Hizi ndizo sababu zinazonifanya nishupaze mishipa ya shingo kuwa Yanga itachukua kombe mbele ya mwarabu (USM ALGER)

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Sitochoka kutokwa na povu na kushupaza mishipa ya shingo Tena kwa kujiamini kwa asilimia Mia kuwa Yanga itachukua kombe mbele ya mwarabu( USMA ALGER).

Mosi, ushindi wa Yanga (nje na ndani) Kila nikikumbuka azizi key alivyowalaza na viatu wale waarabu kule Tunia, na Yanga ilivyopata matokeo Nigeria na Nyumbani kwa Tp Mazembe Nina Kila sababu ya kuvimba kuwa Yanga atachukua kombe.

Pili, the big brain coacher (BBC) huyu namzungumzia Prof Nabi hakika ni mwamba kabisa akishirikiana na benchi lake la ufundi hakika Sina mashaka na mbinu zake za kumkabili mpinzani, kupitia Prof Nabi acha nivimbe nakushupaza shingo kuwa Yanga watachukua kombe.

Tatu, video analyst Kuna mwamba yupo pale yanga anachambua video yupo bize mno huyu mwamba wachambuzi wamemsahau hakika ni bonge la mwamba na Nina uhakika kabisa USM ALGER wameshachambuliwa na nondo kapewa Prof Nabbi amalize kazi.

Nne, Hamasa kubwa kutoka kwa viongozi wa serikali na viongozi wa timu kwa mashabiki, hakika kwa mkapa hapatatosha hatumwi mtu dukani
Mashabiki wa wydad wamehamia kwa mkapa hii itawapa morali wachezaji kuwafurahisa mashibiki, Nina Imani kubwa sana kuwa wachezaji hawatowaangusha mashabiki watakao jaa kwa mkapa.

Tano, uwepo wa wachezaji wenye uzoefu ndani ya kikosi Cha yanga.
Nikimtazama Bernad Morrison,Djuma shabani Aziz kii, Mayele Diara nk.
Hakika moyo wangu unafarijika sana nakuona kwamba Yanga kukosa kombe ni kujitakia tu.

Kila la heri Yanga na Kila la heri Mashabiki wa Yanga ndani ya East Africa.
 
Jambo la kutia moyo ni kwamba, USM Alger wanafungika ugenini! Na wanajitahidi sana kujitutumua wakiwa kwao.

Hivyo Yanga wanatakiwa kuitumia vizuri mechi ya kesho kwa kupata ushindi mnono, ili kuwawekea hao wapinzani wao mlima mrefu wa kupanda kwenye mechi ya marudio.

Lakini pia ikumbukwe mwaka 2015 katika fainali kama hizi, walifungwa jumla ya magoli 4-1 na Tp Mazembe! Hivyo hawana maajabu kivile.

Imagine kwenye hatua ya makundi walishika nafasi ya 2 nyuma ya Marumo Gallants!! So Yanga washindwe wenyewe kuchukua huu ubingwa. Maana ukizilinganisha hizi timu mbili; hamasa kwenye timu ya Yanga iko juu kuliko hao USM Alger.
 
Mimi nasikitika na Aucho tu, nimeingiwa na hofu na hii mechi.
 
NAKAZIA [emoji123]
 
Back
Top Bottom