Hizi spana za CHADEMA; ni karma au ni hujuma?

Evolution theory huwezi ielewa kama una amini uumbaji. Muumini hahoji inakuwaje biblia hesabu ya tangu adamu mpaka leo ni miaka 6000 lakini kuna masalia ya mifupa ya binadamu ya zaidi ya miaka 3m inagunduliwa ardhini?
Carbon 14 dating that is used to calculate age of fossil is based on unrealistic assumptions that don't exist in real word. Further evolution isnt the only explanation to fossils and biodiversity. Universal flood and creation explain everything perfectly
 
Kongole sana ndugu The Palm Beach kwa mchango bora wa mwezi.
Umemaliza kila kitu.
Mods Active , Paw Maxence Melo , tafadhalini huu mchango uwekwe chini ya mchango wa mwanzisha uzi na uwe "sticky".

Majibu ya maswali mengi yanapatikana ndani ya huu mchango.
Mungu akubariki sana ndugu The Palm Beach .
 
 

Attachments

  • VID-20250527-WA0138.mp4
    6.7 MB
tatizo uongoz mpya uliwadharau waliopita, umeshindwa kuleta walioshindwa kujiona nao ni wanachadema, yaan ni sawa na chama kipya kimechukua nhi wakati ni wamoja. ukawakashifu, kuna watu wametumikia hicho chama kwa jitiada zoote, mali, jasho, leo hii unapewa uongozi unawatukana, sasa ni mda wakuonyeshena ubabe, lazima chama kirud kwa mwasisi
 
Said Issah Kobazi mnafki kuwahi tokea.
Muda wote Alikuwa Chadema zaidi ya Miaka 10 Alikuwa haoni mgawanyo kuwa Sawa ila awamu hi nyoka katoka shimoni.

Kituo kinachofuata ni Mali za Chama kushambuliwa.
 
yaani hapo unaulizwa kaswali kadogo tuu unajibu stori ndefu na bado unakosea. huu ni utumbo, jibu ni kuwa uongozi mpya uliwadharau waliopita. umeshindwa kutibu majeraha , umeshinďwa kuleta wanachadema viongoz pamoja, unajiona wao wanapendwa zaid na wananchi kuliko uongoz uliopita, fitina zimeanzia ndani, hata hivyo adui anaweza tumia udhaifu kwa kuchochea kuni tuu, ila chanza ni (dharau na matusi kwa uongozi uliopita)
 
KUna watu ni waajabu.....chadema ni balaa
 
NO REFORMS NO ELECTION NI kama UBAYA ubwela
Haturudi nyuma mpaka kieleweke
 
Umeeleza vizuri, ila ukichukulia hasira utabebeshwa zigo la misumari. Hao uliowataja sasa hivi wanalindwa na CCM, na Serikali yake kama lulu yao. Ukisema uwabinye waseme, sijui utawabinyia wapi, kwa sasa wao ni kama mboni za jicho lao. Wakipata ushahidi tu umewateka umewabinya, kelele zoote za wasiojulikana unapewa wewe, na wanakuangushia ukuta na huto amka.

Hao wameesha eleweka, waachwe, chama waendelee na njia za kupangua hizo drama huko mahakamani kama walivyotaka ccm.
 
Nini mchango wa Timu Mbowe kwenye haya?
Kujitenga kwake na chama ktk wakati kama huu..

Yeye Mbowe alipofungwa gerezani 2021 na Chura Kiziwi huyuhuyu, Mwenzake Tundu Lissu tena akiwa hospitali Leurven - Ubelgiji kwa kushirikiana na wenzake alipambana kwelikweli kumwokoa...

Yeye kimya, ishara kuwa hajali na ni mbinafsi kweli maana anaona kuwa chama kwake kwa sasa ni kama hakina faida kwake kwa kuwa hakimpi manufaa ya kiuchumi tena kama ilivyokuwa akiwa Mwenyekiti...
Maana aliyeshtaki chama kwa msajili ni Timu Mbowe, Walioishtaki chama mahakama kuu ni Timu Mbowe. Kwanini Mbowe na baadhi ya waliomuunga mkono wasihisiwe kuwa ni sehemu ya hizi hujuma?
Nisome hapo juu...

