Hizi ni shule zetu za Tanzania

Hizi ni shule zetu za Tanzania

Halafu eti wanaunda tume kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne!!

Naunga mkono hoja, hata mimi sioni haja ya kuunda tume kwani ushahidi upo tele kila kona katika shule za serikali, na hasa hasa za vijijini


Over Crowding_Taifa la Kesho.jpg
 
Duh sikuwa nimeupitia huu Uzi, Hizi picha kwa kweli zinasikitisha kama sio kuhuzunisha.
Kwa Mzingira haya ya Picha kwa kweli hatutafika kabisa, kwa sababu Mtoto aka Mwanafunzi hajaandaliwa kiakili kusoma, mwanafunzi atakuwa na mawazo mengi kichwani na kuna wengine hata Mlo wa Asubuhi au Mchana hawajala.

Hapo hakuna Mwanafunzi atakayependa shule, akili zao zitakuwa ni kuenda kujishughulisha ili kujinasua na hili lindi la umasikini na hali ngumu ya maisha.

My Take: Viongozi waboreshe hii sekta ya Elimu, ni Sekta muhimu sana kwa Mustakabadhi wa Taifa letu, waboreshe kuanzia Vitabu, Majengo aka Madarasa, Mitala, Kwa walimu waboreshewe mazingira yao ya kazi na vitendea kazi. Kweli Masikini hafilisiki aka Masikini halali mchana.





Umepata ndugu yako mkuu ila unasemaje kuhusu huu uzi mkuu
 
Ni kweli Jina langu la Kikarara78 lina uhusiano na Kijiji cha Kikarara, Old Moshi, Hapo ndio nyumbani, Kumbe Kamanda aka Mkuu SUMU wewe ni Jirani aka Ndugu yangu.

Kama ni hivyo sisi ni maharawa kabisa. Nimefurahi kujua wewe ni jirani yangu.

Huwa nikirudi Moshi December kusali huwa ninasali kwenye kanisa la Roman Catholic lile lililopo nyuma ya Matemboni Primary School.
 
Kwenye issue ya madawati na madarasa ni kama sio 1999 bali kama 1985, kama wewe ni wa Kilimanjaro una haki ya kuamini kwamba kuna improvement katika sekta ya elimu hasa issue ya madawati kutokana na eneo ulilotoka. Kuna maeneo mkuu madawati wanakalia walimu tu na wanafunzi wachache na yapo mengi tu

Tuendelee kutoa ushirikiano kwa serikali mambo yatakuwa safi mkuu wangu.
 
Back
Top Bottom