Hizi ni propaganda lyrics....(fid q)

Hizi ni propaganda lyrics....(fid q)

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,194
Reaction score
1,365
Machungu unapozimwa,ili ufunikwe na asiyeweza/
Mbaya zaidi wanampa Promo halafu kwenye Show unammeza/
hautaki kuwa tatizo sababu unaweza tatuka/hauwezi jua wapi nitatua ka Jiwe gizani likitupwa/
wanaficha ili nisione wakati tayari nishajua/hamkomi? igeni nione jinsi msamba mnaupasua/
hivi mnaishi ili mle au mnakula ili muishi?/
kumbuka a small leak will sink a ship/
mazingira hatarishi, Mabwana afya wanamaPesa Mob/
uswazi tunaomba mvua zinyeshe ili tutapishe vyoo/
ogopa kuoa haraka kama unaogopa talaka/
na ukivote in a hurry ujue unaproduce corruption/
maneno yao ni matamu lakini midomo yao inanuka/
ukipewa usisahau,ukitoa TOA bila kukumbuka/
usihofie kupitwa ilimradi muda haukuachi/
amini kesho itafika kama ipo ili uipate/
tunachukiana kwasababu tunaogopana/
tunaogopana kwa sababu hatujajuana/
hatujuani kwasababu tunatengana/
dunia ni nzuri.. walimwengu hawana maana/

(KIITIKIO)
Polisi wanasapoti Gangsta Rap ''ili uhalifu uongezeke''
Wabana pua kuimba mapenzi ''je itafanya ukimwi usepe''
Media zinapromoti beef ''wanadai zinakuza mziki''
Wadau wana wasanii wabovu ''nyie wakali mtatoka vipi?''
hizi ni PROPAGANDA.. usiulize ni nani?ni yupi?saa ngapi?ilikuaje?na nani?ili iweje?
hizi ni PROPAGANDA.. utaibiwa ukicheza blanda/yule last King of Scotland sio IDD AMIN wa Uganda
Polisi huniita Mzururaji na wanajua mie ni MC/
Kisha hunipa ishara kama wanavuta uradi kwa Tasbih/
Baya lisilo nidhuru ni Jema liso na faida/
nashukuru kote nasikika napotoa haya mawaidha/
kuanzia Kata,Tarafa,Wilaya,Mikoa hadi Ngazi ya Taifa/
nikifa siachi Skendo, ninauhakika nitaacha Pengo/
kwa hivi vina hata Wakulima hujikuta wanameza Mbegu/
pia ni kama Liberation struggle machoni mwa Chegu/
ukiwa mkali ka Marco Chali.. raia watafeel tu/
wajinga ndo hufa kwa wivu sababu hawako real tu/
rafiki sio urafiki usipochanganywa na Kazi/
Mlango sio mlango hadi ufungwe au uachwe wazi/
haupaswi kumuamini Muongo hata kama akiongea Ukweli/
ni Dhambi kutumia Dini kama njia ya kututapeli/
wanajiingizia kipato kwa kimvuli cha misaada/
hawatufunzi tuwe Viongozi labda Viongozi wakuwafata/
utata huja, tunapoanza kuwachunguza/
badala ya kuwafata ndipo Siri zinapovuja/
tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga/
ukishindwa kujiendesha ujue mwenyewe tu ulipenda/
kama umevutiwa na Asali, jiandae kumkwepa Nyuki/
hauwezi kumtisha kwa Mawe Adui aliyeshika Bunduki/
ni uchunguzi tu wa Kisayansi ambao haukufanikiwa/
kama ule wa Ng'ombe kula Nyasi tu halafu anatoa Maziwa/

(KIITIKIO)
Polisi wanasapoti Gangsta Rap ''ili uhalifu uongezeke''
Wabana pua kuimba mapenzi ''je itafanya ukimwi usepe''
Media zinapromoti beef ''wanadai zinakuza mziki''
Wadau wana wasanii wabovu ''nyie wakali mtatoka vipi?''
hizi ni PROPAGANDA.. usiulize ni nani?ni yupi?saa ngapi?ilikuaje?na nani?ili iweje?
hizi ni PROPAGANDA.. utaibiwa ukicheza blanda/yule last King of Scotland sio IDD AMIN wa Uganda
 
nimeinunua hiyo albam wiki iliyopita ni kali sana jamaa ndie Mfalme wa Rhymes Bongo hamna kipingamizi kabisa sema ndio hivyo HIP HOP HAIUZI
 
Huyo lazima auze kwa sababu ya ubora wa mashairi.Wasiouza ni wale wenye tungo zisizo na mvuto mfano yule diwani siijui nyimbo yake hata moja but fidq,prof j,mwanafa,joh makini,mansulii,nako2nako,motechnic,nonini&juakali utazipenda tu.
 
Hili i bonge la k2 kaka. Kuna wasanii na wanamziki bana!
 
