Pole Mkuu,chukua hatua ya kwenda hospitali kupima ili usiwe na hofu omba ufanye vipimo vyote muhimu ongea na daktari wako wazi kabisa kuhusu unavyojisikia,unachoona kwa macho kama hivyo vipele na kujikuna na hata uchovu usioisha,madaktari wana uzoefu mkubwa na ushauri mzuri sana,hutajuta,endelea kumuomba Mungu sana ukifanya toba na kuomba amani ili upokee kila kilicho mbele yako kwa uvumilivu,Mungu wetu anatupenda Sana na hakika utapokea majibu yako kwa amani yawe positive au negative maana maisha ni lazima yaendelee,Mungu akusaidie sana na akupe amani,utakuwa sawa tu ,ubarikiwe.