Niamini ninachokwambia ndugu unaweza usiamini. Passo hizi unazoona hizi. Ukitaka upate gari ndogo nzuri tumia IST ipo very economical na engine zake zipo safi kwa nguvu.
Passo usije ukajiloga. Engine yake hamna kitu.... Ni ubahiri tu ndio unatufanya tuone gari ndogo ni nafuu ila passo hapana.....
Nilifanya service nikabadili plugs zote, aircleaner, nikachange oil, na tairi mpya, ndio ikawa inacheza wastani wa hizo lita 12 na sometimes 13 kwa wastani. But nikaja kujua tatizo ni engine ndogo. Na engine za passo hazinaga nguvu.
Ukibeba watu ukawasha AC kwenye muinuko unaona kabisa gari inastruggle kupanda.... Haina nguvu. So hii ikanionyesha wazi kuwa haka kagari hakana nguvu na ndio sababu mafuta kanakula isivyo stahili.
Na pia na wenzangu kama watatu wamekuwa na experience hiyo hiyo nimeona.