Much respect fid we ndio king of hiphop nashangaa hawakupi tuzo ila ma **** 2 hao watoa tuzo wanampa Joh
 
nimeinunua hiyo albam wiki iliyopita ni kali sana jamaa ndie Mfalme wa Rhymes Bongo hamna kipingamizi kabisa sema ndio hivyo HIP HOP HAIUZI

Yani umenunua album alafu unasema hip hop haiuzi? Mbona wakata imetoka wadau wamechukua copy za kutosha. Na mimi ninayo ya kwangu, its the best hip hop album in Tanzania.
 
Huyo lazima auze kwa sababu ya ubora wa mashairi.Wasiouza ni wale wenye tungo zisizo na mvuto mfano yule diwani siijui nyimbo yake hata moja but fidq,prof j,mwanafa,joh makini,mansulii,nako2nako,motechnic,nonini&juakali utazipenda tu.

Huyu ndo MC pekee anayewagalagaza wakongwe wote kwa sasa. Watu wakifanya nae collabo wanaandika mistari mara 3 tatu ili tu wasifunikwe!
 
Huyo lazima auze kwa sababu ya ubora wa mashairi.Wasiouza ni wale wenye tungo zisizo na mvuto mfano yule DIWANI siijui nyimbo yake hata moja but fidq,prof j,mwanafa,joh makini,mansulii,nako2nako,motechnic,nonini&juakali utazipenda tu.
sio diwani yule ni mbunge anaitwa sugu aka mis tatuu,ni boya 2yule hajui kitu yoo
 
nimeinunua hiyo albam wiki iliyopita ni kali sana jamaa ndie Mfalme wa Rhymes Bongo hamna kipingamizi kabisa sema ndio hivyo HIP HOP HAIUZI
Mkuu Una uhakika? Au na ww unafuata Propaganda za wafu FM? mbona akina Snoopy na Master P ni matajiri au unadhani wanaimba kiduku wale? Fani yako ni kupost picha za utupu kule MYK usiongee vitu ambavyo huna uhakika navyo!
 
hapo pengine hufahamu hata wimbo wake mmoja halafu unaponda tu! pole sana!


We umezaliwa juzi unategemea utamjua Sugu?Ruge,January na Kusaga waliokula chumvi ndo wanamjua ni nani,wewe bado mtoto endelea na akina Mr. Blue wenu,kama hautajali sana tafuta kitu "ana miaka chini ya 18" waweza pata la kuongea kumhusu mheshimiwa.
 
Uzuri wa Fid amekomalia level yake,ndio maana kina Joh Makini wamekuja wamemuacha..tunaisubilia Kitaalogy Mixtape.
 
"Hawatufunzi tuwe viongozi labda viongozi wa kufuata" Inasound vizuri hasa ukiangalia na elimu inayotolewa shule za kata, kweli madogo wanafundishwa namna ya kuwafuata viongozi wao ila si wao kuja kuwa viongozi....Huwa napenda uandishi wa mashairi wa Fid Q, Jay Mo, Mwana Fa na D Knob.
 
1. Baya lisilo nidhuru ni Jema liso na faida/
2. kwa hivi vina hata Wakulima hujikuta wanameza Mbegu/
3.
Mlango sio mlango hadi ufungwe au uachwe wazi/
4. hauwezi kumtisha kwa Mawe Adui aliyeshika Bunduki/
5. wanaficha ili nisione wakati tayari nishajua/
6. usihofie kupitwa ilimradi muda haukuachi/
7. tunachukiana kwasababu tunaogopana/tunaogopana kwa sababu hatujajuana/hatujuani kwasababu tunatengana/dunia ni nzuri.. walimwengu hawana maana/.

Unajua dhana yetu ya wanafalsafa ni finyu mno..mfano watu wanafikiri Mwanafalsafa ni yule anaendika vitabu vikubwa vikubwa vyenye dhana nzito na za kufikirisha..kumbe hata mistari michache ya kufikirisha kama ya Fid Q inaweza kumfanya awe Mwanafalsafa...Kwa Roho safi na mtunuku Farid Kubanga tuzo ya Ufalsafa wa ghani za bongo kwa tungo na tenzi fupi ila za kufikirisha....
 
Tanzania hii kuna wasanii wengi lkn wanamziki wachache kama fid q kama unabisha tafuta album zake VINA MWANZO KATI NA MWISHO NA PROPAGANDA
 
sio diwani yule ni mbunge anaitwa sugu aka mis tatuu,ni boya 2yule hajui kitu yoo

Wewee ni greatsinker una akili za kuchotewa Sugu ni legend kuna msanii yeyote bongo ana albamu nyingi zenye nyimbo zenye sense ka sugu? Sio hawa kina quick raka na hao mashoga zenu albamu nyimbo sita afu 3 ni remix ya hzo nyingine kubali ukweli sugu ni legend
 
Back
Top Bottom