Hizi ni baadhi ya sababu juu ya kwanini hukumbuki ndoto unazoota

Hizi ni baadhi ya sababu juu ya kwanini hukumbuki ndoto unazoota

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam ,shalom!!

Mara nyingi umewahi kuota ndoto na unapoamka huikumbuki, na Hali hiyo inakupa huzuni na Kupata shauku ya kutaka kukumbuka usiweze.

Usilolijua, Ufalme wa Nuru na WA Giza, falme hizi zinaweza kuleta na kufuta ndoto nafsini mwako Kwa sababu mbalimbali. Na ndoto Si igizo au simulizi, ni tukio halisi NAFSI / Roho Yako inaona katika Ulimwengu wa Roho.

Hali hiyo hiyo ilimkuta mfalme mbabe Nebukadreza, ( Daniel 2:1-49). Mfalme aliota ndoto na akaisahau, kumbuka hapo alikuwa amewachukua pallace waisrael Daniel, Meshach, Abednego na Shadrack, sasa alipoisahau ndoto akatoa amri Waganga na waisrael wenye BUSARA na HEKIMA wauwawe ikiwa watashinda kumwambia aliota ni I usiku na tafsiri ya ndoto ni nini!!, hapo utajua nani alimwotesha na kufuta ndoto kichwani mwa mfalme na sababu, ni Ufalme wa Nuru au Giza.

Daniel kuona Hali hiyo ya hatari, akaomba Ruksa aende kumuuliza Mungu ambaye Hana kikao pamoja na wenye mwili( Waganga na wasoma nyota) ambaye Mungu huyo, wa Israel, wa Daniel ana uwezo kujua nini mtu aliota Jana na kusahau.

Ndoto ilikuwa hivi, Mfalme Nebukadreza aliona sanamu kubwa mno ya kutisha,

1. KICHWA Cha sanamu hiyo kilikuwa DHAHABU safi.

2. Kifua na mikono ni FEDHA.

3. Tumbo na viuno ni vya SHABA .

4. Miguu yake ni NUSU CHUMA NUSU UDONGO.

Daniel akampa Tafsiri ya sanamu hiyo kuwa Dhahabu ndiyo ufalme wa Nebukadreza, ufalme wake ukiweza kutawala Dunia nzima na yote ilimtii na kushikamana.

Mfalme baada ya Kupata tafsiri ya ndoto na kujua kuwa ufalme wake ni Dhahabu, yaani Imara, kesho yake akaagiza ichongwe sanamu ya DHAHABU tupu,na kuiweka na kuamrisha watu wote wakusanyike kuiabudu. Nadhani Hadi hapo, utakuwa umejua Nia ya ndoto Ile kufutwa, na nani Hasa aliifuta na ni Kwa sababu Gani.

Kwa ambao hawajaelewa Bado, tuendelee....

SABABU ZA KUOTA NDOTO NA KUZISAHAU.

1. KWA USALAMA NA AFYA YA AKILI YAKO
Kwa kuwa ndoto ni HALISI, vipo viumbe vya kiroho ukiviona na uvikumbuke, unaweza kufariki muda mfupi ujao Kwa HOFU na mawazo ndio sababu zinaondolewa kichwani mwako Ili uwe salama.

Ukifanikiwa kuiona siku ya kufa kwako ndotoni, au uione siku ya kuondolewa na uwapendao, kumbukumbu hizo Si njema, na kifo ni Fumbo, so ukiyaona hayo katika Ulimwengu wa Roho, Mungu huzifuta Ili uendelee kuwa na Amani na maisha yaendelee.

2. KUKUEPUSHA NA KOSA LINALOWEZA KUKULETEA ADHABU MBELE
Mfalme asingekumbuka ndoto, asingeamua kuchonga sanamu Ili aabudiwe na kumkosea Mungu. Hapo unaweza jua kwanini ndoto yake ilifutwa kichwani mwake. Likewise wewe nawe zipo ndoto Mungu au Ibilisi huzifuta kichwani mwako usizikimbuke Kwa sababu na Nia na makusudi Yao Kwa faida zao.

3. NDOTO ZINGINE HAZINA UMUHIMU WOWOTE
Ndoto ambazo hutokana na shughuli za Kila siku mchana, ambazo ni marudio ya uliyoyafanya mchana, hazina umuhimu wowote ndio maana nyingi huja na kuondoka na huzikumbuki na hazina impact yoyote.

