Wengi wataona Mbele ya Pazia kama Mwandishi Kabendera anaonewa ila kiukweli yaliyojificha ama mambo yanayofanywa na kabendera nyuma ya pazia Sio ya kiungwana na yanapaswa kulaaniwa na kila mtanzania anayeipenda nchi hii.
Yapo Mengi ila yanawekwa bayana kwa uchache angalau watanzania Mjue sio kwamba Polisi wanaonea watu bali wanajitoa kuhahikisha uhai wa Taifa hili Tukufu la TZ
Yataelezwa mambo makuu mawili, kimsingi mambo hayo yapo nyuma ya mashitaka yanayomkabili 1.Utakatishaji Fedha 2. Uraia
1.Utakatishaji Fedha..
Baada ya kunyimwa Tenda na serikali ya awamu ya 5 kampuni 3 za kibeberu kutoka kwenye mataifa yenye nguvu yalianzisha jitihada za makusudi za kumkwamisha Rais JPM na Kuchafua taswira nzima ya serikali yake.
Lengo lao kubwa ni kuhakksha Rais anapoteza imani kwa wananch wake na hadh yake ya urais inayeyuka na baadaye anawekwa mtu wao.
Kampuni hizo zilisuka mpango kabambe, zikatengeneza vikundi ambavyo vinahusisha wazawa na wasio wazawa, pia ikaundwa mifumo maalumu ya namna ya kuvifadhiri.
Mifumo hii ya ulipaji iliwalazimisha wakuu wa mkakati huu (Mabeberu) kuwatumia wazawa na hapo ndo likaja wazo la kuwaajili (Recruit) Eric Kibendera Na mjasiriamali Maarufu nchini(Anawekwa kapuni hadi wakati wake utakapowadia) Kazi kubwa ya Kibendera ikawa ni kuhakikisha kuwa pesa ambayo itatumika kwenye kazi haramu (Kumuhujumu Rais na Serikali yake) inaingizwa kwa kupitia mifumo halali ,
Kabendera akawa anaingiziwa pesa nyingi kama mwandishi wa kujitegemea fedha ambazo kimsingi hazilingani na kazi anazozifanya, Kabendera kwa mwezi ikawa anaingiziwa dola za kimarekani 95000 ambazo ni takribani milioni 200 Za kitanzania na zaidi. Fedha hizi alizokua akiingizwa Kabendera ndizo ambazo zilikua zinatumika Kulipa vikundi mbalimbali ambavyo vimezuka hususani mitandaoni kukwamisha kila jema alifanyalo Mh Rais
Kila kikundi kina mkuu wake ambaye ndiye anawajibika kupokea tunu kutoka kwa Kabendera, Wakuu hawa ambao wamo wanasiasa na wengine wanaharakati uchwara (Wanaharakati wenye ajenda ya pembeni tofauti na wanachojinasibu kukipigania). Baada ya kupokea bahasha za tunu wao huwapatia vijana walio chini yao posho ndogo ndogo za vocha .
Vijana ambao ndo wengi wakishapokea pesa hii ndogo huwa kama mbogo waliojeruhiwa huweka data huingia online na kuanza kumtusi,Kejel,Ongopea, beza na kumdhihaki Rais kwa kila namna wanayoweza.
Wengi wanafanya sababu ya njaa hawajui wanaharibu amani ya taifa letu kwa maslahi ya nani
Hivi ndivyo Kabendera hutakatisha mamilioni ya Fedha kuhakikisha Rais aliyejitolea kusimamia rasilimali za Watanzania anapotezwa na nchi inaendela kuliwa na wachache kama iivyokua destruri hapo kabla.
Mlinzi wa Kweli ni Mungu watanzania tuzidi kumuombea JPM wakwame wao kabla.
Hii ni post ya tatu sasa kuhusu Eric, ambayo kama mbili zilizotangulia ni uthibitisho mwingine kuwa Idara yetu ya Usalama wa Taifa imeshiwa kabisa na mbinu kiasi cha kuwategemea vichwapanzi wa MATAGA kuja kufanya porojo mtandaoni.
Ukweli kuhusu Eric upo wazi: anadhaniwa kuwa na nyaraka zilizopelekea mauaji ya kinyama ya Injinia Mwijabe - ambaye watu wa Kitengo wakiongozwa na Nyaulingo walimteka, wakamtesa, wakambaka kisha wakamuua. Wakati hayo yanatokea, Eric alikuwa ameitwa Dodoma kubanwa kuhusu "nyaraka alizopewa na marehemu Mwijabe."
Kwanini nyaraka hizo zimepelekea Mwijabe kuuawa na Eric kukamatwa? Ili kuelewa suala hili unapaswa kufahamu wadhifa wa marehemu hapo Hazina. Alikuwa kitengo cha EU ambacho pamoja na mambo mengine kinaratibu fedha za misaada kutoka EU.
Sasa hii ni siri ya wazi kwamba kuna ufisadi mkubwa unaoendelea hapo hazina ambapo yule mpwa wa Mzee Meko anafisadi pesa atakavyo kwa vile licha ya kuwa mpwa wa Meko, pia alimwaga pesa zake nyingi kwenye kampeni ya mwaka 2015, pesa alizofisadi TANROADS wakati Mjomba wake akiwa Waziri wa Ujenzi.
Marehemu Mwijabe na Eric walikuwa partners katika kampuni binafsi ya usadi (consulting).
Wanamshikilia Eric kwa sababu moja kuu: hawajafanikiwa kupata hizo nyaraka ambazo zilikuwa zifikishwe kwa nchi na taasisi mbalimbali wahisani, zikionyesha kinagaubaga jinsi fedha zao zinavyofisadiwa hapo Hazina.
No wonder Marekani, Uingereza na Canada zimeshaonyesha kukerwa kwao na uonevu anaofanyiwa Eric. Siku chache zijazo, EU inatarajiwa kutoa msimamo wake kuhusu suala hilo.
Tuweke hayo kando. Mtoa mada aeleze kwamba kama Eric alikuwa "mhaini" anayetumiwa na Mabeberu, kwanini Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa ina-outsource analyses ya taarifa mbalimbali kwa mwandishi huyo? Tunalazimika kuweka hadharani siri hizi kwa sababu sio uungwana hata kidogo "kumtumia" kisha kumchafua. Eric hakutumiwa na Idara kwa sababu ya pesa bali (a) he is extremely intelligent (b) has extensive international connections (c) UZALENDO wake (he used to be in the army kabla ya kuwa mwanahabari).
Tukiweka hilo kando, kama Eric alikuwa "mhaini" kwanini mara kadhaa Mzee Meko aliagiza taarifa kutoka kwa mwanahabari huyo?
Lakini kubwa zaidi, iweje "uhaini" wa Eric uje mara tu baada ya mshirika wake Mwijabe kutekwa, kuteswa, kubakwa na hatimaye kuuawa na Nyaulingo na wenzake? Why now?
Na kama tuhuma hizo za kipuuzi zingekuwa za kweli, kwanini kwanza ilielezwa kuwa Eric amekamatwa kuhusiana na immigration status yake kisha ikadaiwa ni cybercrime kabla ya kumbadilishia kesi na kudai ni mhujumu wa uchumi?
Tell you what, nyote safari yenu ni moja kama ya Nyaulingo. Ni suala muda tu.