Hayo ya kuwategemea 100% ndio yaliyotufikisha hapa hivi sasa, hata mwanao akikuuliza kitu unashindwa kujibu kwa kuwa hukufunzwa kujishughulisha!
Japo mimi sina taaluma ya kufundisha lakini kwa sasa bila shaka mfumo wa utoaji elimu umebadilika!
Umetoka kwenye content based hivi sasa ni competence based, ambapo mwanafunzi ndiye anayepaswa kuwajibika zaidi! Mwalimu kazi yake ni kumwelekeza mtoto cha kufanya, hivyo kumtengenezea namna ya kufikiri na kutafiti zaidi!
Binafsi mwanangu anapofika nyumbani na homework ninavyoona anavyopambana kutafuta maelezo, nafurahia sana! Japo mara chache nipatapo nafasi namsaidia kidogo ila ameshazoea, na mara nyingi inabidi kitu kiwe kigumu sana ndio aulize!
Na hiyo ni baada ya kukosa majibu aliyoyaelewa maana hapendi kabisa kuandika kitu ambacho hakielewi!
Hivyo tusiwalaumu waalimu wa watoto wetu hivi sasa kwamba wanawabebesha mizigo, badala yake tuulaumu mfumo tuliopitia sisi ambao zaidi ulitufanya tuwe tegemezi pasipo kupata ujuzi wa kutosha!