Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Katika ulimwengu wa biashara kuna fursa nyingi ambazo mtu aweza kuzitumia ili kupiga hatua maishani.Baadhi ya mbinu hizo ni pamoja na hizi hapa chini:
Ili kufanya kazi vizuri kama Muuzaji katika maeneo haya yote unahitaji kuwa na sifa zifuatazo.
- Kuwa reseller wa huduma au bidhaa.Katika eneo hilo unaweza kununua bidha kwa bei ya jumla na kuuza kwa bei ya rejareja kulingana na mtaji.Ila pia unaweza ukafanya kazi yakutafuta wateja na kupeleka katika ofisi au biashara ya mtu kwa makubaliano maalum.Katika eneo hili kuna aina tofauti za Reseller program kama vile:
- White label reseller ambapo unapewa bidhaa au huduma ambayo unaibrand mwenyewe na kuifanyia promotion.Wengi sana wanafanya njia hii hasa kwa kutumia China kama sehemu ya kuzalishia na kuzibrand bidhaa zao kisha wanapokuja ahapa wanazifanyia marketing na kuendelea
- Affiliate Partnership pia ni aina ya reseller ambapo wewe kazi yako inakuwa ni kuwapa wateja taarifa kuhusu bidhaa au huduma na kisha wateja wanaponunua unapewa commision fulani
Ili kufanya kazi vizuri kama Muuzaji katika maeneo haya yote unahitaji kuwa na sifa zifuatazo.
- Hakikisha unakuwa na bei maalum kwa bidha ambazo unapenda kuziuza
- Tengeneza business card yenye contact details zako na taarifa za muhimu kuhusu bidhaa zako
- Tengeneza website ambayo utaweka taarifa zako,bidha unazouza,mawasiliano na maelezo yote yanayohusu bidhaa au huduma
- Hakikisha kwa kila wiki unatenga siku tatu za kutembelea wateja wako na siku mabili za kutembelea suppliers wako ili kuhakikisha kwamba unakuwa na mawasiliano ya mara kwa mara
- Biashara za kuuza huduma za teknolojia kama software,hardware,Domain names,Hosting n.k.
- Biashara ya kuuza bidhaa kama vile make ups,Nguo,
- Biashara ya kuuza Magari,
- Biashara ya kuuza vipuri vya mitambo ya viwandani
- Biashara ya utalii,hoteli na usafiri
- Pia tunaweza kukupa mwongoz wa jinsi ya kuandaa Affiliate Program kwa ajili ya Biashara yako.