Tetesi: Hizi tuhuma ni nzito sana, kama ni kweli, hii ‘chain’ itapeleka wengi gerezani kwani ni sawa na uhaini


Hawawezi kujionyesha waziwazi hawa sio ndugu zako acha upofu. Kwani kule Kongo, Somalia , Libya, Afghanistan walishasema wao ndio tatizo? Wakikuta mbulula kama ninyi na wenzio unaowatetea basi wanawatumia kama toilet paper wakishavuruga nchi wanakuacha kuwa makini
 
Unaweza kuweka hio bank statement ya Kabendera?
 
Kwa mwendo huu,Na yule jamaa mwenye jina la mwisho linalofanana na la Mwalimu ajiandae,haiwezekani auze vitabu mil 200 kwa mwezi kwenye mtandao wa mabeberu,anatakatisha fedha tu
 
Kama kuna nchi ambayo usije ukajidanganya kuwa utaweza kufanya Mipango yako Ovu ( Mibaya ) dhidi yake hasa ukilenga Kuuchafua Uongozi uliopo / Mamlaka iliyopo kwa Maslahi yako pamoja na hao wanaokutuma basi ni hii yetu ya Tanzania. Na ili uone kuwa Tanzania pia ina Watendaji Nyeti Wastaarabu na Waungwana kabisa huyu huyu Mwandishi nimedokezwa na Mtu kutoka huko huko kuwa baada ya Kugundulika anachokifanya alishafuatwa na Watu kama Wawili hivi ambao ni Wabobezi kama Yeye katika hiyo Tasnia ( japo Wao sasa wapo huko Idara Muhimu ) wakimsihi kuwa aachane Kutumika kwani ameshajulikana nadhani kwa Jeuri ya hizo Pesa na Kiburi cha hao waliokuwa wakimtumia akawa anawaonyesha dharau ( ukichanganya na ile ya Kabila lake ) na akiwaambia kuwa haogopi chochote / lolote lile. Na labda tu asichokijua huyu Mwandishi ni kwamba kati ya Watu ambao wamefanikisha Yeye Kukamatwa Kwake hivyo na hadi sasa kuwa Matatani hivi ni wale wale Marafiki zake, Wanaharakati na Wanasiasa baadhi kwa kutoa details zake za ndani kabisa halafu cha Kushangaza ili uone kuwa Watanzania tumebarikiwa kwa Sifa ya Unafiki ndiyo hao hao leo hii wanajifanya Kukimbilia Mitandaoni Kumtetea kuwa aachiwe huru na wengine wakijifanya Kuhudhuria Mahakamani hadi Kumpa Mkono wakati Kiuhalisia kumbe ni wao wao ndiyo wamemmaliza. Matatizo mengine huwa tunajitakia wenyewe na kamwe usimuamini Mtu yoyote bali jiamini tu mwenyewe.
 
Hivi wakati unaandka hili,KICHWA CHAKO ULIKIACHA WAPI?
1.CHOONI
2.KWA MKEO?
 
Na wewe hii umeambiwa au umechimba?! Tupe source
 
Chaka la viongozi wadhalimu ni kubambikizia wakosoaji kesi!
 
Mtu mchafu unawezaje kumchafua?

Mtu aliyekwama unawezaje kumkwamisha?

Yule mwenye kuudhi ndiye huchukiwa!
Yule mwenye kukera ndiye huchukiwa!

Kwa mwenye njaa Kipande cha mkate kinathamani kubwa kuliko mgodi wa dhahabu.
 
Nyie mtakuwa ni wazee lazima, bado mkono kwenye karne hii ya 21 mnaongelea siasa za mabeberu mambo ya karne iliyopita!?
ndugu, kwani mabeberu hawapo? na madikteta hawapo? kipi kwenye karne hii ambacho hakikuwepo karne zilizopita??? maana asilimia kubwa ya mifumo inayotumika leo iligunduliwa kwenye makarne hayo yaliyopita - me hata sioni jipya naona kama historia zinajirudia rudia tu hata ukora unaofanyika kwa pande zote ni ule ule ni nguvu zinataka kubaki madarakani kwa kivuli cha wananchi na nguvu zinataka watoke madarakani kwa kivuli cha wananchi maana wananchi ndo pawn wao, wasikusumbue wote wale wale tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…