Hizi oil perfumu za kupima zinadumu mda mrefu kama original?

Imagine kwenye top ten yako sijui hata moja, yaani achilia mbali kutumia, hata jina sijui🤣🤣🤣
Mimi majina ya perfume huwa sihangaiki nayo. Maadamu nalijua duka la kununulia na kampuni yangu pendwa naingia kwenye duka langu pendwa.

Anayehangaika na majina ya perfume ni mwenzangu na wanawake hayo ni mambo yao.

Ananisubiria labda kipindi hiki natumia aina fulani ya perfume ikiwa inakaribia kuisha anaenda kunichukulia ya aina nyengine kwenye duka hilo hilo na kampuni hiyohiyo! Utasikia mara ya kwanza ulikuwa unatumia hii kwa sasa tumia hii!
 
Wapo na Mlimani City pia...
Ajabu ile perfume yao iliyokuwa 35k sasa hivi ni 40k[emoji57]
 
Jamaa wanachezea hela kipumbavu
Hahahah!

Ndugu yangu, ukiwa na hela hata kwa mwezi ukiwa unapata millioni 7 au iwe hata ya mshahara kuna manunuzi ukiyafanya unaona ya kawaida sana.

Naweza kusema natoa 2.5 million kwenye mambo yangu mengineyo! Na 4.5 nabaki nayo!

Kwa siku ukiamua kufanya manunuzi ya million ni kitu cha kawaida.

Mimi na mke wangu tukienda kufanya manunuzi ya kununua vitu huwa tunaenda mpaka 1.9million.

Lakini hayo yanakuwa ni makorokoro. Mara nyingi huwa tunaenda mwezi 11 Mlimani City vitu huwa vimeshuka bei 😂😂😂😂.

Tutachukua mazulia ya kituruki ni mazuri. Yaani nikikaa yale najiona kama mimi Ottoman Bay. Kuna washing machine huwa zinashuka bei na za kisasa.

Kuna vitu vingi utavipata kwa wakti mmoja. Vitu bora kwa bei nafuu! Nimekupatia siri hiyo!
 
Duh kwahiyo unataka kuniambia nitafute helaa!
 
Eti Kenge aliekaangw a waja mna maneno[emoji23][emoji23]
 
[emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Yaani Mtu unatoa hadi 1.2 for perfume tu maaamaeee huko ni kukufuru? Japo naweza afford bora kukomaa tu na madeodorant for men Axe na Rexona 72 hours na elfu kumi tu.
Mimi natumia Nivea deodorant bei chee kabisa ila saivi mademu wanasema nanukia kinyama..sasa sijui hawa mademu ni wa kienyeji au vipi??

Nikihamia Dior Sauvage si ndo nitawauwa kabisa..
 
Mimi natumia Nivea deodorant bei chee kabisa ila saivi mademu wanasema nanukia kinyama..sasa sijui hawa mademu ni wa kienyeji au vipi??

Nikihamia Dior Sauvage si ndo nitawauwa kabisa..
Unatumia Nivea ipi?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…