Tetesi: Hizi tuhuma ni nzito sana, kama ni kweli, hii ‘chain’ itapeleka wengi gerezani kwani ni sawa na uhaini

Joined Yesterday , umejiunga JF kwa lengo la kutakatisha ishu ya Kabendera tu ! Aibu sana !
 
mwongo mkubwa weeee!
 
Hili andiko lako ni UPUMBAVU tu. Labda uweke hapa ushahidi wa malipo ya hizo pesa. Hakuna mtanzania anaweza kupokea hizo pesa kama unavyodai kirahisirahisi hivyo. Wewe ni punguani kama walivyo punguani wengine huko Lumumba.
 
Jamani kelele zinawatesa Hawa...wanajitetea kijinga...na ben ametumiwa na Nani?azory?wa virobani?,injinia lwejaba?nchi yetu sote hii acheni kutuletea laana!! tunahitaji kuvitengenezea mazingira Mazuri vizazi vyetu kesho vitunenee Mazuri juu ya makaburi yetu!!huu ni upuuzi.hii yote ni kwa ajili ya naniiii!!?
 
Ila mtambue ya kwamba zama zimebadirika, wafuasi wa chama dola jaribuni kuwa na ubunifu wa kutengeneza propaganda zinazolandana na wakati tulionao, watanzania wameelimikia ijapokuwa si wengi na kutambua mambo yanayoendelea hapa duniani. Maana hii propaganda ni sawa na ile usichague wapinzani maana watawaletea machafuko nchini. Kabendera hakuna anayemlipa kwa ajili ya kutaka kumuaribu magufuli katika utawala wake isipokuwa JPM anajiharibia mwenyewe..

Mfano Mimi sipendezwi na Magufuli pamoja na serikali yake kwa mambo mengi lakini linalonipa kinyongo zaidi kuzuia pesa nilizokuwa nachangia kwenye mfuko ya hifadhi ya jamii kwa kuniondolea fao la kujitoa na kuniwekea hilo fao la kukosa ajira, kwa mantiki hiyo vijana wanaotaka kujikwamua kiuchumi ndo wamekwama na ukizingati kuna janga kubwa la ukosefu wa ajira kwa wananchi. Je mimi ntakuwa napewa pesa EK kwa kuikosoa serikali na utendaji wake?? Jibu hapana,JPM ameharibu future za vijana wengi walio kwenye sekta ,serikalini na wakina sie tunaotaabika mitaani.

-Mwambie kuwa watu hawatoacha kulalamika mitandaoni/sehemu mbalimbali hapa nchini kama hatojirekebisha kufanya yalio sahihi(uhadilifu) kwa wananchi wake,kama kusemwa
Walisemwa waja wema waliotangulia kabla yake,yeye ni nani mpaka asiambiwe,tutamkosoa pale anapokosea kwa lengo la kujenga na tutamsifia panapostahili pongezi

Ndugu zangu tuache kusujudia viumbe (binadamu)wenzetu ambao wanasifa zinazofanana na zetu, kama kwenda haja wote tunakwenda.hata kama tunatafuta vyeo ama kulipwa fadhila na wapenda kusujudiwa sio hivyo, tujifunze kutokuwa watumwa wa kifikra

Naipenda nchi yangu Tz.
 
Dooh makubwa jamaa anajilia tu akuna lenye mwanzo lisilo kuwa na mwisho japokuwa mwisho unatuadhiri wote
 
Hii ni post ya tatu sasa kuhusu Eric, ambayo kama mbili zilizotangulia ni uthibitisho mwingine kuwa Idara yetu ya Usalama wa Taifa imeshiwa kabisa na mbinu kiasi cha kuwategemea vichwapanzi wa MATAGA kuja kufanya porojo mtandaoni.

Ukweli kuhusu Eric upo wazi: anadhaniwa kuwa na nyaraka zilizopelekea mauaji ya kinyama ya Injinia Mwijabe - ambaye watu wa Kitengo wakiongozwa na Nyaulingo walimteka, wakamtesa, wakambaka kisha wakamuua. Wakati hayo yanatokea, Eric alikuwa ameitwa Dodoma kubanwa kuhusu "nyaraka alizopewa na marehemu Mwijabe."

Kwanini nyaraka hizo zimepelekea Mwijabe kuuawa na Eric kukamatwa? Ili kuelewa suala hili unapaswa kufahamu wadhifa wa marehemu hapo Hazina. Alikuwa kitengo cha EU ambacho pamoja na mambo mengine kinaratibu fedha za misaada kutoka EU.

