Hizi ni Documents Tatu (3) Zinazohitajika wakati wa kuomba TIN ya Kampuni

Hizi ni Documents Tatu (3) Zinazohitajika wakati wa kuomba TIN ya Kampuni

Luhamba II

Senior Member
Joined
Mar 22, 2025
Posts
137
Reaction score
219
Uombaji wa TIN ya Kampuni unaweza kuchukua muda mrefu kama muombaji akiwa anakosea documents au hajui ni documents gani zinahitajika.

Lakini process hii inaweza kua fupi kama muombaji akifika TRA akiwa na documents sahihi.

Kwenye Thread hii nimekuandikia documents tatu zinazohitajika wakati wa Uombaji wa TIN ya Kampuni.

1. Leese agreement/Title deed
Huu ni mkataba wa upangishaji pango au ofisi, mkataba huu utatumika kuonesha mahali ambapo kutakua ndio ofisi kuu ya Kampuni.
Title deed hii utaenda nayo ikiwa tuu wewe ni Mmiliki wa jengo ambalo ndio litakua ofisi za Kampuni.

Hapa nakushauri tutafute mwanasheria akufanyie drafting ya document vizuri ili isikataliwe TRA.

2. Katiba ya Kampuni
Hapa zinakua documents mbili Yaan memorandum of association na articles of association ambazo hizi utatumia zilezile ulizoandaliwa na mwanasheria wakati wa usajili wa Kampuni.

3. Certificate of Incorporation

Hichi ni cheti Cha Kampuni kile ulichopewa na Brela baada ya usajili wa Kampuni yako kukamilika.

TRA wakizipitia documents zako na kuona zipo sahihi watakupa forms za kujaza na Kisha watakupa TIN number ya Kampuni.

I hope this helps.

Your Favorite Lawyer.
 
what if nataka kufungua NGO nahitaji TIN na ofisi ipo kijiji ambapo hamna Title deed.
 
what if nataka kufungua NGO nahitaji TIN na ofisi ipo kijiji ambapo hamna Title deed.
Usajili wa NGO unatofautiana na usajili wa Kampuni.
Kuna mambo mengi sana ya kuelezea.
Please nicheki WhatsApp 0678131068 nikupe full consultation.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom