Uchaguzi 2020 Hizi teuzi na tengua ninazoweza ziita kuwa ni za "vurugu mechi" za Rais Magufuli zinaipeleka wapi nchi yetu?

Uchaguzi 2020 Hizi teuzi na tengua ninazoweza ziita kuwa ni za "vurugu mechi" za Rais Magufuli zinaipeleka wapi nchi yetu?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Tumeshuhudia katika kipindi kisichozidi wiki moja, Rais Magufuli akifanya teuzi na tengua, za nafasi zaidi ya mia moja, katika nafasi zake za uteuzi, kama vile maRC, maDC, maDAS, maDED nk.

Kitu ninachoweza ita imeleta sintofahamu kubwa yote hiyo na kuweza kuiita ni "vurugu mechi" za teua na tengua hizo, kiini chake ni hao wateule wake, kwenda kuchukua fomu na kutaka kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM.

Hebu sasa tuangalie hivi ni kweli anachofanya Mheshimiwa Rais Magufuli ni sahihi kwa kutengua nafasi zao hao wateule wake?

Tuangalie sasa kauli zake za awali za Rais wetu ili tuone kama kweli yuko sahihi au laa, katika teuzi hizo na tengua.

Niseme wazi kuwa kauli zake za "ndimi mbili" za Mheshimiwa Rais, ndizo zinazoleta "confusion" yote hii ndani ya nchi yetu

Hebu turejee katika kauli zake, alizowahi zitoa siku za nyuma.

Tuanze na kauli yake aliyowahi itoa siku za nyuma, kuwa katika serikali yake, akishakutengua, basi usitegemee tena kuteuliwa katika nafasi yoyote ile ya uteuzi wake, kwa kuwa wapo watu wengi sana wenye sifa, walioko kwenye "waiting list"

Lakini wananchi tunashuhudiia namna ambavyo Rais wetu anavyokula matapishi yake kwa kuwarejesha watu wake wale wale, aliowatengua siku za nyuma, tena kwa kuainisha makosa yao kibao ya kutengua huko!

Tuje kwenye hizi teuzi zilizoshika "headlines" zinazoendelea sasa za wale watumishi wa Umma, waliokwenda chukua fomu za kugombea nafasi za ubunge.

Huu "utitiri" wa watia nia wa CCM umetokana na kauli zake, kwa kuwa tulimsikia kwa masikio yetu, akiwahimiza wateule wake, wakati akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM, uliomazika siku za karibuni, akiwahimiza waende majimboni kwao, waende wakagombee nafasi hizo na yeye hatakuwa na pinganizi za kuwanyima ruksa!

Vile vile hebu tuangalie hii kauli yake aliyotoa sasa hivi kuwa yeye hajatuma mtu yeyote kwenda gombea nafasi ya ubunge mahala popote nchini.

Hivi ni nani ambaye amesahau, kuwa Rais anapofanya ziara zake mbalimbali, amekuwa akiwapigia debe la waziwazi kabisa, watu "wake" mbalimbali, wakagombee ubunge huko majimboni kwao?

Hivi Mheshimiwa Rais, anadhani kuwa tumesahau namna ambavyo amekuwa akitumia ushawishi wake, kuwasihi wananchi kwenye maeneo yao, wawachagulie pendekezo lake?

Hivi amadhani tutakuwa tumesahau namna ambavyo aliwashawishi wakazi wa Kongwa na Kilosa, wawachagulie watu "wake" Spika Ndugai na Profesa Kabudi?

Hivi anadhani huu "utitiri" wa watia nia ya hawa wasanii "wavaa milegezo" hautokani na kauli zake za kuwahimiza wakagombee ubunge majimboni kwao?

Hivi anadhani Mheshimiwa Rais wananchi tutakuwa tumesahau, namna alivyo-mpampu msanii Harmonize akagombee kwenye jimbo lake la Tandahimba?