4. KUKUWEKA HATARINI ILI USICHUKUE HATUA, UANGAMIE

Mungu akikuletea taarifa kupitia ndoto kuhusu Ajali uliyopangiwa na maadui zako ambayo ingetokea kesho baada ya usiku wa NDOTO, ufalme wa Giza wakifanikiwa kukuibia ndoto hiyo usikumbuke, Nia ni uache kuahirisha safari Ili UANGAMIE. Ambapo Mungu alipanga kukujulisha uahirishe Ili usiangamie.

JE, INAWEZEKANA KUOMBA KISHA UKARUDISHIWA NDOTO ULIZOOTA ZENYE MAANA, ZILIZOONDOLEWA NA ADUI ILI KUKUANGAMIZA?

Hilo linawezekana, na WA kukusaidia ni Mungu pekee ukimwomba, shetani hawezi kujua mtu aliota nini Jana, Mungu anaweza kukurudishia ndoto Ili ujue taarifa zilizoko ndani ya ndoto na hatua za kuchukua haraka kurekebisha situation mbaya.

Ukimwomba Mungu aweza yote.

Mungu awabariki.

Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako, fuatisha Sala hii,

EE, MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN

Karibuni 🙏
 
Ukiota ndoto na ukaamka asubuhi na huikumbuki ndoto hiyo,

Na ukihisi HOFU au shauku ya kuijua ndoto na tafsiri yake,

Kamwe usipuuzie,

Mwombe MUNGU, mwambie akurudishie ndoto na akupe tafsiri na akujulishe nini Cha kufanya, na Amini ukiombacho.

Uwe na HAKIKA, Malaika wa Mungu atakurudishia ndoto na kukupa yote uliyoyaomba.

UBARIKIWE 🙏
 
Kuota unamchapa mtu ambae kimaisha kawaida si mtu poa ina maana gani?
 
Kuota unamchapa mtu ambae kimaisha kawaida si mtu poa ina maana gani?
Fafanua kumchapa kivipi?

Mtu ambaye kimaisha Si mtu poa, unamaanisha nini? Ana TABIA mbaya au ni fukara?

Fafanua vizuri ulichoona bila kusahau vitu vyote ulivyoona yakiwemo mazingira, the way ulivyohisi wakati unafanya kitendo hicho, mazingira yepi, RANGI ya nguo za wahusika ndotoni nk nk🙏
 
Sio mtu poa maana yake hatuna maelewano mazuri

Alikuwa amevaa kanga amebeba mtoto wake akaongea kejeli juu yangu tukaanza kupigana baadae nikachukua fimbo na kumchapa mpaka akawa anamuita ndg yangu (marehemu) amsaidie nae akaogopa kuunga juhudi akasepa zake
 
Unamwamini Mungu na Huwa unaenda kuabudu?

Samahani lakini!!
 
Sio mtu poa maana yake hatuna maelewano mazuri

Alikuwa amevaa kanga amebeba mtoto wake akaongea kejeli juu yangu tukaanza kupigana baadae nikachukua fimbo na kumchapa mpaka akawa anamuita ndg yangu (marehemu) amsaidie nae akaogopa kuunga juhudi akasepa zake
Ikiwa u muumini na Huwa unaabudu, unatakiwa umuombee na UMSAMEHE Ili apewe neema ya wokovu Ili arudi kuwa mtu mwema mmalize tofauti zenu.

Changamoto ya ndoto hiyo IPO hapo anapoomba msaada Kwa ndugu Yako ambaye ni marehemu amsaidie.

Ikiwa nduguyo marehemu hakuwa mtu mwema, kwamba Yuko kuzimu, yaezakuwa mtu huyo unayegombana naye ni mchawi hivyo anaomba msaada wa kukuangamiza Toka kuzimu alipo huyo ndugu Yako, na haombi msaada Kwa nduguyo direct, Bali mapepo ya huko ambayo yatacgukua taarifa zako Kutoka huyo ndugu Yako, au nduguyo aweza badilishwa kuwa Malaika wa Giza na kutumia kwako aje amsaidie huyo adui Yako mchawi kukuangamiza.

Kuona huyo nduguyo hamsaidii, na kuona unamwadhibu, ni Ishara kuwa una nguvu kubwa na ulinzi kiroho.

Ikiwa ni mwombaji, ongeza bidii kuomba na kushinda vita zako Rohoni.

Lakini mwilini, tafuta Amani nae na mwombee na mshawishi aokoke ingawa katika Roho endelea Kupambana naye Ili ushinde nguvu za Giza zinazomtuma apambane nawe!!

Ubarikiwe 🙏
 
Ayubu 33:14-17

soma ukiweza tuwekee hapa
kicm nachotumiw nimeshindwa kuwekw
Pole,

Kama simu inakupa changamoto, take some time, chukua BIBLIA, quote kifungu hicho umuwekee akisome.

