Hizi nyakati sio za kutegemea cha Mtu wala Kanisa la Mtu

Hizi nyakati sio za kutegemea cha Mtu wala Kanisa la Mtu

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Watu wanaojiita watumishi wa Mungu walio wengi kwa sasa sio wa kuwaamini asilimia 100

Hata kama mtu anajua kufundisha na anaonekana kama ana Nguvu za Mungu sana usiwe mwepesi kuamini hadi pale ambapo Mungu wako atakupa ruhusa wewe binafsi kwanza.

Tafuta kumsikia Mungu wewe binafsi.

Kwanini utafute kusikia baraka na mwenendo wa Maisha yako kupitia Mtu mwingine, Utakua hatarini sana kupotezwa kabisa kwani wahongo ni wengi.

Hata kwenye maandiko Yupo nabii aliyedanganywa na nabii mwenzie kutoka mji jirani na kupelekea kifo chake kwani alidanganywa na kujikuta anavunja maagizo ya Mungu.


1 Wafalme 13:15-18
15 Akamwambia, Karibu kwangu nyumbani, ule chakula.

16 Naye akamwambia, Siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala sinywi maji pamoja nawe hapa;

17 kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, Usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.

18 Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.


Lakini watu wa leo kwenye mambo mazuri ya mwilini mnakimbilia kama kuku,

Mungu kasema Mungu kaniambi hivi na hivi.. Je ni kweli una hekima na maarifa ya kusikia Sauti ya Mungu akiongea.

Je nisauti unaisikia kwa Masikio ukiwa macho aua ni sauti gani,


Mungu akizungumza, hutumia channel ipi ya mawasiliano...


Tueleze sio unakurupuka tu na mawazo yako huko unakuja kumshauri mtu mwingine Mungu kasema kitu fulani.

Dr. Mwaka yupo Kenya huko anashusha nondo za kiroho.. spirituality inaelezewa, unapata picha vita ya ulimwengu wa roho Kati ya Nuru (mema) na Giza (maovu) ilivyochachamaa.

Nguvu ni nguvu ila nakushauri tafuta nguvu za Nuru sio za Giza.

Dr. Mwaka sijui yeye anatumia Nguvu zipi but ana information za kumfungua mtu akili zaidi.

View: https://youtu.be/y8vB-riPN4M?si=p2jJTjTRNk-Qzyef
 
Back
Top Bottom