Ingekuwa vyema Mheshimiwa Rais, kama alivyosema kwenye hotuba yake ya karibuni kabisa wakati wa kuwaapisha wateule wake kule Chamwino, kuwa anaviachia vikao vya maamizi vya wajumbe wa majimboni kwao, kwani hao ndiyo waamuzi wa mwisho wa kuteuliwa kwenu ubunge kwa tiketi ya CCM na kuwa wao Kamati Kuu wataidhinisha mapendekezo hayo ya majimboni kwao
 
Hata hii kauli aliyowahi itoa Mwenyekiti kuwa kura za maoni za wajumbe wa majimbo si lolote wala chochote safari hii, kwa kuwa itategemea yeye Mwenyekiti kaamkaje siku hiyo ya kikao cha Kamati Kuu, kwa kuwa yeye ana uwezo wa kuwakata wagombea wote walioshika nafasi za juu na kuwarudishia jina, ambalo ni chaguo lake yeye Mwenyekiti ili ndiyo awe mgombea wa kiti cha ubunge.

Hivi kwa kauli hiyo, bado tu wananchi tutaendelea kumwamini yeye Mwenyekiti kwa kauli yake kuwa hana mtu hata mmoja aliyemtuma akagombee ubunge?
 
Umeiba ukaficha kisha ukasahau umeficha wapi!
 
Umeandika vema sana. Bado watu pia wana vidonda mioyoni kuhusu kuchukuliwa fomu moja tu ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Hii haina udikteta wa mwenyekiti ndani yake?!?
 
Mshika mawili lazima moja likuponyoke
Watu mnalalamika hakuna ajira,walio na ajira wanalalamika hawapandi vyeo
Hii ni safi nenda kagombee ili wengine wapate ajira,wengine wapande vyeo
 
Kikatiba ya nchi hana...........

Ila kwa kuwa nchi yetu hivi sasa inaendeshwa kama gari bovu na Jiwe anapenda "kujimwambafai" ndiyo ameamua kutupeleka kukote kule anakotaka yeye!
Anayo hayo Mamlaka. Onesha kifungu kinachomkataza
 
Huo utaratibu anaofanya Mhe. Rais upo sahihi kwa asilimia [emoji817] kwa mujibu wa miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma. Miongozo inasema mtumishi yeyote akitaka kwenda kugombea nafasi ya kuteuliwa kugombea ubunge anatakiwa kuomba likizo ya bila malipo na endapo atateuliwa kuwa mgombea kupitia chama chochote basi utumishi wake utakuwa umekoma rasmi kuanzia siku ya kuteuliwa kwake.

Mtu anapoomba likizo bila malipo kwa kawaida nafasi yake huwa haiachwi wazi, vinginevyo basi we mwajiri unakuwa ulifanya overstaffing kiasi kwamba mtumishi anaondoka na pengo lake kutoonekana. Na kwa mujibu wa miongozo na kanuni za utumishi wa umma ni kuwa mtu akiomba likizo bila malipo na endapo atataka kurejea kwenye utumishi, mwajiri wake atamchukua endapo tu kuna nafasi wazi ya taaluma hiyo kwenye Ikama ya mwajiri. Nadhani wengi mmeelewa. Rais hana kosa, mtumishi anaruhusiwa kwenda kugombea chama chochote na utaratibu ni huo ulioelezwa hapo. Aidha, utaratibu huu hauwahusu mawaziri kwasababu wao Ofisi zao kuu ni majimbo, hivyo hawahitaji kuomba ruhusa bila malipo.

Wanaolalamika humu mitandaoni nadhani ni wale ambao wamepoteza vyeo vyao na hawana uhakika wa kuteuliwa kupeperusha bendera za vyama vyao, so wana wasi wasi kibarua kitaota nyasi. Ukweli ni kwamba wahitaji wa nafasi hizo wapo wengi sana, wasijedhani wao pekee ndio walikuwa qualified kutumikia nafasi hizo. Mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote
 
Kutokana na ubovu wa uendeshaji wa nchi anajikuta anamaliza muda wake wengine ahajawapa fadhila. So anajaribu kukimbizana na muda.
 
Teua, tengua, teua tena. Hii ni tabia ya mtu ambaye hayuko connected.
You have a problem somewhere, Unataka unavowaza wewe ndio iwe hivyo hivyo. Kwa haraka nikikutazama wewe ungekuwa rais ungekuwa mvunja sheria mzuri sana, maana nimekuonesha fact bado unapinga.
 
Back
Top Bottom