Hiyo ndio KAZI tuliyoitiwa mtumishi.
 
Ikiwa u muumini na Huwa unaabudu, unatakiwa umuombee na UMSAMEHE Ili apewe neema ya wokovu Ili arudi kuwa mtu mwema mmalize tofauti zenu.

Changamoto ya ndoto hiyo IPO hapo anapoomba msaada Kwa ndugu Yako ambaye ni marehemu amsaidie.

Ikiwa nduguyo marehemu hakuwa mtu mwema, kwamba Yuko kuzimu, yaezakuwa mtu huyo unayegombana naye ni mchawi hivyo anaomba msaada wa kukuangamiza Toka kuzimu alipo huyo ndugu Yako, na haombi msaada Kwa nduguyo direct, Bali mapepo ya huko ambayo yatacgukua taarifa zako Kutoka huyo ndugu Yako, au nduguyo aweza badilishwa kuwa Malaika wa Giza na kutumia kwako aje amsaidie huyo adui Yako mchawi kukuangamiza.

Kuona huyo nduguyo hamsaidii, na kuona unamwadhibu, ni Ishara kuwa una nguvu kubwa na ulinzi kiroho.

Ikiwa ni mwombaji, ongeza bidii kuomba na kushinda vita zako Rohoni.

Lakini mwilini, tafuta Amani nae na mwombee na mshawishi aokoke ingawa katika Roho endelea Kupambana naye Ili ushinde nguvu za Giza zinazomtuma apambane nawe!!

Ubarikiwe 🙏
Kuna namna umegusa kiasi flani mtafaruku ulivyokuwa mpk kufikia huko kutofautiana ila ndoto ya kuchapa watu huwa naiota sana sema hii nimeiota usiku wa kuamkia leo tu

Kutafuta amani nae sijui naanzaje mi ni mtu ambae tukiudhiana na hasa ukinichokoza nakufuta ktk maisha yangu hutoona simu yangu wala muingiliano kinamna yoyote kwahiyo kumtafuta huyo kiumbe nadhani ni ngumu
 
Kutafuta Amani naye ni kutubu Kwa niaba yake!!

Yaani kosa amekosa Yeye, ila Kwakuwa hawezi kutubu Kwa wakati huo, wewe ndio unapasa uombe Msamaha Kwa Mungu Kwa niaba yake.

Ukifanya hivyo, utajikuta unapata Amani ndani ya moyo wako, yaani hutakumbuka mabaya aliyokutendea.

Amani ndani ya moyo wako, itapeleka taarifa katika Roho, ataanza kupata ndoto nzuri na atapata HISIA nzuri juu Yako na atarudi kukuomba msamaha wewe na Amani itarudi.

Kumbuka Yesu alisema, waombeeni adui zenu na wanaowaudhi.

Mungu akubariki 🙏
 
Hapo pa kumuombea adui yako ni pagumu sana mkuu , sina kinyongo nae kihivyo wala uadui ila vijitabia vyake na kikosi chake naona kukaa mbali nao kwangu ni amani maisha yanaenda
 
  • Thanks
Reactions: apk
Kuna namna umegusa kiasi flani mtafaruku ulivyokuwa mpk kufikia huko kutofautiana ila ndoto ya kuchapa watu huwa naiota sana sema hii nimeiota usiku wa kuamkia leo tu

Kutafuta amani nae sijui naanzaje mi ni mtu ambae tukiudhiana na hasa ukinichokoza nakufuta ktk maisha yangu hutoona simu yangu wala muingiliano kinamna yoyote kwahiyo kumtafuta huyo kiumbe nadhani ni ngumu
Kwa kuwa umesema kuwa Huwa unaabudu,

Badili picha ya avatar hapo huu maana haileti utukufu wa Mungu zaidi ya kusababisha watu wasomjua Mungu kuzini moyoni waitazamapo.

Ubarikiwe 🙏
 
Hapo pa kumuombea adui yako ni pagumu sana mkuu , sina kinyongo nae kihivyo wala uadui ila vijitabia vyake na kikosi chake naona kukaa mbali nao kwangu ni amani maisha yanaenda
Ni jambo gumu sana Hilo kibinadamu,

Lakini inawezekana Kwa msaada wa Roho mtakatifu.
 
Kwa kuwa umesema kuwa Huwa unaabudu,

Badili picha ya avatar hapo huu maana haileti utukufu wa Mungu zaidi ya kusababisha watu wasomjua Mungu kuzini moyoni waitazamapo.

Ubarikiwe 🙏
Aroooo 😂😂😂mtumishi sasa unaingilia yasiyokuhusu
 
Back
Top Bottom