Hizi ndizo silaha/sumu 10 za kikemikali hatari zaidi duniani

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
10- BZ au 3-Quinuclidinyl benzilate

Hii ni silaha ya kikemikali iliyogunduliwa na Wanasayansi wa Kimarekani miaka ya 1960. Sumu hii inakumbukwa kwa kuwaangamiza mamia ya Wapiganaji wa jeshi la Ukombozi nchini Vietinam maarufu kama Viet Cong

Dalili: Kizunguzungu, kupoteza mawasiliano katika mfumo wa fahamu, kutapika, kukauka kinywa, macho kupoteza uono, kuchanganyikiwa, nk.

stufftoblowyourmind-23-2013-12-BZ.jpg

===

9- Mustard Gas

Wataalam wanasema kuwa sumu ya kikemikali si lazima ifanye mauaji ili iheshimike bali inaweza kuleta madhara mengine kwa walengwa.

Silaha hii hutegwa kwa walengwa kwa masaa 24 kabla ya kuanza kufanya kazi na wakati wa vita ilitumika kutegwa kwenye mahandaki ya jeshi pinzani na matokeo yake huonekana baada ya saa 24 kupita. Sumu hii inaweza isisababishe vifo lakini utendaji kazi wa jeshi pinzani hukosekana kwakuwa hubaki kwenye mwili wa mlengwa kwa wiki 2 zaidi

Dalili: Ngozi kuwaka moto, maumivu ya macho, macho kuvimba, kutokwa machozi, kuwa na hali ya kuukwepa mwanga wa jua, macho kupoteza uono kwa muda fulani, chafya mfululizo, kutokwa kamasi, kutokwa damu puani, kukosa hewa, maumivu ya mwili, kuharisha, homa, kukohoa, kutapika, nk.

stufftoblowyourmind-23-2013-12-mustardgas.jpg

===

8- Ricin

Jina la silaha hii limetokana na mme aina ya Ricinus communis. Sumu hii pia imegunduliwa na Wamarekani, aidha sumu hii ilipigwa marufuku The Hague Convention mwaka 1899.

Sumu hii haifanyi kazi kwa harasa sana kwani huchukua masaa 4 hadi 24 kuanza kufanya kazi. Miligramu 1 tu ni hatari sana endapo itavutwa na walengwa

Dalili: Kuharibika kwa mfumo wa hewa, homa, kikohozi, mafua, kifua kubana, shinikizo la damu, kutapika, kuharisha damu, kiu kikuu cha maji, kuharibika kwa mawasiliano kati ya ubondo na uti wa mgongo, nk.

stufftoblowyourmind-23-2013-12-ricin.jpg

===

7- Chlorine Gas

Ebu jaribu kufikiri silaha/sumu inayoleta madhara hata kwa wale walipiga. Wanahistoria wanasema kuwa silaha hii ilitumika katika mapigano ya Ypres mwaka 1915, Wajerumani wanakumbukwa kwa kuziangamiza Divisheni 2 za Jeshi la Ufaransa na Algeria kwa kutumia sumu/silaha hii.

Dalili: Macho kukosa uoni, ngozi kubanduka, macho kuwaka moto, koo kuwaka moto, pua kuwaka moto, kikohozi, kupumua kwa shida, kichefuchefu, mapafu kuvimba, kutapika, kutokwa machozi, nk

stufftoblowyourmind-23-2013-12-chlorinegas.jpg

===

6- Phosgene Gas(COCl2)

Hii inatajwa kuwa ndio silaha ya kikemikali iliyouwa watu wengi zaidi wa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Dalili:
Kikohozi, macho kuwaka moto, koo kuwaka moto, macho kutokwa machozi, macho kupoteza uoni, kupumua kwa shida, kichefuchefu, kutapika, mapafu kuvimba, shinikizo la damu, fizi kuvimba na kujaa usaa, moyo kushindwa kufanya kazi.

stufftoblowyourmind-23-2013-12-phosgenegas.jpg

===

5- Sarin

Hii ni moja ya silaha zinazowekwa kwenye orodha ya sumu za kikemikali zilizopewa jina la Nerve agents silaha hii hushambulia mwili kwa haraka na kwa upekee sana. Hushambulia mfumo wa mawasiliano kati ya viungo vya mwili na ubongo

Sumu hii husababisha kifo ndani ya sekunde chache sana na kimiminika chake hakina rangi, harufu wala radha. Silaha/sumu hii iligunduliwa na wanasayansi wa Ujerumani mwaka 1938 ikiwa ni katika kile kizazi cha sumu hatari aina ya G-Series. Hata hivyo USSR na Marekani zilitengeneza sumu hii pia.

Mwaka 1988 aliyekuwa Mtawala wa Iraq, Saddam Hussein aliitumia kuwaua Wakurdi 5,000 katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo kijiji cha Halabja

Hivi karibuni sumu hii ilitumika kuua watu zaidi ya 1,500(Wanaume, Wanawake na Watoto) katika mapigano yanayoendelea Syria.

