WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Nimekuwa nikijiuliza toka juzi hii thread ilipoanza kwa nini usimuombe mtu wa karibu na wewe akukande? Kama unaenda salon inaweza wakandaji wa salon wakakuelewa kuwa labda una nia nyingine, kumbuka kuwa watu wengi hawana professional ethics za kudhani kuwa hii ni kazi tu nisiteghemee kuanzisha uhusiano. Sitashangaa kama nikisikia kuwa wafanya kazi hao nao wanalalamiika kuwa wateja wao wanapita mpaka kwa kutojua kuwa hiyo kazi ya kukanda ni kazi tu mteja asitegemee kitu cha ziada. Kwa kweli sijui kwa nini usimuombe mke/mume wako akukande kama unadhani kuwa salon hawatakuelewa.
Kila kazi inapaswa kuwa na maadili yake lakini katika kila kazi kuna uwezekano wa ama watendaji au wanaofuata huduma kukiuka mipaka au kutokuzingatia maadili ya kazi.Kuanzia kazi za maofisini, kwenye biashara hadi majumbani kuna kupotoka kwa namna hii.
Sasa wewe ndugu unaekwenda salon ni wajibu wako wewe mwenyewe kuweka mipaka baina yako na anayekuhudumia.Kama wewe unakuwa mwepesi kujiweka karibu na mhudumu hadi anakuita "mpenzi" na kuanza kukuomba pesa ujilaumu mwenyewe na wala usilaumu salon! Usichukie mchezaji bali chukia mchezo wenyewe!