Hizi ni sababu za figo kushindwa kufanya kazi (kufeli)

Ndege Tai

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2020
Posts
4,439
Reaction score
8,184
Wadau tupate dondoo za Afya kidogo ili kuimarisha afya zetu na kuepukana na matatizo ya kiafya.

Sababu za figo kufeli ni zile zile ambazo zinaongelewa kila siku
1. Kula chumvi kupita kiasi

2. Kula nyama kupita kiasi,

Maana protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia ama sumu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako na kupelekea kufeli.

3. Unywaji mwingi wa Caffeine
Caffeine hutokana na Pombe, Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redbull n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo kuanza kushindwa kufanya kazi yake taratibu.

4. Kutokunywa maji

Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri. Endapo hutokunywa maji ya kutosha, sumu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, na kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo.

Baadae itapelekea kushindwa kufanya kazi vizuri na kufeli.
 
5. Kutumia madawa mengi, au makali sana.. hii hupelekea mwili kuwa na sumu ambayo pia itaathiri utendaji kazi wa figo.

6.Matumizi ya pombe kali kupita kiasi. Pombe ina tabia ya kuathiri mfumo wa water filtration katika figo. Hvyo kuathiri utendaji kazi pia
 
Hapo kwenye nyama umemaanisha nyama yoyote iwe ng'ombe kuku mbuzi pork etc au kuna baadhi ni hatari nyengine siyo hatari?
 
Hapo kwenye chumvi asee, nahisi kiwango cha chumvi nachopendelea ni kikubwa maana sehemu nyingi lazma niongeze kwenye chakula. Pia insemekana wanasema chumvi haikupikwa katika chakula ina athari zaidi
 
Kula chumvi ni nzuri kwa afya yako.
Sitegemei yeyote aliyesoma kemia aseme chumvi isiyopikwa ni mbaya. Tunachokiangalia ni minerals zilizoko kwenye chumvi yaani Iodine, Sodium, Chloride. Mwishowe hayo madini yote hakuna ambayo yanaathiriwa na heat
 
Ahaa but ngoja tupate maoni zaidi
 
Sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…