Dalili: Kamasi zisizokoma, machozi yasiyokoma, maumivu ya macho, macho kupoteza uono, kutokwa udenda, kutokwa jasho, kikohozi, kifua kubana, kupumua kwa haraka, kuharisha, kichefuchefu, kutapika, kukojoa kuliko pitiliza, kuchanganyikiwa, kukosa nguvu, maumivu ya kichwa, shinikizo la damu, kupoteza fahamu, kupooza, nk.

stufftoblowyourmind-23-2013-12-sarin.jpg

===

4- Soman

Hii ni sumu/silaha ya tatu katika kizazi cha Nerve Agent au G-Series, sumu hii hatari iligunduliwa na Mkemia wa Kijerumani, Richard Kuhn mnamo mwaka 1944 ikiwa ni muda mfupi tangu atunukiwe tuzo ya Nobel katika masuala ya Kemia

Sumu hii ilitumika kupoteza maisha ya maelfu ya watu wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Dalili: Kamasi zisizokoma, machozi yasiyokoma, maumivu ya macho, macho kupoteza uono, kutokwa udenda, kutokwa jasho, kikohozi, kifua kubana, kupumua kwa haraka, kuharisha, kichefuchefu, kutapika, kukojoa kuliko pitiliza, kuchanganyikiwa, kukosa nguvu, maumivu ya kichwa, shinikizo la damu, kupoteza fahamu, kupooza, nk.

stufftoblowyourmind-23-2013-12-soman.jpg

===

3- Cyclosarin

Sumu hii ni muendelezo wa Nerve Agent katika kizazi cha G-Series. Sumu hii inafanana kila kitu na Nerve Agent nyingine lakini hii ni rahisi kuing'amua ingawa pia haina rangi wala haina harufu

Dalili: Kamasi zisizokoma, machozi yasiyokoma, maumivu ya macho, macho kupoteza uono, kutokwa udenda, kutokwa jasho, kikohozi, kifua kubana, kupumua kwa haraka, kuharisha, kichefuchefu, kutapika, kukojoa kuliko pitiliza, kuchanganyikiwa, kukosa nguvu, maumivu ya kichwa, shinikizo la damu, kupoteza fahamu, kupooza, nk.

stufftoblowyourmind-23-2013-12-Cyclosarin.jpg

===

2- VX

Hii nayo ni Nerve Agent lakini katika kizazi cha V-Series na sio G-Series. Sumu hii iligunduliwa na Wanasayansiwa Uingereza miaka ya 1950 na ilipofika mwaka 1958 waingereza walilazimika kuwapa fumula yake Wamarekani ili na wao wapewe ujuzi wa masula ya Nyuklia.

USSR hawakua nyuma kwani na wao walitengeneza sumu kama hii (V-Series) na kuiweka katika orodha ya silaha wanazozimiliki

Sumu hii inaua kwa haraka mara 10 zaidi ya Sarin(nimeielezea hapo juu).

> Kwa siku za hivi karibuni sumu hii ilitumika kuondoa uhai wa Kim Jong Nam Kaka yake Kiongozi wa Taifa la Korea Kaskazini, Kim Jong Un

Dalili: Kamasi zisizokoma, machozi yasiyokoma, maumivu ya macho, macho kupoteza uono, kutokwa udenda, kutokwa jasho, kikohozi, kifua kubana, kupumua kwa haraka, kuharisha, kichefuchefu, kutapika, kukojoa kuliko pitiliza, kuchanganyikiwa, kukosa nguvu, maumivu ya kichwa, shinikizo la damu, kupoteza fahamu, kupooza, nk.

stufftoblowyourmind-23-2013-12-VX.jpg

===

1- Novichoks

Sumu hii ni hatari zaidi ulimwenguni, inatajwa kuua kwa haraka zaidi kuliko sumu nyingi na mara 5 zaidi ya VX.

Sumu hii ni ugunduzi wa Warusi, ikiwa na maana ya 'Mgeni' huku ukiwa ni ugunduzi wake Vil Mirzayanov na alianza kutumika miaka ya 1980.

Sumu/silaha hii imeleta mzozo mkubwa hivi sasa ulimwenguni katika ya Uingereza na Washirika wake dhidi ya Urusi, baada ya Waingereza kuwatuhumu Warusi kujaribu kumuua Shushushu wao Sergei Viktorovich Skripal pamoja na Binti yake Yulia. Skripal pia aliwahi kuwa afisa usalama wa Urusi

Dalili: Kamasi zisizokoma, machozi yasiyokoma, maumivu ya macho, macho kupoteza uono, kutokwa udenda, kutokwa jasho, kikohozi, kifua kubana, kupumua kwa haraka, kuharisha, kichefuchefu, kutapika, kukojoa kuliko pitiliza, kuchanganyikiwa, kukosa nguvu, maumivu ya kichwa, shinikizo la damu, kupoteza fahamu, kupooza, nk.

stufftoblowyourmind-23-2013-12-Novichok.jpg

===

Ahsante!
 
Mpaka Leo bado hizo siraha zinatumika?
 
Mkuu hebu ifatilie na BOTOX uijue vizuri!.. size ya ukucha tu ikitumika dunia nzima chali!.
 
aisee....its very interesting ingawa inatishia kidogo amani ya dunia kwa kweli........
 
Botox ndio sumu hatari duniani gramu 4 tu inatosha kutumaliza dunia nzima.
 
Matusi sumu

Haya matusi sumu yanagunduliwa na wanawake waliolewa kwenye karne hii wakishirikiana na mama zao unaweza kutukanwa ukadhani mademu zako wanakuchangia kumbe mama na mwana wameshauriana ujinga

Dalili.kuwa mlevi wa kupindukia,macho kutoka machozi hovyo,kushinda njaa,kususia nyumba, dalili hizi automatic zinampa nafsi adui yako kuomba taraka kuolewa na njemba kama hukujiandaa utaachwa umehang kama bembea
 
Nadhani hii haijawekwa kwasababu hutumika kama dawa pia
Botox-class H ndio Malaika Izrael alipojificha!..hizo nyingine zinaweza tumika hadi kumpalaralyze mtu tu!.
 
Back
Top Bottom