Si kwanini "asihisiwe", bali kwa trend ya matukio ni wazi kuwa anahusika kwa 100% na hujuma hizi. Kwa msemo wa Sulemani Bungara "Bwege" ni kuwa hao waliofungua kesi mahakamani (Said Mohamed, Maulida Komu nk) ni vitoto vya bata, mama yao Freeman Mbowe yuko nyuma huku watekelezaji (facilitators wa mkakati kifedha na kwa kutumia vyombo vyao Msajili wa vyama, polisi, TISS na mahakama wakiwa ni CCM)...

Na malengo ni mawili;

1. Yeye na watu wake, wanafikiri kwa kusaidiwa na CCM na dola, inawezekana chama kikarudi mikononi mwao tena

2. Wakishindwa kabisa kuupindua kwa namna yoyote ile uongozi wa Mwenyekiti Tundu Lissu, watahakikisha kile wanachokisema mara kwa mara kuwa "wamekijenga chama hiki kwa jasho na damu", wakakiharibu wakose wote au wagawane mbao kama ilivyofanyika kwa CUF. Ndio msingi wa kesi hizi zilizopo mahakamani sasa kwa kuwatumia Wazanzibari. Hata kusambaratika kwa CUF Uzanzibari na Utanganyika ndio ilikuwa silaha, kama ilivyo sasa kwa CHADEMA..

#Hii ☝🏻ya pili itawawia vigumu sana kui - execute kwa sababu scenario ya mgogoro wa CUF Lipumba vs CUF Maalim Seif Sharriff ni quite different na wa CHADEMA..

#Ni tofauti kwa sbb, CHADEMA administration mpya imeingia kwa njia ya uchaguzi halali wa kikatiba. Huyu Freeman Mbowe na kundi lake ambaye ushahidi wa kimazingira unathibitisha pasipo shaka kuwa ndiye anayeratibu vurugu hizi ktk kuudhoofisha uongozi wa Tundu Lissu akishirikiana na CCM na dola ambao ndio watekelezaji wa mikakati yote inayochorwa from within.

#Mgogoro wa CUF ulikuwa rahisi kuisambaratisha kwa sbb Prof Ibrahim Lipumba alijiuzuru uenyekiti publicly. CUF waliobaki hawakufanya waliyopaswa kuyafanya ili kuukamilisha mchakato wa kujiuzuru kwake kisheria. Baada ya hapo, CCM na dola yao wakautumia udhaifu huu kuwamaliza. Wakamtumia Registrar of Political Parties (Tendwa by then) kusema still hana document mezani kwake kuonesha kuwa Lipumba si Mwenyekiti tena wa CUF. Profesa akapigwa pesa za kutosha, akakubali kurudi kwa mlango wa nyuma kwa kukana uamuzi wake wa awali wa kujiuzuru. Vita ikaanzia hapo iliyo escalate mpaka kuigawa CUF ktk makundi mawili (CUF Zanzibar - Maalim Seif na CUF Tanganyika - Lipumba). Na kwa kuwa Lipumba Kisheria alitambuliwa kama Mwenyekiti, akamfukuza Seif na kuwa disqualified kuendeleza harakati zake kisiasa ikiwemo kuwania u Rais. Dola na CCM wakawa wamemaliza kazi yao na Seif kukimbilia ACT - Wazalendo na kuishia hukohuko...

#The same strategy iliyotumika kuisambaratisha CUF, ndo inatumika sasa kupandikiza mgogoro CHADEMA lengo ikiwa ni uwezekano wa kuileta chini, kuiangusha. Na kama nilivyosema hapo juu, kwa CHADEMA hawatafanikiwa kwa sbb mazingira ya mgogoro wa CUF ni tofauti kabisa na ya CHADEMA. Mgogoro wa CUF ulikuwa wa viongozi wakuu ndani ya chama. CHADEMA hakuna kitu kama hiki. Wanaojaribu kuleta mgogoro ni watu walio nje ya chama kabisa, hawana nafasi zozote za uongozi ukiachilia mbali Freeman Mbowe ambaye ni mjumbe wa KK, the rest ni holigans tu wasio na threat yoyote kisheria kuuleta madhara ya ki - CUF...

Wanachoweza kufanya ni kupooza kwa muda tu makali na fierceness ya CHADEMA kuikabili CCM lakini, hawawezi kufika popote zaidi ya hapo..!
 
