Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu unataka tuchekwe mjini ? pamoja na hali kuwa ngumu inabidi tu-maintain lifestyle ya kiwango flani hapa mjini, unavaa vizuri, elfu 10 ya barber shop kwa wiki,simu bei mbaya hata kama unapanda daladala na`mfukoni yamejaa makaratasi lol!Achaneni na hizo "Baba Shopu", mbona kwenye zile "hea kating salun" ambazo tunanyoa kwa jero tu uswahilini hakuna hao "wajasiria mwili"?
Kuanzia Sinza Bamaga hadi Shekilango kwa haraka haraka kuna BarberShop zinazofika 20 au zaidi ya hapo
Sijawahi ona mwanaume anaenda kunyoa au kufanyiwa facial akiwa na mke wake!!
Za kike mara nyingi huwa ni kwa ajili ya umbea nani anatembea na mume wa mtu, nani kufulia, na anajishebedua ndio maana mara nyingi unawakuta wakongo wanafanya kazi mule na wanawatafutana kweli wamama na wake za watuMwenye ujuzi na zile za kike pia atujuze, je ni kusukwa tu!
Kwa vijana wa zamani watakumbuka jinsi huduma ya kunyoa nywele ilivyokuwa ikitolewa.
Kama siyo chini ya mti mkubwa wenye kivuli basi ilikuwa ni kwenye vibanda vidogo vidogo ambavyo kulikuwepo na kinyozi mmoja mwanaume.
Taratibu kwa kadri muda ulivyoendelea na utandawazi kushika hatamu, sasa tunashuhudia naweza kusema nyumba za kisasa kabisa zimejengwa ama kugeuzwa kuwa maeneo ya kunyolea nywele huku huduma nyingine za kuosha nywele,uso, kucha na nyingine kama hizo zikifanywa na akina dada tena warembo kweli kweli.
Baadhi ya hawa akina dada wamekuwa wanavaa nguo ambazo wakati mwingine zinaacha maswali mengi kwamba je ni huduma hii ya kufanya usafi wa nywele na uso ama ni zaidi ya hapo. Na zaidi ya hapo wakati wa hizi huduma wana minjonjo mingi tu kama kufungua vifungo vya shati ili waweke taulo/kitambaa, wasugue masikio, shingo,..nk.
Nawaulizeni wana-JF wenzangu, je kama uko na mai waifu wako akaona unayofanyiwa na hawa akina dada atakuruhusu uwe unakwenda peke yako? Au kama maiwaifu wako angekuwa anafanya kazi huko, ungemruhusu awafanyie wanaume wengine vile hawa akina dada wanafanya?
Na tujadili!
Ni kwanini mkuu huwa haiko hivyo?
Mkuu naona umeniita. Naam......