Hizi ndizo sifa za kugombea nafasi za uongozi TFF, Karia kakosa ipi?

Hizi ndizo sifa za kugombea nafasi za uongozi TFF, Karia kakosa ipi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
Zifuatazo ni sifa za wagombea ndani ya TFF.

1. Awe raia wa Tanzania.
2. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha Elimu ya Sekondari).

3. Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.

4. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.

5. Awe na umri angalau miaka 25.

6. Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.

7. Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.

8. anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

KWA HISANI YA MICHUZI BLOG!
 
Hiyo namba 6 ingeboreshwa kwa kuondoa hiyo sentensi yote inayoanzia na au........

Hiyo sentensi ndiyo imekuwa kichaka cha wahuni kama akina Jamal Malinzi, Michael Wambura na Wallace Karia kujimilikisha TFF! Badala ya wachezaji wastaafu kama ilivyokuwa enzi za rais Leodgar Chilla Tenga.
 
Zifuatazo ni sifa za wagombea ndani ya TFF.

1. Awe raia wa Tanzania.
2. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha Elimu ya Sekondari).

3. Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.

4. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.

5. Awe na umri angalau miaka 25.

6. Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.

7. Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.

8. anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

KWA HISANI YA MICHUZI BLOG!
Namba 7, ni kinara wa rushwa.
 
Kwa namna Karia alivyopanga watu wake huko kwenye vyama vya michezo na mikoani, sio wa kuondoka leo wala kesho. Ni mpaka Mungu au serikali iingilie kati!

Uhuru waliopewa vyama mpira wa kutoingiliwa na serikali kwenye majukumu yao unatumiwa vibaya kujenga himaya za kishetani! Dawa ni kumuandama mtu binafsi kwa uchunguzi wa kijinai!
Kama si hivyo, Malinzi na Wambura wangekuwepo mpaka leo!
 
Labda anabebwa na kitengo lakini sidhani kama yeye mwenyewe ni mtu wa kitengo.

Nakumbuka jinsi kitengo walivyopambana kumtoa Muhidin Ndolanga.
Huyo karia ametoka kuwa ded uko mvomero mpaka kuwa rais wa tff unadhani hilo limetokea bahati mbaya, amekosa sifa namba 3, na 6 na bado ghafla tu amefika hapo ulitakiwa ujiulize hiyo nguvu ameipata wapi?.
 
Back
Top Bottom