SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
1.Unaegesha gari yako sehemu fulani ya mji unaendelea na shughuli zako. Ukirudi kuelekea ulikoacha gari unaona kwa mbali watu wawili watatu wamelizingira gari.Unapokaribia unaona vizuri vijana wawili wameegemea gari lako wanapiga stori. Unazidi kukaribia wala hawastuki wala nini ndo kwanza wanapigiana mikono na kucheka. Unafungua mlango unaingia na wanakutazama kama vile umewavua nguo.Ukiwasha gari kidoogo wanasogea pembeni na kushangaashangaa.Tabia mbaya sana hii!
2.Una kiplot kiko pembeni ya barabara.Umejitahidi umekizungushia nguzo na seng'eng'e
ili watu wasikatize njia.Unatembelea plot yako siku moja.Ukiwa unakagua plot unamwona mtu mwanaume anainama na kunyanyua seng'eng'e ili apate nafasi ya kupita kwa kuinama.Anafanikiwa, na huyoo anaanza kufungua zip ya suruwale na kukojoa. Anazungushazungusha macho anakuona lakini anaendelea na haja yake.Unamstua kwa kumwambia:"Eee bwana, hapo ni mahali pa kujisaidia?" Anajibu kwa sauti ya ugomvi,"Acha unoko mtu wangu! Kukojoa tu? Anakung'uta limrija lake anageuka na kuondoka. Tabia chafu sana hii.
Bila shaka zipo tabia nyingine za aina hii. Tukumbushe!