Kama umetumwa basi kawaambie hatuja shawishika mana tunaakili sio kama wanavyo tufikiria.Wengi wataona Mbele ya Pazia kama Mwandishi Kabendera anaonewa ila kiukweli yaliyojificha ama mambo yanayofanywa na kabendera nyuma ya pazia Sio ya kiungwana na yanapaswa kulaaniwa na kila mtanzania anayeipenda nchi hii.
Yapo Mengi ila yanawekwa bayana kwa uchache angalau watanzania Mjue sio kwamba Polisi wanaonea watu bali wanajitoa kuhahikisha uhai wa Taifa hili Tukufu la TZ
Yataelezwa mambo makuu mawili, kimsingi mambo hayo yapo nyuma ya mashitaka yanayomkabili 1.Utakatishaji Fedha 2. Uraia
1.Utakatishaji Fedha..
Baada ya kunyimwa Tenda na serikali ya awamu ya 5 kampuni 3 za kibeberu kutoka kwenye mataifa yenye nguvu yalianzisha jitihada za makusudi za kumkwamisha Rais JPM na Kuchafua taswira nzima ya serikali yake.
Lengo lao kubwa ni kuhakksha Rais anapoteza imani kwa wananch wake na hadh yake ya urais inayeyuka na baadaye anawekwa mtu wao.
Kampuni hizo zilisuka mpango kabambe, zikatengeneza vikundi ambavyo vinahusisha wazawa na wasio wazawa, pia ikaundwa mifumo maalumu ya namna ya kuvifadhiri.
Mifumo hii ya ulipaji iliwalazimisha wakuu wa mkakati huu (Mabeberu) kuwatumia wazawa ,na hapo ndo likaja wazo la kuwaajili (Recruit) Eric Kibendera Na mjasiriamali Maarufu nchini(Anawekwa kapuni hadi wakati wake utakapowadia).
Kazi kubwa ya Kibendera ikawa ni kuhakikisha kuwa pesa ambayo itatumika kwenye kazi haramu (Kumuhujumu Rais na Serikali yake) inaingizwa kwa kupitia mifumo halali.
Kabendera akawa anaingiziwa pesa nyingi kama mwandishi wa kujitegemea, fedha ambazo kimsingi hazilingani na kazi anazozifanya,
Kabendera kwa mwezi ikawa anaingiziwa dola za kimarekani 95000 ambazo ni takribani milioni 200 za kitanzania na zaidi.
Fedha hizi alizokua akiingiziwa Kabendera, ndizo ambazo zilikua zinatumika Kulipa vikundi mbalimbali ambavyo vimezuka hususani mitandaoni ,kukwamisha kila jema alifanyalo Mh Rais.
Kila kikundi kina mkuu wake ambaye ndiye anawajibika kupokea tunu kutoka kwa Kabendera, Wakuu hawa ambao wamo wanasiasa na wengine wanaharakati uchwara, (Wanaharakati wenye ajenda ya pembeni tofauti na wanachojinasibu kukipigania).
Baada ya kupokea bahasha za tunu ,wao huwapatia vijana walio chini yao posho ndogo ndogo za vocha .
Vijana ambao ndo wengi, wakishapokea pesa hii ndogo huwa kama mbogo waliojeruhiwa, huweka data ,huingia online na kuanza kumtusi,Kejel,Ongopea, beza na kumdhihaki Rais kwa kila namna wanayoweza.
Wengi wanafanya sababu ya njaa, hawajui wanaharibu amani ya taifa letu kwa maslahi ya nani.
Hivi ndivyo Kabendera hutakatisha mamilioni ya Fedha kuhakikisha Rais aliyejitolea kusimamia rasilimali za Watanzania anapotezwa, na nchi inaendela kuliwa na wachache kama iivyokua destruri hapo kabla.
Mlinzi wa Kweli ni Mungu watanzania tuzidi kumuombea JPM wakwame wao kabla.
Magereza na vyombo vya sola vyote awamu hii vinakazi moja, yaani vijuu yawale wote au kitendo chochote cha kumkosoa Raisi kuliko usalama na ustawi wa wananchi wake. Sisi tunajua kuwa Magu akihisi kuwa wewe ni hatari kwa uraisi wake ( hatakama hatari hii ni ndani ya sheria za nchi) atatumia vyombo vyetu vya dola kuku angamiza kwa maslahi yake binafsi katika kutawala kimabavu.
Kinacho sikitisha ni kuona anataka kutuhusisha wananchi kwa kusingizia kuwa mtu huyo ni hatari kwa taifa. Sio marayakwanza wakosoaji wake na serikali yake, kuwasingizia kuwa wanaitukana nchi na watanzania wake, wakati ukweli yeye ndo mlengwa, anatujumuisha wote ili tumtetee bila kujua.