Sasa hii ni siri ya wazi kwamba kuna ufisadi mkubwa unaoendelea hapo hazina ambapo yule mpwa wa Mzee Meko anafisadi pesa atakavyo kwa vile licha ya kuwa mpwa wa Meko, pia alimwaga pesa zake nyingi kwenye kampeni ya mwaka 2015, pesa alizofisadi TANROADS wakati Mjomba wake akiwa Waziri wa Ujenzi.

Marehemu Mwijabe na Eric walikuwa partners katika kampuni binafsi ya usadi (consulting).

Wanamshikilia Eric kwa sababu moja kuu: hawajafanikiwa kupata hizo nyaraka ambazo zilikuwa zifikishwe kwa nchi na taasisi mbalimbali wahisani, zikionyesha kinagaubaga jinsi fedha zao zinavyofisadiwa hapo Hazina.

No wonder Marekani, Uingereza na Canada zimeshaonyesha kukerwa kwao na uonevu anaofanyiwa Eric. Siku chache zijazo, EU inatarajiwa kutoa msimamo wake kuhusu suala hilo.

Tuweke hayo kando. Mtoa mada aeleze kwamba kama Eric alikuwa "mhaini" anayetumiwa na Mabeberu, kwanini Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa ina-outsource analyses ya taarifa mbalimbali kwa mwandishi huyo? Tunalazimika kuweka hadharani siri hizi kwa sababu sio uungwana hata kidogo "kumtumia" kisha kumchafua. Eric hakutumiwa na Idara kwa sababu ya pesa bali (a) he is extremely intelligent (b) has extensive international connections (c) UZALENDO wake (he used to be in the army kabla ya kuwa mwanahabari).

Tukiweka hilo kando, kama Eric alikuwa "mhaini" kwanini mara kadhaa Mzee Meko aliagiza taarifa kutoka kwa mwanahabari huyo?

Lakini kubwa zaidi, iweje "uhaini" wa Eric uje mara tu baada ya mshirika wake Mwijabe kutekwa, kuteswa, kubakwa na hatimaye kuuawa na Nyaulingo na wenzake? Why now?

Na kama tuhuma hizo za kipuuzi zingekuwa za kweli, kwanini kwanza ilielezwa kuwa Eric amekamatwa kuhusiana na immigration status yake kisha ikadaiwa ni cybercrime kabla ya kumbadilishia kesi na kudai ni mhujumu wa uchumi?

Tell you what, nyote safari yenu ni moja kama ya Nyaulingo. Ni suala muda tu.
 

Amejiunga ana siku 2, ndio kitengo mpya kaja na kasi ya moto mabua.
 
Mabeberu sio watu, ni vema serikali iwekeze kwenye tafiti juu ya mbinu zitumiwazo na mabeberu ku distabilise mataifa machanga. Hilo likifanyika tutajua mbinu za kapambana na kuwazuia. R I P Patrice Lumumba nawengine Kama Nkuruma etc
 
Wengi wetu tukichapa maji ya mende angalau tunaweza kutumia lugha ya malkia ktk kuchangia uzi kama huu.

I feel big danger, indeed daunting when start thinking about hidden propaganda towards issues which are supposed to be next of none. Equally, in my logical equations for my own understanding can be taken as material thing in articulating the subject in matter.

I believe the matter concerned with Mr. Kabendera can not be circumscribed by details of those allegations leveled against him per se, of which in any case, can be taken as the effective tool to intimidate his freedom of expression.

With the vouch of veracity, this seems to be the Achilles' heel of the concealed political agenea and state rooted juggernaut, that seems to be vividly sceptical to his work of art as an self centered journalist.
 

Umejiunga una siku 3 ndio unakuja na story za kitoto, yaani umeajiriwa kitengo ndio umeonekana unaweza kupika propaganda mfu. Kwa bahati mbaya watu walishaamka Muda mrefu wanawachora tu.
 
Mabeberu sio watu, ni vema serikali iwekeze kwenye tafiti juu ya mbinu zitumiwazo na mabeberu ku distabilise mataifa machanga. Hilo likifanyika tutajua mbinu za kapambana na kuwazuia. R I P Patrice Lumumba nawengine Kama Nkuruma etc

Nyie mtakuwa ni wazee lazima, bado mkono kwenye karne hii ya 21 mnaongelea siasa za mabeberu mambo ya karne iliyopita!?
 
Mtu kama ni msafi utaonekana tu hata watu wakuchafue vipi usafi wako utakutetea popote ingawa pia vice versa is also true.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…