Hizi Terms and conditions za UTT AMIS naziona kama kandamizi, msaada kwa anae elewa zaidi anifafanulie

Hizi Terms and conditions za UTT AMIS naziona kama kandamizi, msaada kwa anae elewa zaidi anifafanulie

Amics

Member
Joined
Aug 29, 2024
Posts
25
Reaction score
32
Baada ya kushauriwa na rafiki yangu kuhusu uwekezaji katika mifuko ya pamoja na kunielezea juu ya UTT AMIS nimevutiwa juu ya hili na kutaka kufahamu zaidi kuhusu UTT AMIS.

Katika harakati za kutafuta maarifa kuhusu UTT AMIS nikaperuzi kwa site zao niweze ona pia vigezo na masharti walivyoweka.

Niloyakuta huko ni haya.
1. Lazima uwe na account ya UTT AMIS

2. Uthibitisho wa muamala
Hapa wanadai muamala wowote utafanywa kupitia Siminvest utachukuliwa km umefanywa na mwenye account husika. Hii inamaana mwenye jukumu la kulinda taarifa za account yake ni mwenye account mwenyewe.

3. Makato ya gharama.
Kukubali kufunguliwa makato yoyote yanahusiana na huduma bila malalamiko.

4. HAKUNA UWAJIBIKAJI WA HASARA.
Kampuni inajiondoa kabisa katika uwajibikaji wa hasara yeyote itayotokea kutokana na matumizi ya Siminvest.
Inamaana hata km tatizo ni la mfumo wao bado huwezi kudai fidia

5. HAKI YA KUSITISHA AU KUKATA HUDUMA
Kwamba wanaweza kusitisha au kukata huduma muda wowote, bila sababu yoyote na bila kutoa taarifa

6. MABADILIKO YA HUDUMA BILA TAARIFA
Wanaweza badilisha taarifa au huduma zao wakati wowote bila kutoa taarifa yeyote.

7. Huduma za ulinzi.
Kwamba hawana jukumu la kudhibiti nani anaweza kufikia taarifa zako kupitia simu yako

8. Jukimu lako kutoa taarifa mala simu inapopotea, au kubadirika.

9. Ukijiunga basi umekubaliana na vigezo na masharti

Baada yakusoma haya nahisi pengine huenda sijaelewa kwamba kunauwekezaji wa njia ya sim na ya bank na terms hizo zina apply kwa simu tu?, kama nikweli terms and conditions kwa wanawekeza kupitia bank nazipata wapi.

Kama sikweli maana yake zinamuhusu kila mwekezaji na je ufafanuzi juu ya vigezo nilivyotype kwa UPPERCASE na kuwa kuweka bold ukoje?
 
Ingia kwenye website ya UTT, Pale utapata maelekezo jinsi ya kufungua akaunti zao.
 
Back
Top Bottom