mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Hizi ni baadhi tu za maneno ya hekima ya mzee wa msoga.
1. Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako
2. Kelele za chura hazimzuii mtu kuteka maji
Karibuni tuongezee zingine ikiwezekana tuweke na mazingira/context ambapo jkauli hizo zilitoka. kwa mfano kauli ya "akili ya kuambiwa changanya ya kwako" ilitoka wakati akiwaasa wafanyakazi wasimsikilize kiongozi wa TUCTA alipokuwa anawahamasisha kuanzisha mgomo wakishinikiza kuongezeka kwa kima cha chini cha mshahara.
Mzee wa msoga atabakia kuwa kipenzi cha wafanyakazi maana katika kipindi chake karibuni kila mwaka kulikuwa na ongezeko la mshahara na walimu wote waliokuwa wanamaliza vyuo walikuwa wanaajiriwa. watu husema mnyonge mnyongeni lakini haki nyake apewe! Namtakia mzee wa msoga maisha marefu yenye amani na fanaka!!