Wako kwenye njia sahihi Oppressor atafanya yote mabaya atamaliza CDM itaendelea kusimama nakuwa washindi kadiri wanavyoipiga CDM kwa sasa ndio wanazidi kuiongezea mailage nadhani wange chagua tu mashindano ya kweli mana kwa sasa hata wana sisiemu wenye utimamu wanaona kabisa kinachooiganiwa na CDM ni kwa maslahi ya kila mtu hata kwao pia wamekua wakibanwa nakupeleleshwa kwa muda mrefu sasa wanahitaji reform ili chama chao kiendane na wakati wa sasa sio nyakati zakudanganya siku hizi kuna AI unaumbuka namba hazidanganyi lazima ujenge ushawishi kwa watu sio kujenga hofu kwa watu ambao wameshakata tamaa they have nothing to lose hawana ajira hawnana hela maisha mabovu betting ndio ajira yao ya uhakika wako frastruated elimu haina thamani tena
 
yaani hapo unaulizwa kaswali kadogo tuu unajibu stori ndefu na bado unakosea.
Onesha makosa, weka usahihi wako..

Mimi ni mtu wa fasihi (literature).

Hatuna short anwers...

Hii yote ni kuwasaidia watu mabumunda kama wewe kuelewa

Ukiwa mvivu wa kusoma, utafuga ujinga wako mpaka ukuue...
huu ni utumbo,
Utumbo una wateja pia. Wewe nunua nyama uondoke

After all, sijaona hata kama umenunua...
jibu ni kuwa uongozi mpya uliwadharau waliopita. umeshindwa kutibu majeraha
It seems that you are so stupid..

Mjinga aliyejisababishia majeraha kwa choice yake, hujitibu mwenyewe, hakuna wa kumtibu unless ametubu kusema nimekosa juu ya mbingu na nchi, ndipo aweza kupata msaada wa kumtoa ktk maangamizo yake..!!
, umeshinďwa kuleta wanachadema viongoz pamoja,
Viongozi wa CHADEMA wote kwa umoja wao wako pamoja. Wewe unaongelea viongozi gani? Hawa waliokwenda CHAKU - UUMA? Hao sio viongozi. Hao ni walikuwa normal citizens wenye choices zao kujiunga na chama chochote. Wameenda, CHAKU-UUMA, imetoka hiyo CHADEMA is stronger together..
unajiona wao wanapendwa zaid na wananchi kuliko uongoz uliopita,
Wewe unaonaje kwani? Bila shaka "hawajioni" bali CHADEMA mpya chini ya Tundu Lissu inaungwa mkono na wananchi wote. Ni wewe na tamaa na ujinga wako bado uko nyuma...!

CHADEMA corrupt, ya matapeli, wezi na wajasiriamali wa kisiasa chini ya Freeman Mbowe haipo, imehamia CHAKU - UUMA. Nenda huko wafuate..
fitina zimeanzia ndani,
Tunafahamu, huhitaji kufundisha chochote..
Ndio maana mlipuuzwa (ignored) na sasa mnaonesha rangi zenu halisi..
CHADEMA imerudi mikononi mwa wanachama na wananchi sasa. It's now really PEOPLE'S POWER...
hata hivyo adui anaweza tumia udhaifu kwa kuchochea kuni tuu, ila chanza ni (dharau na matusi kwa uongozi uliopita)
We know..

Lakini kumbuka hili.

HAKI vs DHULUMA, haki daima hushinda...

NURU vs GIZA, daima nuru hulifukuza giza...

MUNGU YEHOVA ni HAKI na ni NURU na DHULUMA siku zote ni shetani Ibilisi na ni GIZA...

Je, Shetani aweza kumshinda Mungu?

Giza laweza kuishinda nuru..?

Je, haijaandikwa mahali kuwa👇🏻👇🏻

"...Mungu wa mbingu na nchi akiwa upande wetu ni nani mwingine aweza kuwa juu yetu...?"

"...Watashindana weeee, lakini hawataweza kushinda..."

Ukipata majibu ya maswali haya, njoo nirudie nikuelimishe zaidi maana naona kichwa kimejaa ujinga mwingi sana unaosababisha ushindwe kujitambua wewe ni nani na unatakiwa ufanye nini hapa duniani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…