Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Kusema kweli mimi home work sion shida kuwasaidia ila mtihani unakua pale mwanangu wa kwanza wa kike na yuko std5 anakuja na maswali ya ejaculation, menstrual cycle, fertilization,sex na anataka umueleze aelewe ilhali yeye mwenyewe hata kukua bado. Hapo napata shida mno mno maana naona aibu sana,najua natakiwa kuongea nae ila sio mtoto wa miaka 11 dah
 
Hehehehehee mtoe hapo mpeleke kayumba aje awe kama wewe...asiweze kufikiri zaidi
Kwa hiyo tuliosoma St Kayumba hatuna uwezo wa kufikiri?

Medium zimekuja juzi remind you......Tanzania imeanziahwa na kuendelea kujengwa na St Kayumbas
 
Pole mkuu, nilipata mtoto mmoja alikua anakuja nimfundishe class 6.
Shida niliyoona watoto wanakariri zaidi ya umahiri(uelewa)
Nilimuuliza 3X4=?
Akajibu 12
Nikamuuliza hiyo 12/4 ngapi hajui.

Kiingereza napo changamoto, inabidi atafsiri kwa kiswahili atafute jibu then alete jibu kwa kiingereza.

Social science nilikuta amejaza kilimo cha miwa ni morogoro na kapata. Nikamuuliza kwanini anafikiri morogoro ndio jibu na isiwe kisarawe, hana jibu.

Conclusion yangu nikaona changamoto tuliyonayo ni watoto kukosa umahiri zaidi ya kukariri kama kasuku na wazazi ndio tunafurahia kuona 75%and above mtoto anapata kwenye mitihani yake
 
Fikisha maoni yako kwenye vikao vya wazazi au shuleni. Hizi shule zina watu wengi ambao hawajasomea ualimu, kingereza kizuri tuu hakutoshi kufundisha
 
Yaani wanakaririshwa wafaulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…