Hizi Ndizo Faida Tano Za Kuwekeza Kwenye Mifuko Ya Pamoja....

Hizi Ndizo Faida Tano Za Kuwekeza Kwenye Mifuko Ya Pamoja....

Mwakawasila

Member
Joined
Oct 23, 2024
Posts
39
Reaction score
68
Mfuko wa uwekezaji wa pamoja
ni aina ya kampuni ambayo
inajishughulisha na uwekezaji ambapo kampuni inakusanya pesa
kutoka kwa wawekezaji wakubwa na wadogo na kuwekezwa kitaalamu chini ya uangalizi wa meneja wa kampuni hiyo,

Hizo fedha zinawekezwa maeneo ambayo yataleta faida,

Wanaweza kuwekeza kwenye HISA zinazofanya vizuri sokoni, Kwenye Hatifungani za serikali au za makampuni , au kwenye bank , na wanaweza wekeza kwenye Real estate,

Mfano wa mifuko ya pamoja Kuna UTTAMIS, SANLAM, INTRUST, TIMIZA FUND, INUKA FUND, M-WEKEZA, FAIDA FUND,.

Hii ni mifuko ambayo unaweza weka pesa yako na ikakuzalishia

FAIDA ZA KUWEKEZA KWENYE MIFUKO YA PAMOJA


👉Meneja mwenye uelewa na uwekezaji,
Kama ukitaka kuwekeza wewe mwenyewe katika hisa lazima uwe na

uelewa na masuala ya hisa, jinsi gani ya kuchagua kampuni ya

kuwekeza na jinsi gani ya kukabiliana na hatari za uwekezaji, muda
gani sahihi wa kuwekeza na mambo kadha wa kadha.

Lakini Meneja wa mifuko anafanya Kwa ajili yako,

👉Ukwasi ((liquidity)

Moja kati ya vitu ambavyo utaipenda Mifuko ya pamoja ni urahisi wa
kununua na kuuza vipande,

kama umewekeza katika hisa utafahamu ya
kuwa ili uweze kununua hisa lazima awepo mtu wa kukuuzia na
kama hakuna mtu wa kukuuzia hisa basi hauwezi kununua.

Pili, kama unataka kuuza hisa lazima awepo mteja wa kununua na
mara kadhaa nimeona watu wanakaa na hisa miezi bila kupata
mtu wa kununua hisa zao

Lakini kwenye mifuko kama UTTAMIS, TIMIZA FUND ni rahisi sana

👉Uwekezaji mseto

Uwekezaji mseto unapunguza hatari za uwekezaji kwani
unakuta mfuko umewekeza katika hisa mbali mbali

na sio hisa tu
bali katika hati fungani, hivyo
hupunguza
hasara

ambayo
inayoweza
kujitokeza
kama
mfuko unakuwa umewekeza sehemu moja au kwenye uwekezaji wa
aina moja,

👉Faida shindani (competitive return)

Ukitaka kuwekeza pesa benki ili upate riba ndani ya mwaka mmoja
sio kitu cha ajabu ukapokea riba ya 3%

au kama utataka upate riba
kubwa basi lazima uwe na
kiasi kikubwa cha pesa ila ukiwa na MFUKO wa pamoja

kwa kiasi kidogo
tu unaweza kupata faida nzuri ya 12%,13% Hadi 15%

ambayo hauwezi kuipata benki
huku ukiwa na uwekezaji mdogo.

👉Kiasi kidogo cha mtaji

Ukitaka kuwekeza katika hati fungani ya serikali ya muda mrefu
kima cha chini ambacho unatakiwa kuwa nacho ni TSH 1,000,000
milioni

na kama unataka kuwekezakatika hatifungani za muda
mfupi basi kiasi ambacho unatakiwa kuwa nacho ni 500,000 laki tano za
kitanzania ila kupitia Mifuko unaweza Anza na 1000, Hadi 10,000 unaweza kuwekeza kwa kiasi kidogo. cha mtaji, na ukapata faida

Coach MWAKAWASILA je niwekeze wapi Kato ya HISA, Hatifungani au kwenye Mifuko ya pamoja??

Sehemu zote nzuri kwa kuwekeza,
Jambo la muhimu angalia malengo yako ya Kifedha,

Ukizingatia malengo ya muda,

Lakini angalia sehemu ambayo unaielewa,

Elimu ni muhimu kabla ya kuwekeza,

Msaada zaidi 0744980339 whatsap
 
Back
Top Bottom