Kama ungekua na uchungu hadi leo??

Je wanandoa wangeishije kama wasingekua na uwezo wa kusahau makosa wanyofanyiana??

MUNGU ANA KUSUDI KWA KILA JAMBO
 
Kuna kusoma, kuelewa, na kukumbuka / kusahau. Tafakari.
 
Hapo kwenye msg za michepuko panagharimu wengi, kuaahau kufuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…