Tetesi: Hizi tuhuma ni nzito sana, kama ni kweli, hii ‘chain’ itapeleka wengi gerezani kwani ni sawa na uhaini

Tetesi: Hizi tuhuma ni nzito sana, kama ni kweli, hii ‘chain’ itapeleka wengi gerezani kwani ni sawa na uhaini

troiker

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
1,551
Reaction score
2,573
Wengi wataona Mbele ya Pazia kama Mwandishi Kabendera anaonewa, ila kiukweli yaliyojificha ama mambo yanayofanywa na kabendera nyuma ya pazia Sio ya kiungwana, na yanapaswa kulaaniwa na kila mtanzania anayeipenda nchi hii.

Yapo Mengi ila yanawekwa bayana kwa uchache angalau watanzania Mjue sio kwamba Polisi wanaonea watu bali wanajitoa kuhahikisha uhai wa Taifa hili Tukufu la TZ unadumu.

Yataelezwa mambo makuu mawili, kimsingi mambo hayo yapo nyuma ya mashitaka yanayomkabili 1.Utakatishaji Fedha 2. Uraia
1.Utakatishaji Fedha..

Baada ya kunyimwa tenda na serikali ya awamu ya 5 ,kampuni 3 za kibeberu kutoka kwenye mataifa yenye nguvu, yalianzisha jitihada za makusudi, za kumkwamisha Rais JPM, na Kuchafua taswira nzima ya serikali yake.

Lengo lao kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapoteza imani kwa Raisi ,ili hadhi yake ya urais iyeyuke na baadaye waweke mtu wao.

Kampuni hizo zilisuka mpango kabambe, zikatengeneza vikundi ambavyo vinahusisha wazawa na wasio wazawa, pia ikaundwa mifumo maalumu ya namna ya kuvifadhili.

Mifumo hii ya ulipaji ,iliwalazimisha wakuu wa mkakati huu (Mabeberu) kuwatumia wazawa ,na hapo ndo likaja wazo la kuwaajili (Recruit) Eric Kabendera na mjasiriamali Maarufu nchini(Anawekwa kapuni hadi wakati wake utakapowadia).

Kazi kubwa ya Kabendera ikawa ni kuhakikisha kuwa pesa ambayo itatumika kwenye kazi haramu (Kumuhujumu Rais na Serikali yake) inaingizwa kwa kupitia mifumo halali.

Kabendera akawa anaingiziwa pesa nyingi kama mwandishi wa kujitegemea, fedha ambazo kimsingi hazilingani na kazi anazozifanya,

Kabendera kwa mwezi ikawa anaingiziwa dola za kimarekani zisizopungua 95000, ambazo ni takribani milioni 200 za kitanzania na zaidi.

Fedha hizi alizokua akiingiziwa Kabendera, ndizo ambazo zilikua zinatumika Kulipa vikundi mbalimbali ambavyo vimezuka hususani mitandaoni ,kukwamisha kila jema alifanyalo Mh Rais.

Kila kikundi kina mkuu wake ambaye ndiye anawajibika kupokea tunu kutoka kwa Kabendera, Wakuu hawa ambao wamo wanasiasa na wengine wanaharakati uchwara, (Wanaharakati wenye ajenda ya pembeni tofauti na wanachojinasibu kukipigania).
Baada ya kupokea bahasha za tunu ,wao huwapatia vijana walio chini yao posho ndogo ndogo za vocha .

Vijana ambao ndo wengi, wakishapokea pesa hii ndogo huwa kama mbogo waliojeruhiwa, huweka data ,huingia online na kuanza kumtusi,Kejeri,Ongopea, beza na kumdhihaki Rais kwa kila namna wanayoweza.

Wengi wanafanya sababu ya njaa, hawajui wanaharibu amani ya taifa letu kwa maslahi ya nani.

Hivi ndivyo Kabendera hutakatisha mamilioni ya Fedha kuhakikisha Rais aliyejitolea kusimamia rasilimali za Watanzania anapotezwa, na nchi inaendela kuliwa na wachache kama iivyokua desturi hapo kabla.

Mlinzi wa Kweli ni Mungu watanzania tuzidi kumuombea JPM wakwame wao kabla
 
Mkuu ulichukua muda gani kuwaza hii na kuiandika? I mean tangu kupanga mawazo yako kuyahariri hadi kushika keyboard na kuanza kuandika hivi?

Anyway lililo kubwa kabisa, tena kubwa sana ni hiyo sentensi yako ya mwisho kabisa. SIJUI HATA KWANINI UMEIANDIKA HAPA!
 
Sijui kuhusu huyo uliyemtaja lakini kuna mtu ambaye ni kama rafiki kwangu aliniambia yupo in dillema kwa sababu amefuatwa na watu wa nje kumuhaidi hela nyingi ili kuandika tafiti na makala za kuchafua serikali. Ni mtu aliyekuwa hata kulipa kodi ya nyumba huko tegeta ilikuwa inakua shida sana. Lakini ndani ya miezi mitatu akamaliza nyumba yake iliyomchukua miaka sita kumaliza. Akanunua magari mawili. Akaoa mke na wakaenda in an exotic island for honeymoon etc. Nilikuwa siamini haya mambo aisee, ila yapo sana. Watu wanakua wabinafsi na myopic sana na kukosa uzalendo.
 
Back
Top Bottom