Hizi Tabia Zinanikera Sana

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
1.Unaegesha gari yako sehemu fulani ya mji unaendelea na shughuli zako. Ukirudi kuelekea ulikoacha gari unaona kwa mbali watu wawili watatu wamelizingira gari.Unapokaribia unaona vizuri vijana wawili wameegemea gari lako wanapiga stori. Unazidi kukaribia wala hawastuki wala nini ndo kwanza wanapigiana mikono na kucheka. Unafungua mlango unaingia na wanakutazama kama vile umewavua nguo.Ukiwasha gari kidoogo wanasogea pembeni na kushangaashangaa.Tabia mbaya sana hii!

2.Una kiplot kiko pembeni ya barabara.Umejitahidi umekizungushia nguzo na seng'eng'e
ili watu wasikatize njia.Unatembelea plot yako siku moja.Ukiwa unakagua plot unamwona mtu mwanaume anainama na kunyanyua seng'eng'e ili apate nafasi ya kupita kwa kuinama.Anafanikiwa, na huyoo anaanza kufungua zip ya suruwale na kukojoa. Anazungushazungusha macho anakuona lakini anaendelea na haja yake.Unamstua kwa kumwambia:"Eee bwana, hapo ni mahali pa kujisaidia?" Anajibu kwa sauti ya ugomvi,"Acha unoko mtu wangu! Kukojoa tu? Anakung'uta limrija lake anageuka na kuondoka. Tabia chafu sana hii.

Bila shaka zipo tabia nyingine za aina hii. Tukumbushe!
 
Haaaaaaa sikiliza kipindi cha wambura mtani,Je Uhu ni Uungwana? Kila Jumapili Saa Tatu na Nusu mpaka saa nne asubuhi.

Station:RFA 98.6 FM DSM.
 
duh . . . .
Hiyo ya kujisaidia kwenye public sevisi ni noma.
 
..upo nyumba ya wageni na mpenzi wako/nyumba ndogo.wakati mkiendelea na mazungumzo yenu chumbani,unabaini kuwa kuna jamaa anazunguka zunguka nje ya dirisha la chumba chenu.tabia inanikera sana hii.....
 
..upo nyumba ya wageni na mpenzi wako/nyumba ndogo.wakati mkiendelea na mazungumzo yenu chumbani,unabaini kuwa kuna jamaa anazunguka zunguka nje ya dirisha la chumba chenu.tabia inanikera sana hii.....
Wataalam wa chabo hao! Nao ni kero ya ajabu!
 
Mijitu inatoka huko inakojua yenyewe, alafu inakuja kutongozeana dirishani kwako tena usiku! Kama haitoshi wanashikishana ukuta hapo hapo......wanakera sana!! Aaaarrrrgh
 
Mimi hakuna kianacho nikera kama a missed call, yani mtu anakupigia na anashida yeye, afu anataka umpigie...shenzi type.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…