Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Tumeshuhudia katika kipindi kisichozidi wiki moja, Rais Magufuli akifanya teuzi na tengua, za nafasi zaidi ya mia moja, katika nafasi zake za uteuzi, kama vile maRC, maDC, maDAS, maDED nk.
Kitu ninachoweza ita imeleta sintofahamu kubwa yote hiyo na kuweza kuiita ni "vurugu mechi" za teua na tengua hizo, kiini chake ni hao wateule wake, kwenda kuchukua fomu na kutaka kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM.
Hebu sasa tuangalie hivi ni kweli anachofanya Mheshimiwa Rais Magufuli ni sahihi kwa kutengua nafasi zao hao wateule wake?
Tuangalie sasa kauli zake za awali za Rais wetu ili tuone kama kweli yuko sahihi au laa, katika teuzi hizo na tengua.
Niseme wazi kuwa kauli zake za "ndimi mbili" za Mheshimiwa Rais, ndizo zinazoleta "confusion" yote hii ndani ya nchi yetu
Hebu turejee katika kauli zake, alizowahi zitoa siku za nyuma.
Tuanze na kauli yake aliyowahi itoa siku za nyuma, kuwa katika serikali yake, akishakutengua, basi usitegemee tena kuteuliwa katika nafasi yoyote ile ya uteuzi wake, kwa kuwa wapo watu wengi sana wenye sifa, walioko kwenye "waiting list"
Lakini wananchi tunashuhudiia namna ambavyo Rais wetu anavyokula matapishi yake kwa kuwarejesha watu wake wale wale, aliowatengua siku za nyuma, tena kwa kuainisha makosa yao kibao ya kutengua huko!
Tuje kwenye hizi teuzi zilizoshika "headlines" zinazoendelea sasa za wale watumishi wa Umma, waliokwenda chukua fomu za kugombea nafasi za ubunge.
Huu "utitiri" wa watia nia wa CCM umetokana na kauli zake, kwa kuwa tulimsikia kwa masikio yetu, akiwahimiza wateule wake, wakati akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM, uliomazika siku za karibuni, akiwahimiza waende majimboni kwao, waende wakagombee nafasi hizo na yeye hatakuwa na pinganizi za kuwanyima ruksa!
Vile vile hebu tuangalie hii kauli yake aliyotoa sasa hivi kuwa yeye hajatuma mtu yeyote kwenda gombea nafasi ya ubunge mahala popote nchini.
Hivi ni nani ambaye amesahau, kuwa Rais anapofanya ziara zake mbalimbali, amekuwa akiwapigia debe la waziwazi kabisa, watu "wake" mbalimbali, wakagombee ubunge huko majimboni kwao?
Hivi Mheshimiwa Rais, anadhani kuwa tumesahau namna ambavyo amekuwa akitumia ushawishi wake, kuwasihi wananchi kwenye maeneo yao, wawachagulie pendekezo lake?
Hivi amadhani tutakuwa tumesahau namna ambavyo aliwashawishi wakazi wa Kongwa na Kilosa, wawachagulie watu "wake" Spika Ndugai na Profesa Kabudi?
Hivi anadhani huu "utitiri" wa watia nia ya hawa wasanii "wavaa milegezo" hautokani na kauli zake za kuwahimiza wakagombee ubunge majimboni kwao?
Hivi anadhani Mheshimiwa Rais wananchi tutakuwa tumesahau, namna alivyo-mpampu msanii Harmonize akagombee kwenye jimbo lake la Tandahimba?
Ingekuwa vyema Mheshimiwa Rais, kama alivyosema kwenye hotuba yake ya karibuni kabisa wakati wa kuwaapisha wateule wake kule Chamwino, kuwa anaviachia vikao vya maamizi vya wajumbe wa majimboni kwao, kwani hao ndiyo waamuzi wa mwisho wa kuteuliwa kwenu ubunge kwa tiketi ya CCM na kuwa wao Kamati Kuu wataidhinisha mapendekezo hayo ya majimboni kwao