Hizi ripoti mbili za CAG zinaonyesha madhaifu ya utawala wa Magufuli. Je, zinazofuata zitaruhusiwa kuonesha madhaifu ya Rais Samia?

Hizi ripoti mbili za CAG zinaonyesha madhaifu ya utawala wa Magufuli. Je, zinazofuata zitaruhusiwa kuonesha madhaifu ya Rais Samia?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kashfa nyingi za ripoti ya CAG kwa mwaka jana na mwaka huu zimetendwa wakati wa Magufuli; ndege, nishati, mashirika ya umma ikiwemo TTCL yanatuhimiwa kuiba au kusababisha upotevu wakati wa Magufuli. Hii nikutokana na ukweli kwamba maelekezo yalikuwa mengi kuliko utaratibu.

Maelekezo na speed ya Magufuli ilikuwa haizingatii sheria bali alilenga kuona matokeo makubwa kwa muda mfupi na kwa kweli tukiri kufanya kwake kwa maelekezo kulisaidia, ila side effects zake ni kukiukwa kwa sheria na hivyo kuibua hoja za non compliance ambazo ndizo zilizopamba ripoti ya CAG.

Rais Samia amekuja na compliance type of leadership na hivyo anaonekana speed yake ni ndogo. Watu wasichojua ni ukweli kwamba sheria za ununuzi zina urasimu na hivyo zinapoteza sana muda na ukipoteza muda maana yake mtoa huduma anaamini watumishi wanahitaji rushwa na hivyo nchi inayosimamia sana sheria za umma hugeuka nchi ya kitu kidogo.

This is what is happening kwenye utawala wa Rais Samia. Watu wanapenyeza rupia kuspeed up mchakato wa sheria na upataji tenda

Kwa mantiki hiyo, mfumo wa Magufuli ulizalisha sana hoja za ukaguzi tena za mabilioni na awamu ya sita imeruhusu hizi hoja ziwe public. Biswalo leo anaonekana anatakiwa kuwajibishwa lakini wakati akituhumiwa uone mfumo wa mahakama ukijitokeza kujisafisha unamsubiri mwenye serikali awasaidie kujinasua.

Hii yote inaletwa na mfumo wa Awamu ya Sita, ambao hata ukituhumiwa bado siyo rahisi kukuchukulia hatua. Hali hii ndiyo iliyopo kwenye mfumo mzima wa serikali, nifanye nisifanye hakuna wakunifanya chochote!

Katika maisha haya je, Awamu ya Sita itakubali ripoti inayofuata ambayo itakuwa na hoja nyingi za awamu hii na itatatoka kuelekea uchaguzi iwe na hoja za madhaifu yake? Kwanini tusitegemee CAG akielekezwa kuandika yale yasiyopeperusha kura?

Ningetamani kama wanavyombutua Magufuli na regime yao basi nao wakubali kubutuliwa. Tushike ripoti ikitamka madhara ya kukukopa fedha nyingi kwa lengo la kulipa Kodi. Ripoti ichunguze matumizi makubwa ya OC zinazolipwa kwa viongozi wachache wa Wizara na Idara.

Ripoti ichunguze kuchelewa kwa tenda mbalimbali kwasababu watumishi wa umma wanaamini hakuna wakuwafanya kitu. Ripoti utuambie je, wateule wa Rais wanakidhi au wamepwaya huko waliopo (capacity ya human resource), ripoti ituambie kiwango cha rushwa kilivyoongezeka nk.

Natabiri CAG kuminywa hadi uchaguzi uishe.
 
Kwani Kuna mwaka wewe unaujua ambao ripoti ya CAG iliwahi kuwa nzuri? Nitajie .

Sio swala la udhaifu wa Rais A au B ni udhaifu wa mifumo ya kitaasisi na hakuna siku ripoti itakuja kuwa nzuri kama tuu ambavyo Haijawahi mpaka hapo mifumo ya kitaasisi itakapokaa sawa ndio udhaifu utapungua.
Cheki hii hapa 👇
Screenshot_20230407-020338.jpg
 
Back
Top Bottom