Hizi simu....mmmh!

Hizi simu....mmmh!

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,023
Reaction score
12,811
Kwa kweli uswahilini kuna vituko, hii imetokea mtaani kwetu wikendi hii..........Jamaa katibuana na kimada wake na katika kumaliza hasira zake akaamua kumpigia simu na kumtukana huyo kimada! Sasa kwa hasira kafungua phonebook bila kuwa makini akampigia mkewe badala ya kimada na kumwaga matusi hadi akaridhika......mambo yote yakawa hadharani, jamaa hakurudi nyumbani hadi asubuhi ya jana alipokuja na mshenga na mkwewe kuyasuluhisha. Wazee wa Infidee elimu zaidi inahitajika juu ya zile sheria zenu!!
 
ha ha ha hii kali ya mwaka ni kweli yanatokea haya tetetetete
Sakata limeisha vip hili?
 
ha ha ha hii kali ya mwaka ni kweli yanatokea haya teteteteteSakata limeisha vip hili?
Wazee walitatua tatizo, japo mahusiano sio mazuri kati ya mume na mke.
 
iNAKUWAJE MTU UNAPIGA SIMU,...NA BILA YA KUSIKILIZA HATA SAUTI UNAANZA KUPOROMOSHA MANENO?
Tunatofautiana katika umakini, kwanza kosa kubwa alilofanya ni kutoangalia namba kwa umakini!
 
Always mwisho wa wizi ni kukamatwa. Waweza kuwa smart 99% kitu kidogo kikakutia nguvuni.
 
Ndo mwisho wa ubaya aibu, sasa hapo anamwangaliaje mkewe
 
ha ha haaa hizi simu hizi
kuna mtu namjua amemtuka bosi wake jana tu..
baadae ndo akaomba samahani.....yeye alidhani
ni mtu mwingine..
 
ha ha haaa hizi simu hizikuna mtu namjua amemtuka bosi wake jana tu..baadae ndo akaomba samahani.....yeye alidhanini mtu mwingine..
Ahahahaah!! Ni balaa kwa kweli usipokuwa makini.....
 
Kwa kweli uswahilini kuna vituko, hii imetokea mtaani kwetu wikendi hii..........Jamaa katibuana na kimada wake na katika kumaliza hasira zake akaamua kumpigia simu na kumtukana huyo kimada! Sasa kwa hasira kafungua phonebook bila kuwa makini akampigia mkewe badala ya kimada na kumwaga matusi hadi akaridhika......mambo yote yakawa hadharani, jamaa hakurudi nyumbani hadi asubuhi ya jana alipokuja na mshenga na mkwewe kuyasuluhisha. Wazee wa Infidee elimu zaidi inahitajika juu ya zile sheria zenu!!

Hii ni hatari. Infidel wanapaswa kuwa makini.
 
Back
Top Bottom