Mada inahusika. Kwa maoni yangu hizi ni hoja na Karama
HOJA
1. Msimamo wa wazi wa hatma ya Zanzibar yenye mamlaka kamili au muungano wa usawa
2. Kudumisha umoja wa kitaifa na kuilinda serikali ya GNU
3. Kuitii Katiba ya Zanzibar na kupigania Maslahi ya wazanzibari katika mazingira yoyote.
4. Kupambana na rushwa, ufisadi na upendeleo wa kivyama, ujimbo na udugu.
5. Kuifungua Zanzibar kiuchumi na kufungua fursa za ajira za kijiografia ikiwemo milango ya bahari na utalii
6. Kuondoa uzembe makazini, kujuana na kubebana kisiasa.
7. Kufumua mifumo ya ufisadi na mianya ya kisheria inayowakingia kifua wabadhirifu.
8. Kufumua mfumo wa uajiri wa kibaguzi uliopo na kutoa fursa kwa wataalamu hasa vijana
9. N.K.
KARAMA
1. Mtu ambaye hatiliwi shaka na umma wa wazanzibari (anayependwa na wazanzibari)
2. Mtu wa watu, muadilifu, mkweli na mwenye misimamo isiyoyumba
3. Mwenye historia ya uzalendo wa kweli kwa Zanzibar
4. Asiyefungwa na makondo kando ya uenevu, chuki, itikadi na milengo ambayo kwa sasa wazanzibari wanaihusisha na kupotea mamlaka ya Zanzibar
5. Mwenye historia ya mapambano ya kweli ya kudai haki ya Zanzibar kwenye awamu tofauti tofauti
6. Jasiri na shupavu.
7. Awe ameishi na wazanzibari kwa jua na mvua
8. Asiye fisadi na tamaa, na asiyefungamana na mfumo wa ufisadi na ubadhirifu unaopigiuwa kelele kwa sasa.
9. Anayekubalika maeneo yote Zanzibar (Wazanzibari wana vigezo vyao) vimejificha. (Uzanzibari. Mila desturi, nidhamu n.k)
10. Mwenye kujitoa kwa maslahi ya Zanzibar (mifano na ushahidi unahitajika)
Hizo ni baadhi ya hoja na karama ambazo mgombea yoyote kwa Zanzibar atapimwa na kuchekechwa.
Hapa nakusudia wananchi na sio DOLA.
Kishada