Baada ya kusoma na kucheki video mbali mbali, nimekuja kugundua kuna dini mbili za Ukristo tu. Yaani nina maana dini ambazo zimeshika sheria za Ukristo na tamaduni zake ambazo ni Catholic Church pamoja Orthodox Christian Church.
Hizi ndo dini mbili za Ukristo tu lakini hizi Pentecostal Churchs nina mashaka nazo kabisa.
Ifike hatua kukitokea nabii katika hizi dhehebu za Kipentekoste na matendo yake ni tofauti na jinsi Biblia inavyo tuongoza ni bora aje na kitabu chake kutoka kwa Mungu wake kama manabii wengine wa kale kuliko ivi wanavyo kuja kutafsiri Biblia tofauti ni kuchafua Ukristo na kutufanya tuonekane vituko duniani kwasababu yao leo Ukristo unaonekana kituko.
Mhuni fulani akipigwa na njaa naye yeye anafungua kanisa lake anakuwa anawauzia watu mafuta na mengine kwa mgogo wa Ukristo
kanisa katoliki lisijifiche nyuma ya madhaifu ya makanisa feki ya kipentekoste. Tumeshuhudia mapadre wengi tu wakifanya mambo ya ajabu na bado wanaendelea na huduma.Tumeshuhudia watendaji wengi tu ndani ya kanisa wakifanya mambo ya aibu na kuumiza.
Hoja ya msingi ingekuwa ni kwa namna gani imani zilizopo au zinazoibuka zinaendana na maelekezo kutoka kwenye Biblia.Its clear kuwa kanisa katoliki limesema limechota mafundisho yake kutoka katika Biblia na Mapokeo matakatifu,kama ilivyo kwa dini ya ndugu zetu waislam wanachota mafundisho yao kutoka katika Quran na Hadith.
On the other hand, makanisa ya kiprotestant yakiwemo na makanisa ya kipentecoste yanachota mafundisho yake kutoka kwenye Biblia takatifu pekee. Kitu chochote ambacho kinakinzana na mafundisho rasmi kutoka kwenye Biblia takatifu hakikubaliki.Aya za Biblia zitatafsiri na aya nyingine za Biblia na sio kuongeza mapokeo mengine kuja kutafsiri yaliyoandikwa kwenye BIBLIA.
kama ambavyo kuna mapadri au watendaji wa makanisa walioleta mambo yao ndani ya kanisa na kulifanya lionekane la kishenzi,vivo hivyo kuna Pastors ambao kwa sababu ya ubinadamu wao wameleta mambo yao na kufanya makanisa yote ya Pentekoste yaonekane ya kishenzi.Hivyo basi tulihukumu kanisa katokana na msingi wake wa imani na mafundisho yake na sio kwa kumtazama mchungaji mmoja mmoja.
Makanisa ya Kipentecoste yanaamini
1. Bible as the sole authority (Hakuna kitabu kingine cha kutoa mwongozo wala ufafanuzi juu ya jambo lolote kuhusu imani)
2.Kuna Mungu mmoja nafsi tatu(Baba, Mwana na Roho Mtakatifu)
3.Tumeokolewa kwa neema na si kwa matendo ya sheria
4.Yesu Kristu ni Mungu.
5.Roho Mtakatifu ni Mungu