Hizi zinazoitwa connection ni nini? Je, ni jina sahihi linavyotumika huko?

Hizi zinazoitwa connection ni nini? Je, ni jina sahihi linavyotumika huko?

Cprah

Member
Joined
Jul 31, 2022
Posts
5
Reaction score
3
Kuna mambo mengi yanaendelea huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hili la connection limepamba moto, kwanza kwanini huu udhalilishaji unaitwa CONNECTION? Inaconnect nini na nn? kwanini inaitwa connection ya flani? binti au kijana au mzee mwenye jina lake flan bin fulani

Kwanini jamani kwanini mambo yasiyofaa tunayapea kipaumbele kulikiko mambo mengine? Kwanini ni fahari kudhalilisha mtu na mtu mwingine yupo tayari kuona utupu wa mwingine kwa malipo ya aina yoyote
Tukijaribu kujipea nafasi za hawa wanaofanyiwa hivi, tutaweza kweli kuvumilia ukiachana na umaarufu wao, wao pamoja na wengine wana familia wana ndoto hatuoni kama hii kitu inaathiri sana akili na maisha ya watu.

Wapo wengi ambao hatuwajui wamepoteza kazi na hawata ajiriwa kutokana na kuwepo kwa picha ambazo huwenda hawakujua kuwa zinachukuliwa wakati wa tendo hakuna namna nyingine ya watu kupata pesa jamani?

Yani mtanzania yupo radhi asile chakula asifanyie pesa yake kitu cha maana ili mradi tu alipe pesa aone utupu wa mtu mwingine ambae kama Mungu angeamua kubadilisha mambo huyo unayehangaika kuona utupu wake awe mama yako, shangazi yako au hata dada au mdogo wako basi hata iwe wewe umechukuliwa ukiwa hujui wallah usinge stahimili ungehisi ni kudhalilika ungehisi nikufedheheshwa.

Kuna haja gani ya haya yote laiti kama serikali ingetilia mkazo kutokuwepo kwa biashara ambazo zinaruhusu watu wafanye hivi watu wasingerekodi wenzao wala kujirekodi ila kwa sababu ni biashara na watu wanalipwa basi mtu na akili zake timamu yupo radhi aaribu maisha ya mwenzake na familia yake kwa kumrekodi mwenzake na kumpatia mtu mwingine au kuchukua za mwingine aliyejirekodi na kuwapa wengine.

Tunawaumiza hawa watu jamani watoto wao wataishi je baada ya haya ,wazazi wao wataweka wapi sura zao na katika yote maisha yao uchumi wao utakuwaje.

Inaweza isiwe na tija sana kwa wenzangu waislamu ila vuta picha mdada mkristo uliyemvujishia video yake(baada ya na akiwa hafahamu chochote) kanisa linamtazamaje? Basi sawa ulimwambia kwamba unamrekodi akakubali sawa kwanini uvujishe mambo ambayo n ya faragha. Ingekuwa n sawa kuvujisha basi watu wangekuwa wanafanya hizo mambo hata stendi au kwenye madaraja kwanini wanahitaji usiri kwa sababu ni baina ya wawili.

Wallah Hata Dini hairuhusu kwenda hata kuchungulia wafanyao usiri huu hairuhusu na Quran inasema ni dhambi na ni imani yangu hata biblia inasema vivyo hivyo, tunapotakiwa kusema tuseme tena wa nguvu,tufanye sehemu zetu jamani dada zetu, mama zetu ndugu zetu na rafiki zetu wamedhalilika mno na wataendelea kudhalilika tukilifumbia macho hili jambo.

Allah atupe kukinai na kujihisi wenye hatia kwa kuyaharibu maisha ya wengine kwa ajili ya fedha na anasa ya muda mfupu.
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake, ebu iyo connection tuione kama ni kweli au na ww unaleta kahawa hpa
20220623_045935.jpg
 
Namimi napenda kuiona hiyo connection kwanza Ili nichangie hoja kwa mapana, iweke hapa
 
Ni ushenzi wa kiwango kikubwa sana, Ila kwa wa TZ hawaoni tatizo lolote mpaka yawafake either Dada yake au mtoto wake ndipo atakapojua huo ubaya wake.
 
Mwandishi wa bandiko kamabuna koneksheni tugawie,tugawane dhambi hizo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom